IVORY COAST WAMJUMUISHA ZAHA KIKOSINI

Mabingwa watetezi wa dimba la taifa bingwa barani Afrika Ivory Coast wamemrejesha kikosini wing’a wa zamani wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 33, wanapojiandaa kutetea taji hilo katika mashindano ya mwaka huu baadaye mwezi huu nchini Morocco. Zaha ambaye kwa sasa anawajibikia klabu ya Charlotte nchini Marekani, alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji […]

FKF YAINGIA MOU KUINUA SOKA YA VIJANA

Shirikisho la Soka nchini FKF limeingia makubaliano ya ushirikiano na chuo cha mafunzo ya soka cha Acakoro Football Academy na kuzindua mfumo wa kwanza nchini wa hali ya juu unaotoa makazi kwa wachezaji kwa ajililumu kwa ajili ya kukuza timu ya taifa ya vijana. Ushirikiano huo unalenga kushughulikia mapungufu ya muda mrefu katika uendeshaji wa soka ya vijana kwa kuanzisha njia ya pamoja na […]

WAVINYA, KIUSYA WALUMBANA

Ubabe wa kisiasa umeanza kujitokeza kati ya gavana wa Machakos Wavinya Ndeti na spika wa bunge la kaunti hiyo Ann Kiusya, baada ya Kiusya kusitisha vikao vya jana bungeni humo kabla ya kujadiliwa kwa mswada wa hazina ya kuyawezesha kifedha makundi ya akina mama kwenye kaunti hiyo. Katika kikao na wanahabari, Ndeti amemshutumu Kiusya kwa […]

NPS YAKARIBISHA KUNDI LA KWANZA KUTOKA HAITI

Idara ya polisi NPS imepokea rasmi kundi la kwanza la maafisa wa polisi waliokamilisha muda wa miezi 18 ya kuhudumu katika operesheni ya kurejesha utulivu nchini Haiti, siku 1 baada ya maafisa wengine 230 kutumwa nchini humo kuendeleza operesheni. Maafisa waliorejea na wenzao ambao pia wanajiandaa kurejea walitumwa mwaka jana na Rais William Ruto aliyewakabidhi […]

RUTO APUUZA ‘KELELE’ ZA UPINZANI

Hazina mpya ya miundomsingi itakuwa tayari wiki hii licha ya pingamizi ya muungano wa upinzani kuhusiana na mipangilio ya ufadhili wa hazina hiyo kupitia uuzaji wa hisa za kampuni moja ya mawasiliano. Ni msimamo wa Rais William Ruto akizungumza alipofungua makao makubwa zaidi duniani ya vifaru Weusi katika mbuga ya Tsavo akisema Kenya iko mstari […]

RIPOTI YAONYESHA JINSI MUMBE ALIVYOUAWA

Imebainika kuwa Patience Mumbe, msichana mwenye umri wa miaka 12 aliyetoweka na mwili wake kupatikana baadaye mtaani Embakasi Jumamosi iliyopita, alinajisiwa kabla ya kunyongwa. Ripoti ya upasuaji iliyotolewa na mwanapatholojia Grace Midigo imeonyesha kuwa mwili wake ulikuwa na majeraha mengi kichwani na mwilini, familia ikisema mwanao alitoweka alipokuwa akicheza na ndugu zake nje ya nyumba […]

DUALE: WANAOGOMA SI WAHUDUMU WA AFYA

Vuta nikuvute baina ya wizara ya afya na wahudumu wa afya imechukua mkondo tofauti, Waziri wa Afya Aden Duale sasa akiwalaumu wahudumu hao na kudai kuwa wengi wanaogoma si wahudumu wa afya ila ni watu wasiofahamika wanaoingilia maandamano ili kuhujumu sekta ya afya. Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Duale ametetea utendakazi wake, […]

KNCHR YAPUZILIA MBALI CHAGUZI 

Chaguzi ndogo zilizopita hazikuwa huru na haki kutokana na matumizi ya wahuni, hongo na maafisa wa serikali kushawishi matokeo ya chaguzi hizo. Ndiyo kauli ya tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu, ikisema maafisa wake walinyimwa ruhusa ya kuingia katika baadhi ya vituo vya kujumlisha kura kutoa uangalizi wao inavyohitajika kisheria. Wameitaka IEBC kuwajibikia […]

UPINZANI: IEBC KIBARAKA WA SERIKALI

Muungano wa upinzani umeibua madai kwamba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ni kibaraka wa serikali, ukirejelea chaguzi ndogo zilizopita ambazo muungano huo umesema zilifichua uhusiano kati ya IEBC na serikali ya Kenya Kwanza. Viongozi wa muungano huo akiwemo Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua na Eugene Wamalwa, wameionya tume hiyo inayoongozwa na Erastus Ethekon dhidi […]

KHRC YATHIBITISHA KUKAMATWA KWA WATETEZI WA HAKI SITA NAIROBI

Tume ya Haki za Binadamu Kenya, KHRC, imethibitisha kukamatwa kwa watetezi sita wa haki za binadamu waliokuwa wakitoa ombi katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi Kulingana na tume hiyo, Miongoni mwa waliokamatwa ni Frederick Ojiro, Julius Kamau, Vincent Mboya, Lichuma na Shem huku Mwanaharakati mwingine, Geoffrey Mboya, akifafanua kuwa walienda ubalozini kuonyesha mshikamano na wananchi wa Tanzania. […]