UPINZANI WADAI SERIKALI INAWAPUMBAZA

Ripoti ya kamati ya fedha na mipango katika bunge bunge la kitaifa kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2024-25 inaendelea kujadiliwa bungeni ambapo wabunge wanachambua mapendekezo ya kamati hiyo. Haya yanajiri wakati ambapo wabunge wa upinzani wamepinga mswada huo, wakidai kwamba hatua ya serikali kuondoa baadhi ya mapendekezo ya ushuru kwa bidhaa kadhaa kwenye mswada […]

ONYO YA AFISI YA DETA KWA WAKENYA

Afisi ya msimamizi wa deta imewaonya wakenya dhidi ya kuweka wazi maelezo ya kibinafsi ya wenzao, zikiwemo nambari za simu, baada ya baadhi ya Wakenya katika mitandao ya kijamii kuweka wazi nambari za simu za wabunge na viongozi wakuu serikalini kwa lengo la kuwashinikiza kuangusha mswada wa kifedha. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, afisi […]

NI WAKATI WA VIWANDA KUNAWIRI: DIDMUS

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa, ametetea mapendekezo ya mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25, akisema mapendekezo haya yatalinda watengenezaji wa bidhaa humu nchini na hivyo kubuni nafasi za ajira. Akizungumza bungeni wakati wa kikao kinachoendelea, Barasa amewalaumu wabunge wa upinzani kutokana na kudorora kwa hali ya uchumi hapa nchini. Kulingana na mbunge huyo, mswada huo […]

MAANDAMANO YA USHURU MOMBASA

Licha ya serikali kuondoa baadhi ya vipengee kwenye mswada wa kifedha wa mwaka 2024-25, wakazi katika kaunti ya Mombasa wanaendeleza maandamano dhidi ya mswada huo, wanaosema unamkandamiza mwananchi. Wakiwa na mabango, wakazi hao wamendamana katikati mwa jiji la Mombasa wakilenga kuwashinikiza wabunge wao kutupilia mbali mswada huo. Aidha, wakazi hao wamedai kuwa hatua ya kuondoa […]

WAKULIMA BUSIA WAPINGA ETIMS

Wakulima wa miwa katika kaunti ya Busia wamepinga vikali agizo la mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA kuwataka wajisajili na mfumo wa ETIMS kabla ya kuruhisiwa kuuza miwa yao, wakitishia kung’oa zao hilo na kujitosa katika kilimo mbadala kufuatia agizo hilo. Wakizungumza katika eneo la Busibwabo kwenye hafla ya uhamasisho kuhusu mfumo huo wa ushuru, wakulima […]

“HATUELEWANI, DAWA IKO!”- NAKURU

Naibu gavana wa Nakuru David Kones amekanusha madai ya ukosefu wa dawa katika vituo vya afya kwenye kaunti hiyo, akisema kuna utaratibu unaofuatwa katika kusambaza dawa katika kila hospitali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa dawa za zaidi ya shilingi milioni 26.2 kutoka kwa mamlaka ya usambazaji wa dawa nchini KEMSA, Kones amesema  kuna baadhi ya […]

WABUNGE WAANZA KUJADILI MSWADA WA FEDHA 2024 SIKU YA 1

Vikao vya bunge kujadili kuhusu Mswada wa Fedha, 2024, ambao unaelezea safu ya hatua za kuongeza mapato kwa utawala wa Rais William Ruto vimeanza. Wabunge wanatarajiwa kuujadili Muswada huo hadi saa 9:30 alasiri ambapo wanatarajiwa kutoa maoni yao kuhusu kile wanachotoa kuhusu yaliyomo katika mswada huo. Jana Jumanne, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula […]

WAMALWA: MLIKOPA MKALISHA NANI?

Kiongozi wa chama cha DAP kenya Eugine Wamalwa amekosoa hatua ya serikali kupunguza kodi kwa baadhi ya bidhaa muhimu. Katika mahojiano na klituo kimoja cha redio humu nchini. Wamalwa amesema kuwa serikali ingeonyesha nia ya kusikia kilio cha wakenya kwa kupunguza kodi ya mafuta kwani kulingana naye bila kupunguza kodi hiyo wakenya watazidi kukumbwa na […]

KOBBIE ATAJWA KWA KIKOSI CHA KWANZA CHA RED DEVILS

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo ana furaha kwamba uvumi kuhusu mustakabali wa mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag umeisha, baada ya kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza na Mholanzi huyo. Msimu wa mafanikio wa Mainoo akiwa na hawa  Mashetani Wekundu, ambao ulijumuisha kufunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA […]

MLINZI AUAWA KATIKA UVAMIZI WA SHULE MAI MAHIU

Maafisa wa upelelezi wanasaka genge lililovamia shule moja eneo la Mai Mahiu kaunti ya Nakuru na kumuua mlinzi wa usiku. Kwa mujibu wa polisi Mlinzi huyo kwa jina  Boaz Orono amefariki dunia baada ya majeraha alipowasili katika Hospitali ya moja eneo hilo. Genge hilo lilivamia shule hiyo na kumfunga mlinzi aliyekuwa zamu katika duka baada […]