POLISI NA NCIC WACHUNGUZA KESI 12 ZA CHUKI NA UCHOCHEZI

Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) zimechunguza kesi 12 za matamshi ya chuki, uchochezi wa vurugu, unyanyasaji mtandaoni na usambazaji wa maudhui ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Uwiano wa Kitaifa, Fursa Sawa na Ujumuishaji […]

UWEKAJI MSINGI WA UPANUZI WA SGR HADI KISUMU KUANZA MACHI

Serikali ina mpango wa kuanza kutambua na kuwalipa fidia watu ambao wataathiriwa na mradi wa upanuzi wa Reli ya Standard Gauge (SGR), ambao msingi wake umepangwa kufanyika mwezi Machi. Akizungumza mjini Kisumu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Philip Mainga amedokeza kuwa awamu ya 2B ya njia hiyo itakamilika kufikia Juni 2027, na kufungua eneo la Magharibi kwa usafirishaji […]

BODO GLIMT WAIBANDUA INTER MILAN, ATLETICO NDANI

Klabu ya Bodo Glimt kutoka Norway iliendeleza kisa chake cha kuangusha miamba wa soka bara Ulaya, baada ya kuwapa Inter Milan kichapo cha jumla ya mabao 5-2 nyumbani na ugenini kufuzu raundi ya 16 ya klabu bingwa bara Ulaya. Glimt ambao wameicharaza Manchester City na Atletico Madrid msimu huu, walifika San Siro jana usiku wakiwa […]

KVF: KCB UGANI DHIDI YA SPIKERS

Kivumbi kinatarajiwa kutifuliwa katika ligi ya voliboli nchini, KVF, mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, KCB, watakapopambana na Young Spikers hii leo katika mechi ya mkondo wa pili ugani Kasarani Sports Centre Indoor Arena. Wanabenki hao, chini ya uongozi wa Japheth Munala, watalenga kuvuna ushindi muhimu ili kupanda katika nafasi muhimu ya jedwali. Kwa sasa […]

MKUFUNZI WA TUSKER FC AAHIDI MWAMKO MPYA KLABUNI

Kocha mkuu mpya wa klabu ya Tusker FC, Mfaransa Julien Mette, amesema kuwa klabu hiyo haitazuilika tena punde baada ya wachezaji wake kujifahamisha na mtindo na falsafa yake ya mchezo. Mette ameonyesha kuridhishwa na jinsi wachezaji wake wanavyokumbatia mtindo na mbinu zake, anapojiandaa kwa mechi yake ya pili hii leo dhidi ya Murang’a Seal katika […]

KESI YA MAUAJI DHIDI YA AFISA WA POLISI KUENDELEA

Kesi ya mauaji inayomkabili afisa wa polisi Ahmed Rashid anayetuhumiwa kwa makosa ya kuwaua vijana wawili Jamal Mohammed na Mohammed Dhair Kheri Machi mwaka 2017 inatarajiwa kuendelea leo katika mahakama ya Kibra mbele ya hakimu Diana Kavedza. Mashahidi watatu akiwemo afisa kutoka idara ya upelelezi, DCI, na afisa wa mamlaka ya mawasiliano, CAK, wameratibiwa kutoa ushahidi wao katika kikao […]

SHOKA LA ODM LAWAANGUKIA WAASI BUNGENI

Wabunge wanaokosoa serikali jumuishi akiwemo Caroli Omondi, Anthony Kibagendi na mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kisumu Ruth Odinga ni miongoni mwa waliofurushwa kutoka nyadhifa za uongozi wa bunge kutokana na msimamo wao, bunge likitishia kuwafurusha wakosoaji zaidi. Omondi ambaye amekuwa akihudumu kama mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa katiba bungeni, amefurushwa na wadhifa wake […]

IEBC YATAKA BILIONI 1 KWA MAAKULI

Wabunge wametofautiana na bajeti ya shilingi bilioni 63.9 ya tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, ambapo shilingi bilioni 1 zimetengewa chakula cha maafisa wa tume hiyo katika kipindi cha uchaguzi. Wakifika mbele ya kamati ya haki na masula ya kisheria bungeni, maafisa wa IEBC wamesema kwamba wanahitaji shilingi […]

WANDAYI ATETEA KUJIHUSISHA NA SERIKALI

Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, ametetea kujihusisha kwake na shughuli za kisiasa nchini licha ya ukosoaji kutokana na wadhifa wake serikalini, akisema amekuwa akitumia majukwaa hayo kuwaeleza wakenya kuhusu utendakazi wa serikali. Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Wandayi amepuzilia mbali kwamba hatua hiyo ni sawa na kampeni za mapema za kumpigia debe […]

WANYAKUZI WAFIKIA ARDHI YA IKULU

Suala la unyakuzi wa ardhi ya umma limeonekana kuvuka mipaka, ikiibuka kwamba ardhi ya Ikulu ndogo katika kaunti za Kisumu, Uasin Gishu na Nakuru zimenyakuliwa na watu binafsi. Kwa mujibu wa msimamizi wa Ikulu Katoo Ole Metito akizungumza mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, mwakilishi wadi mteule amejenga makazi yake kwenye ardhi ya Ilulu […]