UHALALI WA JOPO LA KUTIMULIWA KWA GACHAGUA KUBAINIKA

Mahakama ya upeo imeratibiwa hii leo kutoa uamuzi wake kubaini iwapo jopo la mahakama kuu lililoteuliwa kusikiliza kesi ya akubanduliwa afisini kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua lilibuniwa kikatiba. Jopo la majaji 4 wa mahamama hiyo ya upeo litatoa uamuzi kuhusu jopo la majaji 3 wa mahakama kuu lililosikiliza na kuamua kwamba Gachagua atimuliwe Oktoba […]

MWONGOZO WA SHA KUSITISHA ‘UTALII WA KIMATIBABU’

Ni huduma za matibabu ambazo hazipatikani nchini pekee ndizo zitagharamiwa na mamlaka ya afya ya jamii SHA nje ya nchi, katika mwongozo mpya ambao umetolewa na mamlaka hiyo katika juhudi za kuziba mianya ya ufisadi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo. Katika mwongozo huo, SHA imetangaza kugharamia upasuaji 36 pekee nje ya nchi kama […]

MAN UNITED YAPANGA MKATABA MPYA NA KOBBIE MAINOO

Klabu ya Manchester United imepanga kuzungumza kuhusu mkataba wa muda mrefu na kiungo wake Kobbie Mainoo, baada ya kuonyesha mchango mzuri chini ya kocha Michael Carrick. Mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 2027, ukiwemo chaguo la kuongeza msimu mmoja hadi 2028, lakini United wanataka kuanza mazungumzo ya mkataba mpya mapema mwaka huu ili kumhakikishia huduma ya Mainoo kwa muda mrefu. United imedokeza kuwa wanaridhishwa na maendeleo […]

ALDRINE KIBET ANG’ARA HISPANIA

Mshambuliaji wa Kenya Aldrine Kibet ameendelea kung’ara nchini Hispania baada ya kuchangia pakubwa ushindi wa kusisimua wa Timu ya vijana ya Celta Vigo wa mabao 4–3 dhidi ya Atlético Madrid, uliowavusha hadi robo fainali ya Copa del Rey Juvenil. Kibet alihusika moja kwa moja katika mabao mawili, akifunga bao moja na kutoa pasi ya bao katika mechi hiyo kali iliyoonesha mchango wake unaozidi kukua kikosini. […]

AKONNOR AAHIDI USHINDI DHIDI YA SOFAPAKA

Kocha wa Gor Mahia, Charles Akonnor, amethibitisha kuwa timu yake itafanya kila jitihada kushinda mechi dhidi ya Sofapaka katika Uwanja wa Nyayo Jumamosi hii, huku wakilenga kuthibitisha nafasi yao kileleni mwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL). K’Ogalo wanashikilia kilele kwa pointi 36, sawa na wapinzani wao wa jadi AFC Leopards, lakini wapo mbele kwa tofauti ya mabao. Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkali katika […]

MAANDALIZI YA HSBC SVNS 2 YAFIKIA ASILIMIA 80 NCHINI KENYA

c Mwenyekiti wa Shirikisho la Raga Kenya (KRU), Harriet Okatch, amesema hatua kubwa zimepigwa katika maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuvutia timu na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali duniani. Akizungumza kuhusu hali ya utayari, Okatch amewahakikishia mashabiki na wadau wa michezo kuwa kazi inaendelea kwa mpangilio mzuri katika maeneo muhimu, na kwamba mashindano hayo yatafanyika kama ilivyopangwa. Imetayarishwa […]

SHA YAFUNGUA HUDUMA ZA HOSPITALI BINAFSI KWA WAKENYA WOTE

Wakenya ambao awali waliona hospitali binafsi za rufaa kuwa za watu wenye uwezo wa kifedha sasa wanaweza kupata huduma maalum za matibabu bila gharama ya ziada kupitia Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Akizungumza wakati wa Mkutano wa Mafunzo ya Wabunge wa Bunge la Kitaifa jijini  Naivasha, Waziri wa Afya Aden Duale amesema serikali imechukua hatua mahsusi […]

MZEE AHUKUMIWA MAISHA KWA KUMNAJISI MJUKUU WAKE BUNGOMA

Mzee Mmoja kwa jina la Benson Kitui amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mjukuu wake mwenye umri wa miaka kumi Tukio linaloripotiwa kutokea katika eneo la Sasur, kaunti ndogo ya Cheptais, kaunti ya Bungoma. Kitui alifikishwa mbele ya Mahakama ya Sirisia, ambapo hukumu hiyo ilisomwa, ikionyesha msimamo mkali wa mahakama dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kingono, hasa vinapofanywa ndani […]

OSORO AWAAMBIA UPINZANI KULETA AJENDA KABLA YA IEBC

Mbunge wa South Mugirango, Sylvanus Osoro, amewatilia shaka wanasiasa wa upinzani, akiwashauri kuweka wazi ajenda yao ya kile wanachokusudia kufanya kwa wananchi kabla ya kufika Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuzungumzia maandalizi ya uchaguzi. Akizungumza katika sherehe iliyofanyika Kaunti ya Kisii chini ya uongozi wa Rais William Ruto, Osoro alidai kuwa wanachama wa United Opposition hawana ajenda thabiti. Osoro amewataka kwanza kukubaliana juu ya mgombea urais, kuwa na […]

FAMILIA YA JEFF MWATHI YAOMBA MAHAKAMA KUHARAKISHA KESI

Familia ya Jeff Mwathi imeomba mahakama ziendelee haraka na kwa ufanisi na kesi inayohusu kifo chake, ikieleza kuwa mchakato huo umekuwa wa kusababisha maumivu makubwa kwao. Kupitia wakili wao, Danstan Omari, familia imebainisha kuwa Mwathi alizikwa mara mbili, jambo lililozidisha huzuni yao na kuendelea kuendeleza maumivu ya kifamilia. Familia imetaja kuwa wako tayari kujitokeza mahakamani wakati wowote kuhakikisha kesi inasikilizwa na kufikiwa uamuzi bila […]