BEI YA YAI YAPANDA HADI 20% KUFUATIA KUPANDA KWA MALISHO

Bei ya mayai ya kuku jijini Nairobi imepanda hadi asilimia 20 katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, ikichangiwa na kupanda kwa gharama za malisho na mahitaji ya msimu. Yai katika mashamba mengi jijini Nairobi inauzwa kati ya Ksh15 na Ksh18. Kufuatia ripoti ni kuwa, bei za reja reja sasa ni kati ya Ksh450 hadi Ksh480 kwa trei moja, huku maduka makubwa […]

SAKAJA MBELE YA SENETI KUELEZA MKATABA

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja yuko mbele ya bunge la seneti anakokabiliwa na kibarua cha kueleza mkataba wa ushirikiano kati ya serikali yake na serikali kuu uliotiwa saini takribani moja iliyopita. Akiwa mbele ya bunge hilo, Sakaja ametetea mkataba huo licha ya tuhuma kwamba amepokonywa mamlaka ya serikali kuu, akisema utaipa kaunti fedha za ziada […]

USAMBAZAJI WA DAWA ZA KUKABILI HIV WAANZA

Hatimaye wizara ya afya imezindua usambazaji wa dawa za Lenacapavir za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI, zilizowasili nchini wiki jana. Dawa hiyo inayolenga kuzuia maambukizi mapya nchini, inatolewa kama chanjo mara 2 kwa mwaka kwa wakenya walio katika hatari ya kuambukizwa. Zoezi hilo linaoongozwa na Waziri wa afya Aden Duale. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKENYA WATAHADHARISHWA DHIDI YA BIDHAA GHUSHI

Mamlaka ya kukabiliana na bidhaa ghushi nchini, ACA, imewatahadharisha wakenya dhidi ya kumia bidhaa hizo, ikisema matumizi ya bidhaa hizo yamechangia madhara makubwa kwa uchumi wa taifa. Katika kikao na wanahabari baada ya kongamano la siku moja na wadau mbali mbali mjini Bungoma, mkurugenzi wa mamlaka hiyo Henry Maina, amesema kuwa Kenya ni miongoni mwa […]

CHAGUZI NDOGO 4 ZAENDELEA NCHINI 

Tume huru ya ucahguzi na mipaka, IEBC, inaendeleza chaguzi ndogo 4 za kumchagua mbunge na wawakilishi wadi 3 katika maeneo mbali mbali ya nchi. Maeneo hayo ni Isiolo South ambako wakazi wameingia debeni kumchagua mbunge, na katika wadi za West Kabras kaunti ya Kakamega, Muminji za Evurore kaunti ya Embu. Wadhifa wa ubunge Isiolo south […]

KLABU 16 ZASUBIRI DROO YA RAUNDI YA 16 UEFA

Lazar Samardzic alifunga mkwaju wa penalti katika dakika za mwisho na kuizamisha Borussia Dortmund ya Ujerumani waliopokezwa kichapo cha mabao 4-1 na wenyeji Atalanta wa Italia katika kipute cha kufuzu raundi ya 16 ya klabu bingwa bara Ulaya jana usiku. Dortmund waliokuwa wakiongoza mabao 2-0 kutokana na ushindi kwenye mkondo wa kwanza, walishindwa kulinda uongozi […]

SHABANA YAJIWEKA MIONGONI MWA WAWANIAJI KPL

Ushindi mwembamba wa bao 1-0 wa Shabana FC dhidi ya Mathare United uliwapandisha na kuwaweka alama sawa na AFC Leopards, na hivyo kuiweka timu hiyo katika nafasi ya kuwania taji la ligi kuu ya soka nchini, KPL. Bao la pekee la mchezo lilipachikwa wavuni na nahodha George Onyango dakika za jioni, na kuwapa vijana hao […]

ODIRA, HUNTER-BELL NA HODGKINSON KUFUFUA UHASIMU PREFONTAINE CLASSIC

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 800, mkenya Lilian Odira ameratibiwa kufufua uhasama kati yake na Waingereza Keely Hodgkinson na Georgia Hunter-Bell, watatu hao watakapochuana katika mbio za Prefontaine Classic Julai mwaka huu. Kinyang’anyiro chao cha hivi punde ni katika mbio za ubingwa wa dunia jijini Tokyo Septemba mwaka jana, ambapo Odira aliwaonyesha kivumbi […]

MATIBABU YAENDELEA KUSAMBARATIKA NAIROBI, MARSABIT

Wakazi katika kaunti za Nairobi na Marsabit wanaendelea kutatizika kupata huduma za matibabu kwenye hospitali za umma kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya, wanaosema hali imedorora zaidi na kuweka maisha ya wagonjwa hatarini. Kulingana na maafisa wa muungano wa wahudumu hao wakiongozwa na viongozi wa KUCO, takribani asilimia 90 ya huduma sasa hazipatikani, huku […]

FAMILIA YA JAMAA “ALIYERUSHWA’ YALILIA HAKI

Polisi wameimarisha uchunguzi katika tukio ambapo mwanamme mwenye umri wa miaka 25 alifariki baada ya kuripotiwa kurushwa nje ya basi la uchukuzi ambalo hatimaye lilimkanyaga hadi kufa kwenye barabara ya Kitengela kuelekea Namanga kaunti ya Kajiado Jumanne usiku. Familia ya Joseph Mureithi imesema kwamba jamaa yao alikuwa akirejea nyumbani kutoka kazini aliporushwa nje ya basi […]