KQ YAZINDUA SAFARI ZA NDEGE KUTOKA NAIROBI – MSUMBIJI

Shirika la Ndege la Kenya (KQ) limeanza tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Nairobi na Maputo ya Msumbiji ili kusaidia kuimarisha mawasiliano ya ndani ya Afrika. KQ imesema safari hizo tatu za ndege kila wiki, Jumatano, Ijumaa, na Jumapili, zitahudumia wasafiri wanaotoka Kenya na zitatumika kama njia rahisi ya kuunganisha abiria […]

ANGUSHA MSWADA MALIZA WALIMU WA JSS

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro amelitaka bunge kuwazia upya marekebisho yaliyopendekezwa na kamati ya fedha katika mswada wa fedha. Kwa mujibu wa Nyoro baadhi ya idara zitaadhiriwa iwapo baadhi ya mapendekezo yataondolewa au kupunguza ambapo amepeana mfano na fedha zilizotengwa kuwaajiri walimu elfu 46 wa sekondari ya msingi JSS […]

WAZIRI WA FEDHA AANDIKA BARUA KWA BUNGE LA KITAIFA KUHUSU MSWADA WA FEDHA

Waziri wa fedha Prof. Njuguna Ndungu ameandikia bunge barua akieleza wasiwasi kwamba  mabadiliko katika mswada wa fedha utachangia kupungua kwa mapato ambayo serikali inalenga kukusanya Katika barua hiyo Hazina ya fedha imefichua kwamba kutopitisha mapendekezo ya hatua za ushuru zilizoainishwa katika Mswada wa Sheria ya Fedha, 2024, kunaweza kusababisha upungufu mkubwa wa mapato wa Shilingi […]

TUTAWATIBU MKIUMIA KATIKA MAANDAMANO; USHIRIKA WA MATIBABU 

Huku maandamano ya Occupy Bunge yakiingia siku ya pili, Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU)  umetangaza kushiriki kwa wanachama wake, kwa mpango wa kutoa huduma za matibabu kwa waandamanaji. Katibu Mkuu wa KMPDU Davji Atellah amesema madaktari watashughulikia watakaopata majeraha kwa dharura ambazo zinaweza kutokea kutokana na maandamano yaliyopangwa katika […]

USHURU KWA SODO? JAMANI!!!!

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino ameendea kukashifu serikali ya rais William Ruto Pamoja na mapendekezo ya mswada wa fedha. Akihojiwa katika kituo kimoja cha radio humu nchini babu amesikitikia hatua ya serikali kutaka kutoza kodi vitambaa vya hedhi yaani sodo bila kujali mathara yake kwa wasichana na kina mama huku kukiwa na tetesi kwamba […]

KINA MAMA TUJITEGEMEE

Kina mama katika kaunti ya transnzoia wamehimizwa kujiunga na vyama vya  ushirika na biashara ndogo ndogo ili kuimarisha uchumi wa taifa na mapato yao. Afisa wa mamlaka ya vyama vya ushirika Philomena Kirwa  akitoa mafunzo kwa wajane na wakongwe eneo mla Waigama wamesema wamama wana jukumu kubwa katika ukuaji wa uchumi Imetayarishwa na Janice Marete

“TUSHIRIKIANE KUMALIZA MAAMBUKIZI YA MARATHI” KATIBU WA AFYA MARY MUTHONI

Katibu wa idara ya afya ya umma Mary Muthoni amewataka wakenya kushirikiana na wahudumu wa afya wa kijamii ili kudhibiti maambukizi ya magonjwa mbali mbali kusambaa. Akizungumza katika kaunti ya Kisumu Muthoni amesema wahudumu hao wa kijamii wamepokea mafunzo muhimu na vifaa vya kuwawezesha kutoa huduma za kiafya katika kutibu marathi mbali mbali katika jamii. […]

FANYIA KIKOSI MABADILIKO LAMPARD ASEMA

Huku kikosi cha England kikijiandaa kumenyana dhidi ya Denmark katika mchuano wao wa pili wa makundi kwenye michuano ya Euro 2024, lejendari wa zamani wa kikosi hicho na klabu ya Chelsea Frank Lampard ametoa wito kwa kocha Gareth Southgate kufanya badiliko moja kwenye kikosi. Lampard amemtaka Southgate kufanya badiliko la kumuanzisha kinda Kobbie Mainoo katika […]

MICHUANO YA SHULE ZA SEKONDARI KAKAMEGA ZIMECHACHA

Kaunti ya Kakamega inajiandaa kwa mchuano mwingine wa kusisimua wa soka katika shule za upili, huku shule pinzani zikitarajiwa kuibua hisia zitakapokabiliana. Miamba wa soka wa shule za upili tayari wamefuzu kwa mechi za ngazi ya kaunti, zitakazong’oa nanga Alhamisi, Juni 20 katika mji wa Mumias. Mabingwa watetezi wa kaunti hiyo Shule ya Musingu wamepangwa […]

UKOSEFU WA PESA WATATIZA MICHEZO VIHIGA

Michezo ya Shule za Upili za Kenya (KSSSA) katika Kaunti ya Vihiga iliyokuwa ianze Jumatano, Juni 19, 2024 imeahirishwa hadi mwezi ujao kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Kulingana na Tom Justus Aura, Naibu Mwenyekiti wa KSSSA jimbo la Vihiga, mkutano wao na wakufunzi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ebusakami ulikatizwa na mawasiliano […]