WAKAZI WA MAGHARIBI WATOA UJUMBE WA RAIS RUTO

Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Magharibi mwa nchi imeendelea kwa siku ya pili huku wakazi wakimtaka Rais kutimiza ahadi zake kuhusu utekelezaji wa miradi eneo hilo. Baada ya kikao na viongozi wa eneo hilo kwenye Ikulu ndogo ya Kakamega, Rais anatarajiwa kuongoza uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme mashinani katika eneo bunge […]

SUSWA: IPOA YAAHIDI HAKI KWA WAATHIRIWA

Katika juhudi za kurejesha utulivu na mshikamano katika eneo la Suswa kaunti ya Narok, mamlaka ya kutathmini mienendo ya maafisa wa polisi IPOA imesema inafanya uchunguzi wa kina kwenye mauaji ya watu wawili eneo hilo mwishoni mwa juma lililopita. Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, haki itapatikana kwa waathiriwa baada ya uchunguzi kukamilika kwenye machafuko hayo […]

WAFANYAKAZI WA MRADI WA NYUMBA WAGOMA BUSIA

Shughuli za ujenzi katika mradi wa serikali wa makazi ya bei nafuu katika eneo la Alema, eneo bunge la Funyula kaunti ya Busia zimekwama baada ya wafanyakazi kwenye mradi huo kugoma, wakimlaumu msimamizi kwa madai ya kutowasilisha matozo yao ya bima ya SHA na NSSF kwa afisi husika. Wakizungumza na wanahabari baada ya kususia kazi, […]

ABAUTANI YA WAFUGAJI KAJIADO KUHUSU CHANJO

Mpango wa serikali kuwapa chanjo mifugo humu nchini umepigwa jeki baada ya wafugaji katika kaunti ya Kajiado waliokuwa wamepinga mpango huo kubadili msimamo na kusema wataruhusu mifugo wao kuchanjwa. Wakizungumza kwenye kikao cha kuwahamasisha wafugajki katika eneo la Kimana Kajiado Kusini, wafugaji hao wamechukua uamuzi huo baada ya kupata ufahamu wa kutosha kuhusu mpango huo. […]

“TUOKOLEE NZOIA YETU” GAVANA LUSAKA

Katika juhudi za kuhakikisha wakulima wa miwa katika kiwanda cha sukari cha Nzoia wanaboresha Maisha yao, gavana wa Bungoma Ken Lusaka amemwomba Rais William Ruto kuingilia kati na kutatua matatizo ya kifedha kwenye kiwanda hicho. Akizungumza katika eneo la Mumias kaunti ya Kakamega ambako Rais amezindua bonasi kwa wakulima wa miwa, Lusaka amekariri haja ya […]

WATU WATANO WAFARIKI KATIKA AJALI HUKO MIGORI

Uchunguzi umeanzishwa na maafisa wa polisi baada ya watu watano, wakiwemo walimu wawili, kufariki papo hapo baada ya ajali iliyohusisha lori na pikipiki mbili katika daraja la Nyametembe, Kaunti ya Migori, usiku wa kuamkia leo Mashuhuda wanasema lori lililokuwa likiendeshwa kwa kasi lilipoteza mwelekeo na kugonga waendesha pikipiki wawili waliokuwa na abiria, na kuwaua wote […]

MAAFISA WA KLINIKI WAILAUMU SERIKALI KWA KUEPUKA MASUALA YAO WAKATI MGOMO WA KITAIFA UKIENDELEA

Shirikisho la Maafisa wa Kliniki la Kenya (KUCO) limelaani serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi huku mgomo wao ukiendelea. KUCO inadai serikali imeshindwa kushughulikia masuala yao, kama vile ubaguzi wa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) na kukataa kutoa nafasi kwa vituo vya afya vinavyomilikiwa na maafisa wa kliniki. Maafisa wa kliniki wametoa notisi ya […]

CITY YARUDI KATIKA KIWANGO BORA BAADA YA USHINDI WA 6-0 DHIDI YA IPSWICH

Manchester City ilishinda 6-0 dhidi ya Ipswich, huku Phil Foden akifunga mabao mawili na Mateo Kovacic akifunga bao la kuvutia. Jeremy Doku, Erling Haaland, na James McAtee waliongeza mabao baada ya mapumziko, ikifanya City kushinda kwa kishindo. Huu ni ushindi wa tatu kwa City katika mechi zao nne za ligi, wakiwa na matumaini ya kurejea […]

MANCHESTER UNITED WALAZWA MABAO 3-1 NA BRIGHTON

Manchester United walizabwa mabao 3-1 na Brighton kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati wakimkumbuka gwiji wa klabu Denis Law, aliyefariki Ijumaa akiwa na miaka 84. Yankuba Minteh alifunga bao la mapema kwa Brighton kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha kupitia penalti. Kaoru Mitoma na Georginio Rutter walifunga mabao mengine, wakiiwezesha Brighton kupanda hadi nafasi ya tisa, […]

SOKA YA KENYA YAOMBOLEZA KIFO CHA MWENYEKITI WA MATHARE UNITED BOB MUNRO

Mkurugenzi Mtendaji wa Mathare United, Jacktone Obure, amethibitisha kifo Bob Munro mtaalamu wa soka ambaye alifariki asubuhi ya jana Jumapili nyumbani kwake huko Westlands, Nairobi. Munro anahusishwa na kuongoza moja ya mashirika makubwa ya soka nchini Kenya, ambalo limetengeneza mamia ya wachezaji bora wa soka. Mnamo Disemba 12, 2024, wakati wa sherehe za Siku ya […]