JUNIOR STARLETS YAICHAPA UGANDA 3-0

Timu ya taifa ya wasichana U-17 Junior Starlets imeicharaza Uganda 3-0 katika Uwanja wa Nyayo, ikifuzu kwa raundi ya tatu ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA U-17. Brenda Achieng alifunga mabao mawili, huku Patience Asiko akipachika moja mapema dakika ya 4. Ushindi huu unakamilisha jumla ya 5-0 kwa mechi zote mbili baada ya ushindi […]

MGOMO WA WAUGUZI KUWAKUMBA WAGONJWA

Wagonjwa wanaotegemea huduma za wauguzi huenda wakaathirika kuanzia Aprili Mosi mwaka huu kutokana na mgomo wa wauguzi. Muungano wa wauguzi, ukiongozwa na mwenyekiti Seth Panyako, umesema kuwa mgomo huo unatokana na mikataba duni ya ajira inayowaathiri wauguzi. Imetayarishwa na Janice Marete

PIGO KWA POLISI KESI YA LSK KUENDELEA

Ni pigo kwa polisi baada ya Mahakama Kuu kukataa ombi lao la kufutilia mbali kesi ya chama cha wanasheria nchini LSK kuhusu madai ya ukiukaji wa maadili wakati wa maandamano ya mwaka jana. Jaji Lawrence Mugambi ameamua kuwa taratibu za ndani haziwezi kushughulikia ukiukaji wa haki za kimsingi. LSK inataka maafisa wawajibishwe kwa kifo cha […]

MISRI YAWASILISHA OMBI LA KUANDAA BAADHI YA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA

Misri imeomba haki ya kuandaa seti ya mechi za hatua ya makundi kwa Kombe la Dunia la 2034ambalo litafanyika Saudi Arabia, rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo ya Afrika alisemaJumatano. Mashindano hayo yataadhimisha miaka 100 ya Misri kuwa taifa la kwanza la Kiafrika kushirikiKombe la Dunia, baada ya kuonekana kwao katika toleo la […]

ARSENALI YAZIDIDHA MAKALI KWA KUWALAZA PSV EINDHOVEN

Arsenal imekamilisha ushindi mnono wa mabao 9-3 dhidi ya PSV Eindhoven na kutinga robofainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Mabingwa Real waliwashinda wapinzani wao wa mji mkuu Atletico Madrid kwa mikwaju yapenalti – na Arsenal huenda ikalazimika kupata gia ya juu dhidi ya wababe hao wa Uhispaniakatika hatua ya nane bora […]

MUTURI ATOA SABABU ZA KUKOSA VIKAO VYA BARAZA LA MAWAZIRI

Huku tetesi zikiendelea kuibuka kuhusu hatua ya waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi kuendelea kukosa kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri, waziri huyo amejitokeza na kusema kuwa alimwandikia waraka Rais William Ruto amruhusu asiwe akihudhuria vikao hivyo hadi suala la utekaji nyara na mauaji ya kiholela yatakapoorodheshwa kama miongoni mwa ajenda ya vikao hivyo. […]

KAGWE AAGIZA KUHARIBIWA KWA MBOLEA

Katika juhudi za kulinda ubora wa pembejeo na kuimarisha uzalishaji wa chakula, waziri wa kilimo na mifugo Mutahi Kagwe ameagiza kuharibiwa kwa magunia 27,518 na mbolea ambayo muda wake wa matumizi umepita ilhali ingali katika maghala ya nafaka kote nchini. Kupitia taarifa mapema leo, Kagwe amesema zoezi la kuharibiwa kwa mbolea hiyo litasimamiwa na shirika […]

MWANAMME ‘ARUKA’ KUTOKA GHOROFANI NA KUFARIKI

Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamme mmoja ameripotiwa kuruka kutoka ghorofa ya 4 ya jengo moja kwa barabara ya Tom Mboya katikati mwa jiji la Nairobi na kuangukia roshani ya jengo hilo kabla ya kufariki papo hapo. Imearifiwa kuwa mwanamme huyo alikuwa chumbani na mtu ambaye hadi sasa hajafahamika, na polisi wanachunguza kubaini iwapo ni mauaji […]

WANAFUNZI WAATHIRIKA NA CHANGAMOTO ZA CBC

Wanafunzi wanakumbwa na changamoto katika utekelezaji wa mtaala wa umilisi (CBC), huku serikali ikihimizwa kuchukua hatua za dharura kuzitatua. Muungano wa wazazi unasema gharama ya juu ya utekelezaji wa mtaala huo ni miongoni mwa changamoto ambazo bado hazijashughulikiwa ipasavyo, jambo linalowaathiri moja kwa moja wanafunzi. Imetayarishwa na Janice Marete

SERIKALI YALINDA HAKI NA USALAMA WA WAHAMIAJI

Wahamiaji wana mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo serikali imeanzisha mikakati ya kuimarisha usalama wao. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji, George Owili, juhudi hizi zinajumuisha kulinda haki za raia wa kigeni wanaoingia nchini pamoja na Wakenya wanaosaka ajira nje ya nchi. Imetayarishwa na Janice Marete