SALASYA HURU TENA

Mbunge wa Mumias East Peter Salasya ameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 200 baada ya kukesha kwenye seli za polisi wikendi nzima. Salasya amefikishwa katika mahakama ya Milimani ambako amefunguliwa mashtaka ya uchochozi, mawakili wake wakidai kuwa haki zake zilikandamizwa wakati wa kukamatwa kwake. Akizungumza na wanahabari nje ya mahakama, Salasya ameitaka idara ya […]

KENYA YAZUNGUMZIA KUFURUSHWA KWA KARUA

Serikali imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi na wakenya kwa jumla wanatoa kauli za uchochezi, ikisema matamshi ya baadhi ya viongozi yanafufua makovu ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amewakosoa viongozi hao ambao hakuwataja, akisisitiza serikali itafanya kila iwezalo […]

KWANINI TUMEMKAMATA NATEMBEA- EACC.

Gavana wa Trans Nzoia George Natembea, na maafisa wengine 4 wakuu wa serikali yake wanakabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa sheria katika kutoa malipo ya shilingi bilioni 1.4 katika utekelezaji wa miradi kadhaa ikiwemo ukarabati wa uwanja wa Kenyatta mjini Kitale na ujenzi wa makao makuu ya serikali ya kaunti hiyo. Haya ni kulingana na […]

WANAHARAKATI WAANDAMANA KUSHUTUMU TANZANIA

Baadhi ya wanaharakati wameandama nje ya afisi za ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi wakilalamikia hatua ya taifa hilo kuwazuilia na kisha kuwafurusha mawakili na wanaharakati waliokuwa wameelekea nchini humo kufuatilia kesi kuhusu uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini Tundu Lissu. Kulingana na wanahabarakati hao, hatua ya Tanzania sit u ukiukaji wa haki za kibinadamu, bali […]

WAKILI DORCAS ODUOR AOMBA KESI YA MAKAMISHNA IEBC IPINGWE

Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor ameweka pingamizi la awali dhidi ya kesi inayoipinga orodha ya Rais Ruto ya makamishna wa IEBC, akidai haijatimiza masharti ya kisheria na ilipaswa kutumia njia za kikatiba kwanza. Oduor anaitaka mahakama kutupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa ni ya mapema mno. Walalamikaji, Kelvin Omondi na Boniface Mwangi, wanapinga uteuzi huo wakidai […]

MARAGA NCHINI TANZANIA KUSHUHUDIA KESI YA TUNDU LISSU

Jaji Mkuu mstaafu David Maraga amewasili Tanzania kushuhudia kesi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama cha upinzani Chadema. Hii ni baada ya Martha Karua, Gloria Kimani na Lynn Ngugi kuzuiwa kuingia nchini humo na kurejeshwa Kenya. Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na hotuba ya kuhamasisha uasi kabla ya uchaguzi wa 2025. Chama chake […]

KOECH ATETEA UAMUZI WA TANZANIA KUMZUIA KARUA

Mbunge wa Belgut, Nelson Koech, ametetea hatua ya Tanzania kumzuia Martha Karua kuingia nchini humo, akisema kila taifa lina haki ya kudhibiti mipaka yake licha ya ujumuishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Koech, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Ulinzi, Ujasusi na Mahusiano ya Kigeni, amekiri kuwa tukio hilo ni […]

OLE NDIEMA ATAKA MSHIKAMANO NA MAOMBI KWA TAIFA

Mshikamano wa kitaifa umetajwa kuwa nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa, kwa mujibu wa aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Trans Nzoia, Henry Ole Ndiema. Ndiema ametoa wito kwa viongozi wa kidini kuendelea kuliombea taifa, huku akiwatahadharisha wanasiasa dhidi ya kutoa matamshi yanayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi. Imetayarishwa na Janice […]

MGONJWA AJINYONGA HOMA BAY, UCHUNGUZI WAANZA

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha kifo cha mgonjwa anayedaiwa kujinyonga katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay Marehemu, kwa jina Mike Juma, anaripotiwa kujinyonga ndani ya choo cha wodi alipokuwa akipata matibabu baada ya kulazwa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu. Kwa mujibu wa uchunguzi wa Polisi marehemu alikuwa ameacha kutumia dawa za […]

MVUA YAUA WATANO KUSINI MWA CHINA

Mvua kubwa imesababisha vifo vya watu watano na wengine kadhaa kupotea katika mikoa ya Guangdong na Guangxi nchini China. Mamlaka zimetoa tahadhari za mafuriko ya milimani na majanga ya kijiolojia. Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa kimetangaza tahadhari ya njano katika maeneo kadhaa kutokana na hatari ya mvua zaidi, huku mvua ikitarajiwa kuendelea hadi […]