RUTO AMHAKIKISHIA JUMWA WADHIFA SERIKALINI

Rais william Ruto amemhakikishia aliyekuwa Waziri wa jinsia Aisha Jumwa kwamba hatamuacha nje ya serikali yake licha ya kumtimua kutoka baraza la mawaziri. Rais ametoa hakikisho hilo akiwa kwenye ziara ya maendeleo katika kaunti ya Kilifi, ambako Jumwa amempongeza rais kwa kuwatetua mawaziri wawili kutoka mwambao wa pwani. Aidha, Jumwa ameahidi kushirikiana na mawaziri hao […]

DENI LA TAIFA HUENDA LIKAONGEZEKA

Wakopeshaji wa ndani wanafaidika na chaguzi ndogo za ufadhili za serikali kwa mwaka huu wa kifedha ili kusukuma faida kubwa katika soko la deni la ndani. Wachanganuzi wa masuala ya fedha wanahofia kwamba huenda hali hiyo ikazidisha hali ya deni la nchi kwa sasa katika asilimia 70 ya Pato la Taifa (GDP) au Trilioni 10.4 […]

WANGA; RAILA BADO NDIYE KIONGOZI WA AZIMIO

Gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga na mbunge wa kasipul Charles Ongondo Were wamewasuta badhi ya viongozi katika mrengo wa azimio kwa madai ya kupindua uongozi wa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika muungano huo. Wanga amekashifu viongozi hao akitaja hatua ya wao kusema kwamba Kalonzo ndiye atakayeongoza mrengo huo kuwa mapinduzi […]

MJOMBA AZIDI KUNAWIRI

Baada ya kutundika buti zake kama mchezaji wa Equity Hawks mwishoni mwa msimu wa 2022-2023 na kujiunga na timu ya makocha kama kocha msaidizi, Samba Mjomba hakuwahi kufikiria kwamba angeiongoza timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ya Kikapu ya Kitaifa ya Wanawake ya Kenya. Mjomba, ambaye alishinda taji la ligi na Equity Hawks kama […]

SIKUBALIANI NAO KATU!

Kocha mkuu wa klabu ya shule ya upili ya Ebwali Francis Muhambe amekashifu tangazo la serikali mwaka jana la kuwapandisha vyeo moja kwa moja walimu ambao timu zao zitashiriki katika mashindano ya kitaifa ya Chama cha Michezo cha Shule za Sekondari Kenya (KSSSA), kuwa sababu kuu ya udanganyifu katika michezo ya shule. . Muhambe anasema […]

KENYA HARLEQUINS WAKO TAYARI KWA MSIMU UJAO

Mtaalamu wa mbinu wa Kenya Harlequins Paul Murunga ameelezea imani yake katika utayari wa timu hiyo kwa Christie Sevens inayotarajiwa kufanyika kati ya Julai 27 na Julai 28, 2024, katika Uwanja wa RFUEA, Nairobi. Wenyeji Kenya Harlequins, waliomaliza katika nafasi ya tano katika mzunguko wa mwaka jana, wako katika  kundi ‘C’ pamoja na mabingwa wa […]

INGWE WANAOA MAKUCHA

AFC Leopards imewasajili mshambuliaji Sydney Okale na kiungo mshambuliaji Julius Masaba kutoka Kariobangi Sharks ikiwa tayari kwa msimu mpya. Okale ameweka bayana kwenye mkataba wa mwaka mmoja, huku mchezaji wa klabu ya Masaba akiweka wino kwa mkataba wa miaka miwili ambao ungemhusisha na klabu hiyo hadi Julai 2026. Haya yamedhibitishwa na Katibu Mkuu wa Leopards […]

MAELEKEZO YATATOLEWA KATIKA KESI YA KUPINGA MSWADA WA FEDHA ULIOONDOLEWA

Mahakama ya Juu leo hii itatoa mwelekeo katika kesi ambapo mawakili na Wanasheria wa eneo la Mlima Kenya waliwasilisha kesi kupinga kutekelezwa kwa mswada wa fedha 2024-2025. Mnamo Juni, kundi la mawakili na Wanasheria wa Mlima Kenya walielekea mahakamani wakitaka amri ya kumzuia Rais William Ruto asiidhinishe Mswada wa Fedha na Ugawaji wa Fedha, 2024 […]

SERIKALI YATAKIWA KUWAHUSISHA WAKENYA KATIKA MASWALA MUHIMU YA TAIFA

Wakaazi wa kaunti ya Kisumu wanaitaka serikali kuwahusisha wakenya katika maswala mbali mbali ya kitaifa. Wakaazi hao wanasema kuwa maandamano ambayo yamekuwa yakishuhudiwa humu nchini hayangekuwepo ikiwa serikali iliwahusisha wananchi katika swala nzima la mswada wa fedha wa 2024/25. Imetayarishwa na Janice Marete

WANAOPINGA UTEUZI WA WANACHAMA WA ODM KUWA MAWAZIRI NI WACHOYO

Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Transnzoia wamewasuta viongozi wa mrengo wa azimio wanaopinga kuteuliwa kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho katika baraza jipya la mawaziri. Viongozi hao wanasema kuwa kinara wa azimio Raila Odinga amejumuisha baadhi ya Viongozi katika baraza hilo kama njia moja ya kuafikia ugavi sawa wa raslimali za taifa. […]