GAVANA BARASA ACHAGULIWA KUONGOZA ODM KAKAMEGA

Gavana wa Kakamega Fernandez Barasa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Kakamega kufuatia uchaguzi wa mashinani wa chama hicho hapo jana. Barasa alitangazwa kuwa mshindi baada ya mrengo unaoongozwa na mbunge wa Lugari Nabii Nabwera na mwakilishi wa kike Elsie Muhanda kuondoka katika kituo cha kupigia kura, baada ya pendekezo lao la […]

TAHARUKI NAIROBI KUHUSU HOJA YA KUMBANDUA SAKAJA

Wawakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Nairobi wamepanga kuwasilisha bungeni hoja ya kumtimua kutoka afisini gavana Johnson Sakaja na naibu wake Njoroge Muchiri hii leo. Wawakilishi wadi wapatao 90 wameripotiwa kutia Saini hoja hiyo na hivyo kuzidi kiwango hitajika cha 41 ili kuwasilisha hoja hiyo bungeni. Miongoni mwa tuhuma zaidi ya 20 wanazoibua ni […]

WAKUU WA MBUGA YA NAKURU MAHAKAMANI

Mahakama jijini Nakuru imewaagiza maafisa wawili wakuu wa mbuga ya Wanyama ya Ziwa Nakuru kufika mahakamani kuhusiana na utekaji nyara wa mvuvi Brian Odhiambo, baada ya mashahidi wawili hapo jana kutoa kauli za kukanganya kuhusiana na tukio hilo. Kwenye vikao vya kusikiliza kesi hiyo, mashahidi 2 waliiambia mahakama kwamba waliwaona maafisa wa idara ya huduma […]

WAHADHIRI MOI WAENDELEA NA MGOMO

Mgomo wa wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Moi umeingia wiki ya tatu, huku muunganio wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU) na usimamizi wa chuo hicho wakikosa kuelewana. Naibu Chansela wa chou hicho, Profesa Kiplagat Kotut, ametoa hakikisho kuwa mgomo utapata suluhu, akisema mazungumzo mapya yanapangwa ili kushughulikia masuala yaliyowasilishwa na muungano. Hata hivyo, mazungumzo yaliyofanyika wiki iliyopita kati ya pande hizo mbili […]

AFISA WA SILAHA CENTRAL ATETEA SILAHA KWENYE KESI YA REX

Afisa mkuu anayesimamia hifadhi ya silaha katika kituo cha polisi cha Central amepuulizia mbali madai ya kufichwa kwa maelezo kwenye sajili ya bunduki kwenye Kesi ya mauaji ya Rex Masai. Akitoa Ushahidi mahakamani, Afisa huyo amekiri kwamba sajili hiyo ilikuwa na makosa kwani nyaraka hutengenezwa kwa Mikono basi ni kawaida kwa makosa kutokea. Licha ya […]

BARCHOK APATA PIGO MAHAKAMANI

Gavana wa Bomet Hillary Barchok amepata pigo baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kuitaka itoe amri inayozuia kukamatwa au kushtakiwa kwake kuhusiana na tuhuma za ufisadi zinazomwandama. Akitoa uamuzi wake, jaji wa mahakama kuu Bahati Mwamuye ameamuru kesi hiyo isikilizwe wiki ijayo. Kulingana na gavana huyo ambaye alikuwa ameagizwa kujiwasilisha mbele ya tume […]

AFISA WA KENYA AUAWA HAITI

Maafisa wa polisi wanane wa vikosi vya usalama vya Pamoja nchini Haiti akiwemo afisa wa Kenya wamejeruhiwa vibaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani ambako afisa huyo wa Kenya amefariki dunia kutokana na ajali hiyo.Kulingana na  msemaji wa operesheni hiyo, Jack Ombaka tukio hilo lilitendeka majira ya saa 5 jioni wakiwa kazini ambako magari yao mawili yaliyokuwa yakikokotana yalipata matatizo ya kiufundi kabla ya kugongana. Afisa huyo […]

KIUNGO AWASHINDIA LIVERPOOL PAMBANO NA ARSENAL

Ufundi wa aina yake katika upigaji wa ikabu wake kiungo wa Liverpool Dominik Szobozlai uliwapa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza alama 3 muhimu katika safari ya kutetea taji lao, walipomenyana na Arsenal katika uwanja wa Anfield hapo jana. Kiungo huyo wa Hungary aliipa Liverpool bao la pekee la timu na la mchezo […]

NAIROBI UNITED MBIONI KUJIIMARISHA KABLA YA LIGI

Klabu ya Nairobi United ambao wamepanda ngazi kushiriki ligi kuu ya Kenya, KPL wameimarisha juhudi za kuleta ushindani kwenye ligi hiyo, wakifanya usajili kadhaa akiwemo kiungo mkabaji wa KCB, Mwanzur Suleiman ambaye pia ni mmoja kati ya waliokuwa wakiwakilisha timu ya taifa Harame Stars katika mashindano  ya CHAN. United watashiriki sio tu katika ligi kuu ya kenya bali […]

TUZO, FEDHA ZA MOROCCO CHAN

Timu ya soka ya taifa Morocco imetia kibindoni kima cha shilingi milioni 455 baada ya kuvikwa taji la 3 ya ubingwa wa mashindano ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN yaliyokamilika Jumamosi usiku. The Atlas Lions waliibuka mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuwacharza Madagascar mabao 3:2 na kuwanyima fursa […]