NDAKWA AIBUKA MSHINDI MALAVA

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imemtangaza David Ndakwa wa UDA kama mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge eneo bunge la Malava, na kumbwaga mshindani wake wa karibu Seth Panyako wa DAP-K. Kwa mujibu wa IEBC, Ndakwa amepata jumla ya kura 21,564 huku Panyako akifuata kwa karibu na kura 20,210 kwenye kinyang’anyiro kilichokumbwa na vurugu […]

SIMBA ATOLEWA MENO KUCHA BUNGOMA

Umaarufu wa kisiasa wa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula katika kaunti ya Bungoma umewekwa kwenye darubini, baada ya mgombeaji wa kiti cha uwakilishi wadi katika wadi ya Chwele-Kabuchai kupitia chama chake cha Ford Kenya kupoteza kwa mgombeaji huru Eric Wekesa. Wekesa aliyekuwa akiungwa mkono na gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, amepata jumla […]

WAMUTHENDE: NITAWATUMIKIA WOTE

Mbunge mteule wa eneo bunge la Mbeere North Leo Wamuthende, ameahidi kuwaunganisha wakazi wote wa eneo hilo na kutekeleza miradi ya maendeleo bila kujali miegemeo ya kisiasa atakapoanza kutekeleza majukumu yake. Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro kilicholenga kupima ubabe wa kisiasa kati ya naibu rais Kithure Kindiki na mtangulizi wake Rigathi Gachagua, Wamuthende […]

UDA, ODM ZADUMISHA VITI

Vyama vya serikali jumuishi ambavyo ni UDA na ODM vimedumisha nyingi ya viti vyake katika chaguzi ndogo za ubunge zilizoandaliwa jana, mgombeaji wa ODM katika eneo bunge la Kasipul Boyd Were akishinda kwa kura 16,819, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Philip Aroko aliyepata kura 8,476. Katika eneo bunge la Mbeere North, Leo Wamuthende wa […]

UPA YAONYESHA UDA KIVUMBI NYAMIRA

Chama cha UPA kinachohusishwa na aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, kimeonekana kudidimiza umaarufu wa UDA katika kaunti ya Nyamira, kufuatia ushindi wa wagombeaji wa UPA katika chaguzi 3 za uwakilishi wadi katika kaunti hiyo. Jeremiah Ongaro wa UPA amembwaga Francis Amenya wa UDA kwa kura 3,507 dhidi ya 2,292, hali sawa ikishuhidiwa katika wadi […]

DCP YAVUNA KWENYE CHAGUZI NDOGO

Chama kipya cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kimevuna pakubwa katika chaguzi ndogo za wadi mbali mbali, ikiwemo Kariobangi North kaunti ya Nairobi. Kwa mujibu matokeo yaliyotangazwa na IEBC, David Wanyoike wa DCP amepata kura 2,282, mgombea huru John Kimanzi akipata kura 1,956 huku vyama vya ODM na UDA vikifuata kwa mbali […]

WAGOMBEAJI WAZUILIWA KUINGIA KWENYE VITUO VYA UPIGAJI KURA

Baadhi wagombeaji na wafuasi wao wazuiliwa kuingia  kwenye vituo vya kupiga kura kwa nia ya kisingizio cha kulinda kura. Agizo hili limetolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC huku afisa wa uchaguzi eneo bunge la Kasipul ,Rebecca Abwakhu akisema hatua hiyo itazuia ghasia  katika uchaguzi mdogo unaoendelea . Agizo hilo linajiri baada ya […]

You also can show your intercourse toy allegiance through the

Lelo Intercourse Toys For Males Luxurious Male Sex Pleasure Merchandise I love an excellent buzzy, too, however the Magic Wand can be … slightly much! If you’ve found that common wand massagers leave you uncomfortably numb, give the Micro a strive. You also can show your intercourse toy allegiance through the use of the Micro […]

TAHARUKI NAROK TOWNSHIP

Mgombea kupitia chama cha DCP katika wadi ya Narok Township Douglas Makonde amelalamikia uvamizi uliofanyika usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake alipokuwa na mkutano na maanjeti wake. Awali kulishuhudiwa taharuki kufuatia uvamazi huo ukitia baadhi ya wapiga kura wasiwasi. Hali ya utulivu imerejea eneo hilo.   Imetayarishwa na Shadrack Maina

USHURU WA KAUNTI, SHERIA ZA SEHEMU MBALI MBALI ZALEMAZA SEKTA YA USAFIRI

Wito umetolewa kwa serikali kuweka mikakati ya kuoanisha  kwa haraka ushuru wa lori za kaunti na kukagua sheria zinazozuia uchukuzi ili kuongeza ufanisi na ushindani katika sekta ya usafiri wa barabarani kufuatia ripoti mpya ya Mamlaka ya Ushindani ya Kenya (CAK) na Benki ya Dunia. Tathmini hiyo aidha inaonyesha kuwa serikali ya kenya inafanya vyema ikilinganishwa na mataifa mengine ya  kipato cha […]