VIONGOZI WAWASHAURI VIJANA WAJIHAMI KWA KURA

Viongozi mbali mbali nchini wametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kama wapiga kura katika zoezi linaloendelea nchini baada aya kuzinduliwa na tume ya IEBC. Akizungumza katika eneo bunge lake, mwenyekiti wa muungano wa wabunge wa Magharibi mwa nchi ambaye pia ni mbunge wa Sirisia John Waluke, amesema hiyo ndiyo njia ya pekee […]

VIJANA WAJITOKEZA KUSAJILIWA NA IEBC

Usajili wa wapiga kura wapya umeanza rasmi kote nchini, muda mfupi baada ya mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon kuzindua zoezi hilo katika eneo la Mashuru kaunti ya Kajiado. Wengi wa vijana wa kizazi cha Gen Z wameapa kutumia kura hizo kuwaadhibu viongozi wanaozembea kazini. Wakati uo huo, makundi ya […]

MWANASHERIA MKUU APEWA SIKU 14 KWENYE KESI YA BESSIGYE

Mahakama kuu imempa mwanasheria mkuu siku 14 za kuwasilisha tetesi zake kwenye kesi ambapo kiongozi wa upinzani nchini Uganda kanali mstaafu Kizza Besigye ameishtaki Kenya kutokana na kufurushwa kwake kutoka nchini. Kesi hiyo imetajwa hii leo ambapo mwanasheria mkuu alikuwa ametarajiwa kuweka wazi kujitolea kwake kutoa ushirikiano kwenye kesi hiyo, ila wakili wake akasema kwamba […]

PENGO LA MALIPO YA CHAI YA KTDA LAZUA GHASIA MIONGONI MWA WAKULIMA

Tofauti kubwa katika malipo ya bonasi ya chai na viwanda 77 vinavyosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Chai nchini (KTDA) imewakera wakulima, huku wengi wao wakirekodi mapato ya chini kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2025. Ripoti ya muda inaonyesha kuwa wakulima katika maeneo bunge 21 yanayolima chai walishuhudia kushuka kwa bei ya majani kwa kati ya senti 0.80 na shilingi 19.10, kwa kilo moja ya […]

ARSENAL YAPUNGUZA MWANYA, UTOVU WA NIDHAMU WABOMOA DARAJA

Klabu ya Arsenal ililazimisha ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya Newcastle dakika za lala salama, baada ya kuwa nyuma kuanzia kipindi cha kwanza kufuatia bao la kichwa la Nick Woltemade katika dakika ya 34. Mabao kutoka kwa Mikel Merino na Gabriel Magalhaes yalihakikisha kuwa the Gunners wanapunguza mwanya wa alama kati yao na vigogo Liverpool, […]

POLICE FC, NAIROBI UNITED WAFAIDI MABAO YA UGENINI

Klabu ya Police FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini KPL imejipatia nafasi katika awamu ya 2 ya mwondoano kwenye mashindano ya kuwania ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika, licha ya kichapo cha mabao 2:0 mikononi mwa Mogadishu City. Police walifuzu kwa faida ya bao la ugenini kufuatia ushindi wa mabao 3:1 katika mkondo wa […]

RISING STARLETS WAINGIA AWAMU YA 3, KUMENYANA NA TANZANIA

Timu ya taifa ya soka kwa akina dada wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Starlets wametinga awamu ya 3 kipute cha kufuzu kwa kombe la dunia baada ya kuwachabanga wenzao wa Ethiopia mabao 4-0 katika mkondo wa pili, na hivyo kufikisha jumla ya mabao 5-1. Katika mechi ya marudiano hapo jana kwenye uwanja wa Ulinzi […]

IEBC YAANZA USAJILI WA WAPIGA KURA

Zoezi la kuwasajili wapiga kura zaidi linafunguliwa rasmi hii leo, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikisema inalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni 6.3 katika zoezi hilo. Wanaosajiliwa ni wakenya walio na umri wa miaka 18 au zaidi, zoezi hilo likiendeshwa katika vituo vya huduma yaani Huduma Centers na afisi za usajili za IEBC […]

ODM: HATUTAKUWA TENA UPINZANI

Chama cha ODM kimesisitiza kuwa kitabuni serikali baada ya uchaguzi mkuu ujao na kwamba hakitakuwa tena kwenue upinzani. Kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Junet Mohammed, amesema chama hicho kimekuwa kwenye upinzani kwa muda mrefu na hivyo pana jana ya mabadiliko. Naye mwenyekiti wa kitaifa wa ODM Gladys Wanga ambaye pia ni gavana wa […]

UPINZANI WADAI NJAMA YA KUSAMBARATISHWA

Mrengo wa upinzani umeibua madai kwamba kuna njama ya kuusambaratisha mrengo huo kwa kuwashawishi baadhi ya viongozi wake wajiunge na serikali ili kumhakikishia Rais William Ruto muhula wa pili madarakani. Wakizungumza katika eneo la Isinya kaunti ya Kajiado, viongozi hao wakiongozwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua, wameshikilia kuwa jududi hizo hazitafaulu, na kwamba watafanya […]