CRYSTAL PALACE YATWAA CONFERENCE LEAGUE NA KUANDIKA HISTORIA

Crystal Palace wameandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Europa Conference League, taji ambalo linaongeza mafanikio yao makubwa ya mwaka 2025. Kabla ya mwaka huu, Crystal Palace hawakuwa wamewahi kushinda taji lolote kubwa katika historia yao, lakini sasa wamefanikiwa kutwaa mataji matatu ambayo ni FA, Community Shield na Conference League ndani ya kipindi […]

ANTHONY GORDON AELEKEA BARCELONA KWA ADA KUBWA

Anthony Gordon yuko mbioni kujiunga na FC Barcelona baada ya bodi ya Newcastle United pamoja na wamiliki wao kutoka Saudi Arabia kukubali ofa rasmi ya uhamisho huo. Taarifa zinaeleza kuwa Barcelona italipa euro milioni 70 pamoja na nyongeza mbalimbali zitakazofikisha thamani ya dili hilo zaidi ya euro milioni 80 kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Gordon […]

ODEMBA AWAREJESHA MORANG’A NA SHIYONZO HARAMBEE STARLETS

Wachezaji Emily Morang’a na Vivian Shiyonzo ni miongoni mwa waliorejeshwa katika kikosi cha muda cha Harambee Starlets kilichotajwa na kocha Beldine Odemba kwa ajili ya mashindano ya mataifa manne yatakayofanyika Zambia. Odemba amedumisha sehemu kubwa ya kikosi kilichoshiriki mechi za hivi karibuni za kimataifa huku akiwajumuisha tena baadhi ya wachezaji waliowahi kuitumikia timu ya taifa […]

JULIUS YEGO ATAKA MASHINDANO ZAIDI YA KIMATAIFA NCHINI

Bingwa wa zamani wa dunia wa mkuki Julius Yego ametaka shirikisho la riadha nchini AK kuandaa mashindano zaidi yaliyoidhinishwa na shirikishi la riadha duniani humu nchini ili kuwasaidia wanariadha kufuzu kwa urahisi mashindano ya dunia ya mwaka 2027 yatakayofanyika Beijing. Kauli yake imejiri baada ya shirikisho la riadha duniani kutangaza viwango vipya vya kufuzu kwa mashindano hayo, ambapo wanariadha watalazimika kufikia […]

EMILY ADHIAMBO AIAMINI JUNIOR STARLETS DHIDI YA UGANDA

Mshambuliaji wa Junior Starlets Emily Adhiambo amesema ana imani Kenya itaifunga Uganda katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17 itakayochezwa hapo kesho katika uwanja wa Nyayo. Kenya ilipata sare muhimu ya mabao 1-1 dhidi ya Uganda  katika mkondo wa kwanza uliochezwa Kampala, ambapo Adhiambo alifunga bao la kusawazisha baada ya […]

FAMILIA KIBRA YATAKA HAKI BAADA YA MWANAMKE KUCHOMWA MOTO KIBRA

Familia moja katika eneo la Gatwikira huko kibra inataka haki baada ya ndugu yao kudaiwa kushambuliwa kutokana na msimamo wake wa kisiasa. Maureen Matsili ambaye ni mama wa watoto wanne, anadaiwa kushambuliwa na kuchomwa moto Mei 18 na mtu anayemfahamu kutokana na kuunga mkono kauli mbiu ya “Two Term” katika eneo hilo. Polisi wa Kibra wanaendelea kuchunguza […]

DUALE: SHERIA ZA KENYA LAZIMA ZIHESHIMIWE KATIKA USHIRIKIANO WA EBOLA

Waziri wa Afya Aden Duale amesema makubaliano yoyote kati ya Kenya na mataifa ya kigeni kuhusu kushughulikia watu walioathiriwa na virusi vya Ebola lazima yaheshimu sheria za Kenya pamoja na kanuni za afya ya umma. Kauli hiyo inajiri kufuatia ripoti kuwa Marekani inaweza kuzingatia kuwaleta nchini Kenya baadhi ya raia wake waliokaribiana na wagonjwa wa […]

WANAFUNZI KADHAA WAFARIKI KATIKA MOTO WA BWENI LA WASICHANA LA UTUMISHI

Moto mkubwa umezuka alfajiri katika shule ya wasichana ya Utumishi Academy eneo la Gilgil na kusababisha hofu ya vifo pamoja na majeruhi kadhaa baada ya bweni moja kuteketea kwa moto. Ripoti za awali zinaonyesha kuwa baadhi ya wanafunzi wanahofiwa kufariki huku wengine wakijeruhiwa na wengine kuathiriwa na moshi, hali ambayo imezua taharuki kubwa miongoni mwa wanafunzi, walimu […]

MUKHISA KITUYI ASEMA HAGOMBEI WADHIFA WOWOTE

Aliyekuwa Waziri wa Biashara Mukhisa Kituyi amesema hana mpango wa kugombea wadhifa wowote wa kisiasa licha ya baadhi ya watu kumshawishi kufanya hivyo. Kituyi amesema si kila kiongozi anapaswa kuelekeza nguvu katika kuwania urais, akisisitiza kuwa taifa pia linahitaji watu wenye uzoefu na ushawishi wa kusaidia kutoa ushauri kwa viongozi wengine. Ameongeza kuwa kuna haja […]

RAIS RUTO AHUDHURIA KIKAO CHA KITAIFA CHA MAOMBI

Rais William Ruto amewasili katika hoteli ya  Safari Park kuhudhuria hafla ya kikao cha Kitaifa cha Maombi kinachowaleta pamoja viongozi wa kisiasa, kidini na serikali Viongozi mbalimbali wa kitaifa, wanasiasa pamoja na maafisa wa serikali pia wamewasili katika hafla hiyo inayolenga kuombea taifa na kuhimiza mshikamano wa kitaifa Hafla hiyo ya kila mwaka huwakutanisha viongozi kutoka sekta tofauti nchini kwa maombi, […]