LAGAT APATA PIGO MAHAKAMANI

Ni pigo kwa naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat baada ya mahakama kukataa kutupilia mbali kesi inayomshinikiza aondolewe afisini. Katika uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amesema mahakama kuu ina mamlaka ya kikatiba kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu masuala ya kikatiba yaliyo kwenye kesi hiyo. Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanaharakati Eliud Matindi, akitaka Lagat aondolewe […]

SERIKALI: WAKENYA HAWATAATHIRIKA NA AGIZO LA BIASHARA TANZANIA

Wakenya wanaofanya biashara nchini Tanzania hawataathirika na agizo jipya la utoaji lililotolewa na serikali ya taifa hilo kuhusu utoaji wa leseni lililoonekana kuwazuia raia wa kigeni kujihusisha na baadhi ya biashara. Kupitia taarifa, katibu mkuu katika wizara ya masuala ya Afrika Mashariki Dakta Caroline Karugu, amesema wamefanya mazungumzo na Tanzania ambayo imetoa hakikisho kuwa wakenya […]

KENYA YAZIHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUUNDA UTALII UNAOSTAHIMILI HALI YA HEWA

Naibu Rais Kithure Kindiki ametoa wito kwa nchi za Afrika kuwa na bidhaa anuai za utalii ambazo ni endelevu na zinazostahimili misukosuko ya nje, ikiwemo hali ya suitofahamu ya kijiografia na ushindani mkali kutoka maeneo mengine. Wito umetolewa alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 15 ya Utalii ya Magical Kenya jijini Nairobi, ambapo amesema soko la utalii la Afrika lina […]

CHELSEA KUMENYANA NA LIVERPOOL

Chelsea na Liverpool watatarajia kuelekea katika mapumziko ya mwezi Oktoba wakiwa na kasi kubwa watakapomenyana kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Hakuna upande unaoingia kwenye mechi kwa fomu ya kushawishi. The Blues walipata ushindi mmoja kati ya tano wiki hii, wakiichapa Benfica 1-0 kwenye Ligi ya Mabingwa kutokana na bao la kujifunga la Richard Rios. Wekundu […]

BUJEGO AAHIDI MATOKEO MAZURI

Akiwa bado na joto baada ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Kenya Police Bullets FC, mtaalamu David Bujego hajapoteza muda katika kuweka malengo ya ujasiri, akitangaza kuwa yeye ndiye mtu sahihi wa kuwaongoza mabingwa hao watetezi katika enzi mpya ya ubabe. Bujego, ambaye hapo awali aliwahi kuinoa Kibera Soccer Women na kwa […]

KIRWA ATUZWA

Kocha mkuu wa Timu ya Kenya katika Mashindano ya Riadha ya Dunia ya 2025 huko Tokyo, Japan, Julius Kirwa ameteuliwa kuwa Kocha wa Mwezi wa Septemba. Uongozi wa Julius Kirwa ulikuwa muhimu alipoiongoza Kenya kutwaa medali 11 za kuvutia, saba za dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba. Hii ilikuwa hatua ya kutoka kwa […]

WASHUKIWA ‘WALIOCHOMA VITUO VYA POLISI KUFAHAMU KESI JUMANNE

Washukiwa 6 wanaotuhumiwa na mashtaka ya kuteketeza kituo cha polisi cha Matuu na wengine 16 wanaokabiliwa na tuhuma za kuteketeza kituo cha polisi cha Makongeni watafahamu hatma ya kesi dhidi yao Jumanne wiki ijayo. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kuiambia mahakama kwamba ungali kukamilisha uchunguzi, na kwamba unalenga kufanyia marekebisho baadhi ya mashtaka. […]

SERIKALI YAPAMBANA KUWAREJESHA NCHINI WANAHARAKATI

Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ametoa hakikisho kuwa wizara ya masuala ya kigeni inafanya juhudi za kuwarejesha nchini wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo wanaodaiwa kutekwa nyara nchini Kampala walipokuwa kwenye msafara wa kampeni za mwaniaji wa urais nchini humo Robert Kyagulani maarufu kama Bobi Wine. Hakikisho la Murkomen limejiri baada ya mashirika ya haki […]

NPS: TUTAHAKIKISHA MAKURUTU WANASAJILIWA

Idara ya polisi imewahakikishia vijana waliokuwa wakilenga kujiunga na vikosi vya polisi kwamba inatafuta njia nyingine za kisheria ili kuendesha zoezi la usajili wa makurutu lililosimamishwa na mahakama kuu hapo jana. Kupitia taarifa, msemaji wa polisi Muchiri Nyaga amesema idara hiyo itaendelea kuheshimu wa mahakama, huku ikisaka njia mbadala kuhakikisha kuwa vijana 10,000 wanajiunga na […]

FAMILIA KILIFI YALILIA HAKI KWA MWANAO

Familia moja katika kaunti ya Kilifi inataka haki itendeke kwa binti yao mwenye umri wa miaka 15 aliyeaga dunia baada ya kudaiwa kupigwa na mwalimummoja wa shule ya msingi ya Gongoni. Kutokana na upasuaji wa maiti, ripoti ilibaini kwamba Anestine Tunje wagredi ya 8 alifariki kutokana na uvujaji damu wa ndani wa kichwa. Aidha, familia ya Anestine inaamini kwamba majereha […]