UJUMBE WA RUTO, RAILA KWA GEN Z

Rais William Ruto na kinara wa Azimio Raila Odinga wamesema kwamba matatizo yanayolikabili taifa yatatatuliwa kwa njia ya mazungumzo, baadhi ya masuala ya kuangaziwa yakiwa ni ufisadi, madeni ya taifa, usimamizi wa uchumi na ukosefu wa ajira. Kikao cha mazungumzo pia kitakuwa na wawakilishi wa sekta mbali mbali kama vile vyama vya miungano ya wataalamu, […]

RUTO AFUNGUA NJIA KWA IEBC

Rais William Ruto ametia saini mswada wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwa sheria, na hivyo kutoa nafasi kwa kubuniwa kwa jopo la uteuzi wa makamishna wapya wa tume hiyo. Hafla hiyo imeandaliwa katika jumba la mikutano KICC, Rais akiwa ameandamana na Naibu wake Rigathi Gachagua, aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga na makamu […]

SERIKALI IKO TAYARI KUKABILIANA NA WALAGHAI KATIKA IDARA YA ARTHI

Katibu wa arthi Nickson Korir amesisitiza mageuzi yanayofanywa na serikali katika juhudi za kurahisisha shughuli za arthi humu nchini. Amethibitisha kwamba makampuni mengi ambayo yamekuwa yakiwalaghai wakenya kwa muda mrefu yatafutiliwa mbali na kuahidi kuhakikisha kwamba wamiliki na miamala ya arthi humu nchini inafanyika kwa uwazi. Imetayarishwa na Janice Marete

KAMATI YA FEDHA YA BARAZA LA MAGAVANA LADAISHA MGAO WAO

Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandez Baraza ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya fedha katika baraza la magavana ameitaka afisi ya msimamizi wa bajeti na hazina kuu kuharakisha kutuma mgao wa serikali za kaunti ili kuwezesha serikali hizo kutekeleza miradi ya maendeleo bila matatizo yoyote. Imetayarishwa na Janice Marete

IEBC ILIKUWA AIBU 2022, SULUHISHO ZINAWEZA KUPATIKANA – RAILA

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema si mara ya kwanza kuwa na matatizo na IEBCRaila amesema hayo alipohudhuria kutiwa saini kwa Mswada wa IEBC (Marekebisho) kuwa sheria katika KICC. Kiongozi wa chama cha ODM ameongeza kuwa katika uchaguzi uliopita, Wakenya walikuwa na aibu kwa kile IEBC ilifanya. Imetayarishwa na Janice Marete

WEMBE NI ULE ULE ;MALALA AWAAMBIA MAGAVANA

Katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophus Malala ameibua mjadala wa kuwataka magavana kufutilia mbali mgao wao wa bajeti katika afisi za mabibi au mabwana zao. Kulingana na Malala magavana wanapaswa kuiga mfano war ais Ruto kwa kufutilia mbali mgao uliotengewa mama wa taifa bi Rachel Ruto na mkewe naibu wa rais Dorcus Gachagua. Imetayarishwa na Janice […]

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUPUNGUZA MATUMIZI

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro ametoa wito kwa taasisi za umma kutafuta namna ya kupunguza gharama ili huduma muhimu za umma zipewe kipaumbele kwa kutengewa bajeti. Kwa mujibu wa Nyoro kamati ya fedha Pamoja na hazina ya Taifa wanatafuta namna ya kuainisha matumizi ya fedha za umma ikiwemo kupunguza […]

DE LA FUENTE AMEZEA USHINDI KATIKA NUSU FAINALI YA EURO

Kocha wa Uhispania Luis de la Fuente ana imani na kikosi chake watakapo menyana na Ufaransa katika nusu fainali ya Euro 2024 hii leo. Huku wakiwa na wimbi la ushindi mara tano mfululizo, Uhispania wamemulika mchuano huo, wakifunga mabao 11 kwenye njia ya kutinga nusu fainali. Ufaransa wamefikia hatua hiyo licha ya kukosa ustadi wa […]

ZETECH WAPANIA KUBEBA LIGI YA VIKAPU

Licha ya kufuzu kwa fainali ya Ligi Kuu ya Kitaifa ya Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Kenya kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Zetech Sparks Jumapili kwenye Uwanja wa Nyayo Gymnasium, kocha mkuu wa Equity Hawks Benson Oluoch alisema walikuwa na mwanzo mbaya ambao walirekebisha katika kipindi cha pili.  Wanabenki waliwapiga wanafunzi kwa nyundo […]

KOYONZO WATAREJEA KWA KISHINDO ASEMA KOCHA OKWEMBA

Kocha mkuu wa mchezo wa raga wa wachezaji saba wa Shule ya Sekondari ya Koyonzo Eliud Okwemba ameahidi kurejea kwa kishindo katika Michezo ya Mpira wa Shule za Sekondari Kanda ya Magharibi baada ya kushindwa kutetea taji lao la kaunti. Okwemba anasema kokosa kujiamini miongoni mwa wachezaji wake na ulinzi duni nido  sababu za kushindwa […]