MWANARIADHA WA UGANDA REBECCA CHEPTEGEI AFARIKI DUNIA

Mwanariadha wa uganda Rebecca Cheptegei amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret alipokuwa akipokea matibabu kutokana na majeraha ya moto aliyopata baada ya kushambuliwa na mpenzi wake wa zamani. Cheptegei ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 33. Kaimu Mkurugenzi wa hosipitali ya Moi Dkt Owen Menach amethibitisha kufariki kwake usiku wa […]

SINNER AFIKA FAINALI

Mchezaji nambari moja duniani Jannik Sinner amefika nusu fainali yake ya kwanza ya US Open kwa ushindi wa seti nne za 6-2, 1-6, 6-1, 6-4 dhidi ya bingwa wa 2021 na mshindi wa pili mara mbili Daniil Medvedev. Sinner sasa atamenyana na Jack Draper wa Uingereza kutinga fainali. Sinner, 23, ndiye mchezaji pekee wa 10 […]

SUDAN YASHINDA

Sudan ilishinda kikwazo cha kutocheza nyumbani kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kuishinda Niger 1-0 katika mechi ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025. Sudan ilikuwa mwenyeji wa Niger mjini Juba, mji mkuu wa nchi jirani ya Sudan Kusini, na bao la dakika ya 51 kutoka kwa Abo Eisa mwenye […]

VILABU VIJIPANGE UPYA

Kuahirishwa kwa mwanzo wa msimu wa ligi ya kitaifa ya daraja la pili soka ya wanaume NSL ni baraka kwa kuwa kutasaidia vilabu kufuata sheria mpya za CAF, huu sio usemi wangu bali wa kocha wa Luanda Villa Gilbert Selebwa. Msimu wa NSL 2024/25 utaanza Septemba 21 baada ya kuahirishwa kwa wiki mbili na Shirikisho […]

TUPO TAYARI

Katibu Mkuu katika wizara ya Michezo Peter Tum amethibitisha kuwa serikali itaunga mkono tu mashirikisho yanayozingatia sheria zinazoongoza utendakazi wao. Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Nairobi City Marathon hapo jana, TUM alisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika mashirikisho ya michezo. Tum pia alisisitiza kuwa mashirikisho lazima yapeane kipaumbele maendeleo ya chipukizi katika taaluma […]

OLUNGA NJE AMA NDANI

Kocha Engin Firat anasubiri kwa hamu kujua ikiwa nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga atashiriki mechi ya kesho ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 au la, huku akisubiri matokeo ya majaribio ya utimamu wa mwili wake baadaye leo. Kenya itamenyana na Zimbabwe kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala – Uganda lakini Firat […]

BURIANI REBECCA

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amefariki dunia. Alifariki katika Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi mjini Eldoret ambapo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Kaimu Mkurugenzi wa MTRH Dkt Owen Menach alithibitisha kufariki jana usiku baada ya viungo vyake vyote kuharibika Alisema hospitali itatoa ripoti kamili kuhusu suala hilo baadaye mchana Cheptegei alipata […]

IPOA: WANAHABARI MKO SALAMA

Afisa mkuu mtendaji wa mamlaka huru ya kuangazia mienendo ya maafisa wa polisi IPOA Elema Halake ametoa hakikisho la usalama kwa mwanahabari wa Nakuru Catherine Wanjeri aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya kupinga mzigo wa ushuru. Akizungumza katika warsha ya kuwahamasisha wanahabari kuhusu usalama wao jijini Nakuru, Halake amesema tayari IPOA imeanzisha uchunguzi […]

MAFURIKO YAZUA HOFU NAKURU

Hofu ingali imetanda katika eneo la Kaptembwo kaunti ya Nakuru baada ya mtu mmoja kufariki na makumi ya familia kuachwa bila makao kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa. Sammy Tarus amepoteza uhai baada ya kusombwa na mafuriko kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret, vidimbwi sasa vikiwa vimeanza kuchimbika kando kando mwa barabara hiyo na […]

TUKO PABAYA KIFEDHA, SRC

Mwenyekiti wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC Lynn Mengich ameibua hofu kuhusiana na kiwango cha juu cha fedha zinazotumiwa katika kulipa mishahara, ambacho kwa sasa ni asilimia 43 ya mapato ya serikali. Akizungumza na wanahabari, Mengich amesema matumizi ya fedha za serikali yamekuwa yakiongezeka licha ya juhudi za serikali kubana matumizi. […]