WAWAKILISHI WA KENYA WAANZA MICHUANO YAO IJUMAA

Wawakilishi watatu wa Kenya katika Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika ya mpira ya wavu Wanawake mwaka huu wataingia dimbani Ijumaa mjini Abuja kufuatia droo iliyofanyika Alhamisi usiku katika mji mkuu wa Nigeria. Kenya Prisons, ambayo ilishinda taji la bara mara ya mwisho mwaka wa 2013, iko Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Zamalek ya […]

“MNADANGANYWA!”- MUTURI AMSUTA RUTO

Kutimuliwa kwangu kutoka baraza la mawaziri kulitokana na msimamo wangu kuhusu visa vya utekaji nyara na mauaji ya kiholela nchini na wala si kushindwa na majukumu jinsi mnavyoambiwa. Ndiyo kauli ya aliyekuwa waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi, akizungumza na wanahabari siku moja baada ya kuondoka rasmi afisini, akiendelea kukosoa visa hivyo. Muturi amemtaka […]

ODM YAJITENGA NA MADAI YA UPINZANI

Chama cha ODM kimekana madai ya baadhi ya viongozi wanaoegemea mrengo wa Azimio kwamba kinahitilafiana na mchakato wa kubuniwa upya kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, kikilaumu chama cha Wiper kutokana na kucheleweshwa kwa mchakato huo. ODM kupitia kwa katibu wake mkuu Edwin Sifuna imejitenga na madai hayo kwenye kikao na wanahabari baada […]

WAKULIMA WAPATA AHADI YA MBOLEA KUTOKA KWA SERIKALI

Wakulima wamehakikishiwa upatikanaji wa mbolea ya kutosha katika ghala za Halmashauri ya Nafaka na Mazao (NCPB), kufuatia tamko la Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo, Mutahi Kagwe. Akizungumza katika soko la ESP, Naromoru, kaunti ya Nyeri, Kagwe amesema serikali imejizatiti kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo bora kwa bei nafuu, huku akieleza kuwa hitaji la mbolea […]

RAIS RUTO AENDELEA KUKWEA

Rais William Ruto ameendelea na ziara yake ya maendeleo kwa siku ya pili katika eneo la Mlima Kenya ambako amezindua miradi mbali mbali anayosema itasaidia kubadilisha Maisha ya wakazi wa eneo hilo. Kaunti za Meru na Kirinyaga ni maeneo ambako Rais anazuru hii leo, akikariri kuwa urafiki wake na eneo hilo utasalia kuwa imara. Rais […]

ZETECH YASHINDWA KUINGIA KWA FAINALI YA RAGA

Kocha mkuu wa Zetech Oaks Ramsfield Matekwa ameelezea masikitiko yake baada ya wachezaji wake kushindwa kutinga mchujo wa fainali ya Ubingwa ambayo ingewahakikishia nafasi ya kuingia ligi kuu ya raga msimu ujao. Oaks walikuwa wakitafuta kufuzu kwa ligi kuu kwa mara ya kwanza lakini wakabwagwa 41-9 na Chuo Kikuu cha Masinde Muliro (MMUST) RFC. Matekwa […]

EQUITY DUMAS WAWAGWARA WANA BENKI

Kocha mkuu wa Equity Dumas, Zadock Adika yuko na furaha baada ya timu yake kuwanyamazisha wanabenki National Bank Dumas walikuwa katika hali nzuri, kwa kuwalaza Benki ya Taifa ya Kenya 72-59 katika mechi ya ligi kuu ya wanaume iliyoandaliwa katika uwanja wa Nyayo Gymnasium. Wakati huo huo, mtaalamu huyo mwenye sauti ya upole anajivunia uchezaji […]

WAZIRI KHATUNDI ASHUTUMIWA MT. ELGON

Kundi la akina mama kutoka eneo bunge la Mlima Elgon kaunti ya Bungoma wameitaka tume ya uwiano na utangamano NCIC kumchukulia hatua za kisheria waziri wa kilimo kaunti ya Trans Nzoia Phanice Khatundi kutokana na matamshi yake wanayosema inawadhalilisha. Wakiongozwa na Jemimah Temko, wamesema licha ya juhudi za kukabili unyanyapaa dhidi ya akina mama wa […]