DUALE AKANUSHA UFISADI KATIKA MAMLAKA YA SHA

Waziri wa Afya Aden Duale amepuuza madai kwamba shilingi bilioni 11 za fedha za umma zimefujwa katika Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) akisema kuwa fedha hizo ni madai yaliyowasilishwa kwa njia isiyofaa na hospitali mbalimbali. Duale amesema kuwa malipo hayo hayataidhinishwa iwapo stakabadhi zitabainika kuwa za kughushi au zisizokidhi vigezo vilivyowekwa. Aidha, Waziri huyo ametangaza kuwa SHA italipa […]

VYUO VIKUU VYAPITIA UPYA VIGEZO VYA UDAHILI KUELEKEA MFUMO WA CBE 2029

Vyuo vikuu nchini Kenya vimeanza mchakato wa kupitia upya vigezo vya udahili wakijiandaa kwa mpito wa mfumo wa Elimu Inayozingatia Umahiri mwaka 2029. Katika mkutano wa wadau uliofanyika Naivasha, Huduma ya Uwekaji wa wanafunzi katika Elimu ya Juu (KUCCPS) imeeleza kuwa mfumo wa sasa wa udahili utabadilishwa kikamilifu, ukiondoka katika utegemezi wa alama za mitihani pekee na […]

KENYA KUTUNGA KANUNI MAALUM KUENDELEZA MIRADI YA NYUKLIA 

Bunge la kitaifa litaidhinisha kanuni maalum ili kuhakikisha taifa linaendeleza mpango wake wa nishati ya nyuklia. Spika wa Bunge hilo, Moses Wetang’ula, amesema hayo wakati wa kikao na uongozi wa kampuni ya uzalishaji umeme ya Kenya, KenGen, na Shirika la Nishati ya Umeme wa Nyuklia, NuPEA kilichofanyika katika majengo ya Bunge. Mbali na Sheria ya Udhibiti wa Nyuklia iliyopo, kikao hicho […]

UEFA: TIMU ZA EPL ZATAMALAKI RAUNDI YA 16

Klabu 6 zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, ni miongoni mwa timu 16 zinazosubiri kufahamu wapinzani wao kwenye raundi 16 katika dimba la klabu bingwa bara Ulaya hii leo. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu 6 kutoka EPL kufuzu raundi ya 16 ya dimba hilo. Klabu hizo ni Arsenal walioshinda mechi zote […]

WELTEJI APIGWA MARUFUKU YA MIAKA 2

Mwanariadha wa mbio za masafa ya kati Diribe Welteji amepigwa marufuku ya kushiriki mbio kwa miaka 2 na mahakama ya kushughulikia masuala ya spoti, CAS, baada ya kukosa kuwasilisha sampuli zake kwa uchunguzi kuhusiana na matumizi ya dawa za kutitimua misuli Februari mwaka jana. Mahakama hiyo pia ilifutilia mbali matokeo yote ya raia huyo wa […]

JUHUDI ZA INGWE KUNYAKUA TAJI ZAPATA PIGO KPL

Azma ya klabu ya AFC Leopards kutoa ushindani kwa Gor Mahia kuwania taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL, ilipata pigo hapo jana baada ya kucharazwa bao 1-0 na wanabenki KCB katika uwanja wa Kasarani. Ingwe waliingia uwanjani wakilenga kupunguza mwanya kati yao na Gor, ila KCB wakalinda benki yao dhidi ya kucha za […]

UDA MBELE KWENYE CHAGUZI ZOTE NDOGO

Chama cha UDA kimeratibiwa kunyakua nyadhifa zote za ubunge na uwakilishi wadi katika maeneo manne kulikofanyika uchaguzi mdogo hapo jana, wagombeaji wa nyadhifa hizo kwa tiketi ya UDA wakiongoza kulingana na matokeo ya awali. Katika wadhifa wa ubunge eneo la Isiolo South, Tubi Mohammed Tubi aliyekuwa akiwania na dadake kumrithi baba yao, yuko mbele tayari […]

NAIBU GAVANA WA HOMA BAY AJIUZULU

Kinyang’anyiro kikali kinatarajiwa kwenye uchaguzi wa ugavana kaunti ya Homa Bay katika uchaguzi mkuu ujao kufuatia kujiuzulu kwa naibu gavana, Joseph Magwanga, aliyeaminika kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa kwenye uchaguzi mkuu uliopita kabla yake kushawishiwa kumuunga mkono gavana wa sasa Gladys Wanga. Katika taarifa, Magwanga ambaye hajakuwa akielewana kisiasa na Wanga, amesema uamuzi huo umejiri […]

UTATA WA PASPOTI MIKONONI MWA RAIA WA KIGENI

Idara ya uhamiaji inatarajiwa kutoa taarifa kuhusu madai ya kukiuka sheria na kutoa paspoti za usafiri kwa raia wa kigeni wanaohusishwa na Sakata za ufisadi na mapigano , akiwemo Algoney Dagalo Hamdan, kakake mdogo wa kiongozi wa kundi la wapiganaji nchini Sudan RSF, Mohammed Hamdan. Wengine walio na paspoti hizo ni raia wa Sudan wanaoaminika […]

WETANG’ULA ATAKA NCIC IVUNJILIWE MBALI 

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amelitaka bunge kuvunjilia mbali tume ya kitaifa kuhusu uwiano na utangamano, NCIC, kwa misingi kwamba imeshindwa kutekeleza wajibu wake. Akirejelea matamshi ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua dhidi ya mbunge wa Nyaribari Chache Zaheer Janda, Wetang’ula amemwagiza kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wa kuhakikisha kuwa NCIC inavunjiliwa […]