BRANDON OBIERO AWEKA LENGO LA KIPA BORA ZAIDI NCHINI

Kipa wa Tusker, Brandon Obiero, anasema anatamani kuwa miongoni mwa makipa bora nchini baada ya kupata nafasi ya kuanza mechi mbili mfululizo kwenye Ligi kuu ya Kenya. Obiero ameanza dhidi ya Mara Sugar na Ulinzi Stars, akihifadhi clean sheet katika mechi zote mbili ambazo Tusker ilishinda 1–0. Mchezaji huyo aliyejiunga na Tusker mwanzoni mwa msimu akitokea […]

OKAKA AINGIA ROBO FAINALI YA DUNIA BAADA YA USHINDI MKUBWA DUBAI

Bingwa wa taifa wa uzani wa light heavyweight, Robert Okaka, anaendelea kung’ara kimataifa baada ya kutinga robo fainali ya Mashindano ya Dunia ya Ndondi  kwa Wanaume yanayoendelea Dubai, ambapo atakutana na Mrusi Bizhamov Dzahambulat. Okaka amesema anaendelea na utulivu na kujiamini, akisisitiza kuwa mtazamo wake haujabadilika licha ya kupanda kiwango cha ushindani. Bondia huyo alijikatia tiketi ya […]

KPA YAFUZU LIGI YA AFRIKA LICHA YA KUPIGWA NA MAPUTO

Timu ya mpira wa kikapu ya Kenya Ports Authority (KPA) imejihakikishia kufuzu katika mashindano ya Basketball League Africa yanayoendelea Misri, licha ya kupoteza 91–76 dhidi ya mabingwa watetezi Ferroviario de Maputo kwenye mechi ya mwisho ya Kundi B. KPA ilikabiliana vikali na wenyeji waliokuwa na wachezaji sita wenye uzoefu mkubwa  ikicheza kwa ujasiri na kasi sawa katika […]

MURKOMEN APONGEZA MAAFISA 230 WA POLISI KUTOKA HAITI

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen amewapongeza maafisa wa polisi wa Kenya waliokuwa wametumwa nchini Haiti katika jukumu la kudumisha amani. Murkomen amesema kuwa Kenya, kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, ina jukumu la kushiriki katika operesheni za kurejesha amani katika mataifa yanayokumbwa na ghasia na machafuko. Maafisa 230 wa polisi waliorejea nchini juzi […]

JOHO AAHIDI USHIRIKISHWAJI WA UMMA KUHUSU UCHIMBAJI WA DHAHABU IKOLOMANI

Waziri wa Madini na Uchumi wa Baharini Ali Hassan Joho, amesema wizara yake itawahusisha wananchi katika mazungumzo ya kutatua mzozo unaoendelea kuhusu mpango wa uchimbaji wa dhahabu eneo la Ikolomani, kaunti ya Kakamega. Akizungumza baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano na serikali ya kaunti ya Kakamega, Joho amesema ushirikiano wa karibu kati ya serikali […]

WAVINYA AONYA MAAFISA WANAOFYONZA MAFUTA YA KAUNTI

Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti ametoa onyo kali kwa maafisa wa kaunti wanaohusishwa na uhalifu wa kufyonza na kutumia vibaya mafuta ya kaunti katika vituo vya mafuta ya petroli Wavinya amesema tabia hiyo imekuwa ikidhoofisha utoaji wa huduma na kusababisha ufujaji mkubwa wa rasilimali za umma, jambo linalowakosesha wananchi huduma wanazostahili kutoka kwa serikali ya […]

RUTO AWATAKA MAGAVANA KUHARAKISHA MAGEUZI MUHIMU

Rais William Ruto amezitaka serikali za kaunti kuongeza kasi katika kutekeleza mageuzi muhimu, akionya kwamba kuchelewesha hatua hizo kunaendelea kudumaza mafanikio kamili ya ugatuzi licha ya hatua kubwa zilizopigwa kitaifa. Akizungumza baada ya kuongoza Mkutano wa 12 wa Mashauriano kati ya Serikali ya Taifa na za Kaunti katika Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema ushirikiano kati […]

SACCOS 116 ZAPOKEA FIDIA BAADA YA KASHFA YA KSH 13B KUSCCO

Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo nchini (KUSCCO) umelipa Ksh152.4 milioni kwa SACCOs 116 na wawekezaji binafsi, na hivyo kuashiria hatua nyingine katika mpango wake wa urejeshaji kufuatia kashfa ya kifedha ya Ksh13.3 bilioni iliyofichuliwa mapema mwaka huu. Kama ilivyoripotiwa ni kwamba, fidia ya hivi punde imeleta jumla ya malipo hadi Ksh369.3 milioni, na […]

WAKULIMA WA CHAI RIFT VALLEY, NYANZA WAUMIZWA NA USIMAMIZI MBAYA

Wakulima wa chai katika Bonde la Ufa na Nyanza wanapata bonasi za chini zaidi kutokana na usimamizi duni wa kiwanda chini ya bei ya chai duniani kote, kufuatia ripoti ya kamati ya bunge. Ripoti hiyo inahusisha mapato ya chini na utawala dhaifu, gharama zilizopanda, uwekezaji uliokwama na kushindwa kwa ubora katika viwanda vilivyoko magharibi mwa Bonde la Ufa, na kuongeza pengo […]

LIVERPOOL WAONYESHA MWANGA

Mkwaju wa penalti wake Dominik Szoboszlai katika dakika ya 88 uliwapa mabingwa wa Uingereza Liverpool ushindi muhimu dhidi ya wenyeji Inter Milan ya Italia katika kipute cha ligi ya klabu bingwa barani Ulaya. Gumzo kubwa katika maandalizi ya mechi hiyo lilizingira fowadi wa Misri Mo Salah kuachwa nyumbani na kocha Arne Slot, baada ya matamshi […]