CHELUGUI AZUNGUMZIA UPORAJI WA HUSTLER FUND

Waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogo ndogo Simon Chelugui amepuzilia mbali ripoti za matumizi mabaya ya fedha za mikopo ya hazina ya Hustler. Katika kikao na wanahabari, Chelugui amesema kwamba madai yaliyoibuliwa na Wakenya kuhusu utoaji mikopo kwa njia isiyofaa na kusababisha kufujwa kwa mamilioni ya fedha ni ya uongo. Kulingana na Chelugui, […]

WATANO WAFARIKI KWENYE MGODI RONGO

Watu 5 wamefariki baada ya ukuta wa mgodi kuporomoka na kuwaangukia walipokuwa wakichimba migodi katika eneo la Rongo kaunti ya Migori. Akithibitisha kisa hicho, Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo George Matundura, amesema watu zaidi wangali wamekwama kweny mgodi huo na kuongeza kwamba juhudi za uokozi zinaendelea. Aidha, ameahidi kwamba serikali itaweka mikakati ya […]

MAMBO NI MATATU, NAKHUMICHA KWA MADAKTARI

Wizara ya afya imetangaza kwamba itawaajiri madaktari wanagenzi 552 pekee kabla ya wengine kupewa nafasi baadaye kutokana na mapungufu katika bajeti ya mwaka hu. Katika taarifa, Waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema kwamba madaktari wengine wanagenzi zaidi ya 3000 watapewa nafasi wakati ambapo wizara hiyo itapata fedha zaidi. Kulingana na Nakhumicha, kwa sasa wizara hiyo […]

MIGORI: UOKOAJI WA MANSURA UNAENDELEA

Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Rongo kaunti yam IGORI George Matundura, amesema kwamba shughuli za uokoaji zinaendelea baada ya watu 18 waliokuwa wakichimba migodi katika eneo la Rongo kufunikwa na mgodi huo. Akithibitisha maafa hayo, Matundura amesema mkasa huo uliotokea majira ya saa saba usiku umewaua watu 5. Aidha, ameahidi kwamba serikali itaweka mikakati […]

WAKENYA 316 WAMEFARIKI KATIKA MATAIFA YA GHUBA TANGU 2002 – MUDAVADI

Waziri Mkuu wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi amesema kuwa takriban Wakenya 316 wamefariki wakifanya kazi katika mataifa ya Ghuba tangu 2002 hadi sasa. Akizungumza alipofika mbele ya kikao cha Seneti leo Jumatano, Mudavadi alisema wamesambaa katika majimbo sita kati ya manane. Mataifa hayo ni pamoja na Saudi Arabia yenye vifo 166, Qatar 58, Falme […]

WIZARA YA JKILIMO NA MIFUGO YAZINDUA MPANGO WA KUZALISHA NGOZI

Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo imezindua mpango wa shirikishi na sekta binafsi katika dhamira ya kuongeza uzalishaji wa ngozi maradufu ifikapo mwisho wa 2024. Hii inaambatana na utoaji wa ajira mpya takribani 100,000 ikiwa mpango mpya utatekelezwa, ambao pia unalenga kukuza uzalishaji wa bidhaa zinazohusiana na ngozi kama vile viatu ambapo nchi huzalisha […]

WADAU KATIKA SEKTA YA MADINI WALALAMIKIA KUBAGULIWA

Wadau wa sekta ya madini wamekashifu ubaguzi katika utoaji wa vibali na mfumo wa udhibiti usiofaa ambao unadhoofisha uwekezaji wa mabilioni ya fedha katika sekta ya uchimbaji madini Licha ya kuondolewa kwa zuio la miaka minne la kusitishwa kwa leseni, Oktoba mwaka jana, wawekezaji katika sekta hiyo wanakabiliwa na changamoto ya kupata vibali vinavyohitajika kutoka […]

GARETH SOUTHGATE APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate anasema Three Lions wanafahamu historia yao katika nusu fainali ya Euro 2024 wanapoelekea kwa mechi yao ya leo usiku dhidi ya Uholanzi huko Dortmund. Vijana wa Southgate wanalenga kutinga fainali ya michuano mikubwa katika ardhi ya kigeni kwa mara ya kwanza na kufisha kikomo ukame wa […]

RICE ASEMA WATAWAPIKU UHOLANZI

Declan Rice ana imani wana uwezo wa kuibwaga Uholanzi katika nusu fainali na hatimaye kunyakua ubingwa wao wa kwanza wa ulaya. Kiungo huyo wa kati wa Arsenal amekuwa nguzo ya Uingereza toka makala haya kuanza lakini anjihisi mtulivu kuelekea mechi ya leo mjini Dortmund, lakini anatarajia mchezo mgumu. Takwimu zinaonyesha wazi mchango wa Rice kwa […]

UHISPANIA NDANI YA FAINALI

Uhispania walifunga mabao mawili ndani ya dakika tano katika kipindi cha kwanza na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Ufaransa kwa bao la kuvunja rekodi kutoka kwa kijana Lamine Yamal na lengine la Dani Olmo na kuwafanya kutinga fainali ya Euro 2024. Yamal mwenye umri wa miaka 16 alifuta bao la kwanza la Randal Kolo […]