ONGEZEKO LA DHULUMA UASIN GISHU LATINGA WASIWASI

Waathiriwa wa dhuluma katika Kaunti ya Uasin Gishu wanazidi kuteseka, huku Wawakilishi Wadi wa Kike wa Bunge la Kaunti wakilaani vikali kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji. Viongozi hao wanatoa wito kwa wadau wa jamii kushirikiana kukomesha ukatili huu na kuhakikisha waathiriwa wanalindwa dhidi ya madhila zaidi. Imetayarishwa na Janice Marete

PSG YALAZA LIVERPOOL

Ushindi wa Paris Saint-Germain wa mikwaju ya penalti dhidi ya Liverpool Jumanne katika mechiya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kauli ya ushindi kwa klabu hiyo mpya ya Ufaransa katika enzi zabaada ya Kylian Mbappe na inathibitisha kwamba wanawania sana kushinda kombe hilo. PSG zamani walikuwa karibu kuchekwa kote Ulaya kwa uwezo wao wa kupoteza mechi […]

TULIKOSA KUDHIBITI MCHEZO ASEMA KOCHA GENGA

Timu ya mpira wa vikapu ya Chuo Kikuu cha Nairobi, UON Terror, kocha mkuu Eugene Gengaametaja ukosefu wa uthabiti kuwa sababu kuu iliyowafanya kupoteza pambano lao la wikendidhidi ya Umoja. Wanafunzi hao walipoteza 64-75 katika mechi ya Ligi Kuu ya Kitaifa ya Wanaume iliyochezwakwenye Uwanja wa Nyayo Gymnasium.Genga pia ametaja usumbufu ambao haukutarajiwaambao uliyumbisha utulivu […]

KOCHA WA NZOIA ATAJA MAKOSA YA KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa Nzoia Sugar FC, Charles Odero ametaja makosa ya safu ya ulinzi kuwa sababukuu ya kushindwa kwao 3-1 na Naivas FC kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Kitaifa (NSL) Jumamosi. Kipigo hicho, ambacho kiliashiria kushindwa kwa Nzoia kwa mara ya kwanza mwaka huu baadaya ushindi wa kuvutia wa mechi tano mfululizo na sare […]

KOCHA SIMWA APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Kocha wa timu ya Raga ya Shule ya Sekondari ya Senende Boys, Peter Simwa anasema kuawalijitihadi kwa michezo ya Shule za Sekondari Kanda ya Magharibi wikendi iliyopita. Senende Boys nusura wafuzu kwa hatua ya kanda wakiwa mabingwa watetezi pekee kwa VihigaBoys kuangusha Senende 17-0 katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa Nyang’ori Boys. Hata hivyo, Simwa […]

OMANYALA KUONGOZA KIKOSI CHA KENYA KWA MICHEZO ZA ASA GRAND PRIX

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika, Ferdinand Omanyala ataongoza msururu wamfululizo wa ASA Grand Prix, tukio la World Athletics Continental Tour Challenger,linalopangwa Jumatano, Machi 13, katika Uwanja wa Pilditch mjini Tshwane, Afrika Kusini. Omanyala, mshikilizi wa rekodi ya Afrika mita 100, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwawapinzani wake Mark Odhiambo, bingwa wa zamani wa Afrika […]

RUTO ‘APIGA JEKI’ MASOMO MATHARE

Shughuli za masomo katika shule ya upili ya St. Theresa’s Mathare zimepigwa jeki baada ya Rais William kutoa ufadhili wa shilingi milioni 5 kufanikisha ujenzi wa bweni la wanafunzi na uchimbaji wa kisima cha maji. Rais ametoa ufadhili huo kwenye siku yake ya pili ya ziara ya kaunti ya Nairobi, ambako pia amezindua ujenzi wa […]

MZOZO WA ARDHI: WAKAZI MAKUENI WAHAMAISHWA

Serikali ya kaunti ya Makueni imetoa hamasisho kwa wakazi kuhusiana na sheria za urithi wa ardhi kama njia mojawapo ya kumaliza mizozo ya ardhi ambayo imekithiri kwenye kaunti hiyo. Imebainika kuwa wengi wa wakazi hawana hatimiliki za mashamba wanamoishi kutokana na ukosefu wa ufahamu kuhusu utaratibu wa kupata stakabadhi hizo. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CHANGAMOTO ZA MDHIBITI WA BAJETI

Uhaba wa fedha katika afisi ya mdhibiti wa bajeti ya serikali ndicho kikwazo kikubwa katika utendakazi wa afisi hiyo. Haya ni kwa mujibu wa mdhibiti wa bajeti hiyo Margaret Nyakang’o, akiwa mbele ya kamati ya fedha katika bunge la seneti ambvako amesema mara nyingi hulazimika kutekeleza nusu ya majukumu. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KWA KUMBUKUMBU ZA CARLES MINARRO

Kocha wa Barcelona Hansi Flick amesema timu yake itamenyana na Benfica kwenye Ligi ya Mabingwasiku ya Jumanne ikiwa ni mchezo wa kumbukumbu kwa daktari wa klabu Carles Minarro, aliyefarikiJumamosi. Miamba hao wa Catalonia wanaongoza kwa bao 1-0 katika mechi ya 16 bora kutoka kwa mkondo wakwanza mjini Lisbon kabla ya pambano hilo kwenye Uwanja wa […]