DUKUDUKU LA SICHENJE KUANZA KAZI CHARLTON

Beki wa Harambee Stars Collins Sichenje anaamini kwamba uhamisho wake kuelekea klabu ya Charlton Athletic inayoshiriki ligi ya Championships nchini Uingereza ni hatua kubwa katika taaluma yake katika kuelekea kwenye hatma ambayo amekuwa akijiandalia. Sichenje alisajiliwa mapema wiki hii na klabu hiyo kutoka klabu ya FK Vojvodina ya Serbia kwa kima cha takribani shilingi milioni […]

VYAMA TANZU VYAPINGA MAGEUZI AZIMIO

Mvutano wa kisheria unanukia ndani ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kuhusiana na mageuzi ya hivi punde kwenye uongozi wake, baada ya kundi la vyama wanachama kupinga mageuzi hayo likiyataja kuwa kinyume na sheria. Likiongozwa na katibu mkuu wa chama cha National Liberal Party, NLP, Omondi Koyoo, kundi hilo limemwandikia msajili wa vyama […]

RATIBA YA IEBC KUELEKEA 2027

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC iko mbioni kufanikisha masuala muhimu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, ikiwemo kuhakikisha kuwa mtandao wa kupeperusha matokeo ya uchaguzi unafanya kazi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu. Akizungumza wakati wa kuweka wazi ratiba ya kuelekea kwenye uchaguzi huo, mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema tume hiyo imetoa […]

VURUGU ZA KUTOWEKA BUSIA

Polisi mjini Busia na wanatarajiwa kuwafikisha mahakamani hii leo watu kadhaa waliokamatwa hapo jana wakihusishwa na vurugu wakati wa maandamano kufuatia kutoweka kwa mfanyabiashara Ibrahim Mohammed kwa wiki 2 sasa. Familia ya Mohammed na wakazi wanataka polisi kuweka wazi aliko jamaa huyo, wanayesema alitoweka muda mfupi baada ya kushukishwa kwenye basi katika kizuizi cha polisi. […]

PANA HAJA MAGAVANA KUFUATILIWA- MASENETA

Maseneta wamesisitiza haja ya uwazi, uwajibikaji na ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa na serikali za kaunti ili kulinda mali ya umma, baada ya ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kuibua ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa miradi hiyo na ubadhirifu wa fedha za umma. Haya yamebainika wakati magavana wamekuwa wakifika mbele ya kamati ya seneti […]

ELLIOTT AKWAMA ASTON VILLA

Kiungo wa Liverpool Harvey Elliott anakabiliwa na mwisho mgumu wa msimu akiwa Aston Villa baada ya klabu yake kukataa kusamehe ada ya kusitisha mkopo. Hatua hiyo ingezuia kifungu cha uhamisho wa lazima cha pauni milioni 35. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa nje ya mipango ya kocha Unai Emery ili kuepuka kifungu hicho, […]

 CASEMIRO AANGALIWA NA LA GALAXY

Klabu ya LA Galaxy inaripotiwa kuchunguza uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester United Casemiro kwa uhamisho wa bure msimu huu wa kiangazi. Mchezaji huyo wa Brazil amethibitisha ataondoka Old Trafford mkataba wake utakapomalizika mwezi Juni. Casemiro, ambaye ameonyesha kiwango kizuri chini ya kocha wa muda Michael Carrick, pia anahusishwa na dili nono la kuhamia Saudi […]

RISING STARLETS KUPAMBANA NA TANZANIA

Kocha wa Rising Starlets Jackline Juma amesema uimara wa kisaikolojia na utayari wa mechi ndiyo vigezo vikuu alivyotumia kuchagua kikosi cha Harambee Starlets U20 kuelekea mchujo wa Kombe la Dunia la FIFA dhidi ya Tanzania. Kenya itawakaribisha Twiga Stars katika mechi ya mkondo wa kwanza Februari 7 katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex kabla ya […]

SOY UNITED WAMSAJILI MOSES SHIKANDA

Soy United wameimarisha azma yao ya kupanda daraja msimu wa 2025/26 wa FKF National Super League baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Moses Shikanda kwa mkataba wa kudumu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anakuwa usajili wa tatu wa dirisha dogo la usajili, huku Blue Eagles wakiendelea kuimarisha kikosi chao katika harakati za […]