LIVERPOOL WAILEMEA PSG

Liverpool walinyakua bao la dakika za lala salama na kuifunga Paris Saint-Germain ugenini 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano, wakati Bayern Munich waKichukua usukani kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya wapinzani wa Ujerumani, Bayer Leverkusen. Vinara wa ligi ya Ufaransa PSG walitawala uwanjani […]

AFISA ‘ALIYEUAWA’ MAJENGO AFUTWA KAZI, POLISI

Afisa wa polisi anayedaiwa kufyetua risasi na kusababisha kifo cha mvulana mwenye umri wa miaka 17 mtaani Majengo jijini Nairobi amepokonywa bunduki na kusimamishwa kazi huku uchunguzi zaidi ukiendelea. Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa idara ya polisi Michael Muchiri, ambaye amewataka wenyeji kushirikiana na maafisa wa idara DCI na kitengo cha kushughulikia masuala […]

SHOKA LA KK, FURAHA YA ODM

Katika kile kinachoonekana kama kuwaadhibu wandani wa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, mrengo wa Kenya Kwanza umewatimua kutoka uongozi wa kamati mbali mbali katika bunge la kitaifa, chama cha ODM kikiratibiwa kunufaika pakubwa na uongozi wa kamati hizo. Kwenye mageuzi hayo, mbunge wa Embakasi North James Gakuya ameondolewa kutoka uwenyekiti wa kamati ya biashara, Gathoni […]

POLISI KUIMARISHA OPERESHENI MATUNGU, KIRINYAGA

Wakazi wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na utovu wa usalama wanatarajia kupata afueni kufuatia hakikisho la serikali kutangaza operesheni maalum katika maeneo hayo kwa lengo la kukabili magenge ya kihalifu. Baadhi ya maeneo hayo ni Kerugoya na Ngurubani kaunti ya Kirinyaga, Matungulu na Matungu kaunti za Machakos na Kakamega mtawalia. Hata hivyo, akizungumza akiwa katika bunge […]

UTULIVU WAREJEA MAJENGO NAIROBI

Utulivu umeanza kureja katika eneo la Majengo karibu na soko la Gikomba jijini Nairobi kufuatia makabiliano mapema leo kati ya polisi na kundi la vijana lililozua vurugu kulalamikia mauaji ya kijana mmoja, wanayesema alipigwa risasi na polisi wa kituo cha California kufuatia tofauti kati ya polisi na kundi la watu wanaosemekana kuwa wauzaji wa mihadarati. […]

BADILISHENI SHERIA ZA VYAMA VYA KISIASA, NATEMBEA

Katika juhudi za kulinda nafasi ya upinzani na kuhakikisha uwazi, bunge la kitaifa limetakiwa kufanyia marekebisho sheria inayohusu miungano ya vyama vya kisiasa baada ya uchaguzi. Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama waliogura chama cha Ford Kenya na kujiunga na DAP-K, gavana wa Trans Nzoia George Natembea, amesisitiza haja ya kuwepo kwa sheria inayozuia vyama vya […]

UKRAINE TAYARI KUZUNGUMZA NA URUSI- TRUMP

Huenda vita ambavyo vimedumu kwa miaka 3 kati ya Urusi na Ukraine vikafikia kikomo baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutangaza kwamba yuko tayari kwa mazungumzo na Urusi na ukamilishaji wa mkataba wa uchimbaji madini na serikali ya Marekani. Hatua ya Zelensky kukubali mazungumzo imewekwa wazi na mwenzake wa Marekani Donald Trump, ambaye amethibitisha […]

NANDI, RED CROSS ZASHIRIKIANA

Juhudi za kukabili majanga katika kaunti ya Nandi zimepigwa jeki kufuatia hatua ya serikali ya kaunti hiyo kutia saini mkataba wa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu unaoweka mikakati ya kukabiliana na majanga katika kaunti hiyo. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kuipa jamii uwezo wa kukabili majanga na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Imetayarishwa […]

ARSENALI WAIADHIBU EINDHOVEN

Vijana wawili wenye talanta wa Arsenal Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri waliungana Jumanne kusaidia The Gunners kushinda 7-1 katika hatua ya 16 ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven. Kikosi cha Ligi ya Premia kilikuwa katika kiwango tofauti ukilinganisha n ahiki cha ligi ya mabingwa na kilipelekea kuwazaba PSV […]

OLOUCH APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa timu ya mpira wa vikapu ya Chuo Kikuu cha Africa Nazarene (ANU Panthers) MichaelOluoch anaamini kuwa timu yake bado haijapata mdundo tangu kuanza kwa msimu wa ligi ya mpirawa vikapu ya wanawake. Wanafunzi hao hawajashinda mchezo wowote kufikia sasa hata walipoteza 34-51 dhidi ya USIUFlames wikendi wikendi katika uwanja wa Nyayo Gymnasium, […]