BAYERN MUNICH WAONJESHWA KICHAPO CHA KWANZA

Miamba wa soka nchini Ujerumani Bayern Munich walionja kichapo cha kwanza cha msimu baada ya kupeperushwa ugani Fly Emirates na wenyeji Arsenal, na kupokezwa kichapo cha mabao 3-1 katika kinyang’anyiro cha klabu bingwa bara Ulaya. Jurien Timber alianzisha matatizo kwa vijana wa Vincent Kompany kunako dakika ya 22 kupitia kichwa kutokana na kona kiki yake […]

STARS WALENGA KUJINUSURU NA TANZANIA

Timu ya taifa kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars watamenyana na Tanzania katika awamu ya semifainali ya mashindano ya kufuzu dimba la klabu bingwa barani Afrika AFCON kupitia ukanda wa CECAFA, licha ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia. Licha ya kichapo hicho, Stars walimaliza wa pili katika Group A, kutokanna […]

KENYA YATEULIWA KUWA MWENYEJI HSBC

Shirikisho la raga ulimwenguni limethibitisha kwamba Kenya itakuwa mwenyeji wa mechi za ufunguzi za HSBC SVNS 2, likiwa tukio la kihistoria kwa Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki. Kipute hicho kitakachosakatwa tarehe 14 na 15 Februari mwaka ujao jijini Nairobi kitapisha dimba la kimataifa la Sevens Circuit, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini Kenya. […]

UMASKINI WAONGEZEKA KENYA- RIPOTI

Hali ya umaskini imeendelea kuongezeka nchini katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, wakenya 125 pekee wakimiliki utajiri unaoweza kukidhi mahitaji ya wenzao milioni 42. Katika ripoti yake, shirika la Oxfam limebaini pengo kubwa lililoko kati ya maskini na matajiri, wakenya milioni 7 wakijipata katika hali ya umaskini katika kipindi hicho. Aidha, imebaini pengo katika sekta […]

BABAKE OJWANG’ ATAKA LAGAT AKAMATWE

Familia ya bloga na mwalimu Albert Ojwang’ aliyeuawa katika kituo cha Central Police jijini Nairobi sasa inamtaka naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanao. Katika hatikiapo mahakamani, babake Ojwang’, Meshack Ojwang’ anamtuhumu Lagat kwa kupanga utekaji nyara, mateso na mauaji ya mwalimu huyo mapema mwaka huu, akisema […]

DAP-K YATAKA MGOMBEAJI WA UDA MALAVA AZUIWE

Kinara wa chama cha DAP-K Eugene Wamalwa, ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kumwondoa mgombeaji wa UDA eneo bunge la Malava David Ndakwa kwenye orodha ya wagombeaji, kwa madai kwamba Ndakwa amechochea vurugu dhidi ya mgombeaji wa DAP-K Seth Panyako. Akizungumza mapema leo eneo hilo, Wamalwa amesema kuwa Panyako ameshambuliwa na wahuni usiku […]

MLINZI WA LIVONDO

Polisi katika eneo la Malava kaunti ya Kakamega wanachunguza tukio ambapo mlinzi wa mwanasiasa Stanley Livondo, amejeruhiwa usoni na kundi la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo. Imearifiwa kuwa kabla ya hapo, mlinzi huyo alivamiwa na wakazi kwa tuhuma za kuwahonga wapiga kura eneo hilo na kumlazimisha kuvua nguo zote, akishukiwa kuwa na kitita cha […]

UPIGAJI KURA MAENEO 22 WAANZA

Zoezi la upigaji kura katika maeneo 22 yanayoshiriki chaguzi ndogo limeanza rasmi hii leo, vituo vya kupigia kura vikifunguliwa saa 6am alfajiri na vitafungwa saa 5pm kwa mujibu wa sheria za uchaguzi. Miongoni mwa maeneo hayo ni kaunti ya Baringo, maeneo bunge ya Malava, Ugunja, Kasipul, Mbeere North na Magarini, tume huru ya uchaguzi na […]

IEBC: HAKUNA WAPIGA KURA WAPYA

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imepuzilia mbali madai kwamba wapiga kura wapya wamesajiliwa katika maeneo kutakakofanyika chaguzi ndogo hapo kesho ili kufanikisha wizi wa kura, ikisema hakuna wapiga kura wapya walio na uwezo wa kushiriki zoezi hilo. Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Marijan Hussein Marijan, amekariri kuwa sajili itayotumika ni ile ya […]

EACC YATAKIWA KUZUIA UNYAKUAJI WA ARDHI CHEPCHOINA

Wakaazi wa ardhi ambayo imekumbwa na utata ya Chepchoina kaunti nya Trans Nzoia wameitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya maafisa wa serikali ambao wamekuwa wakinyakua mashamba yao. Aidha wakaazi hao wamesema kuwa mgogoro huo huenda ukaleta vurugu ikiwa wizara ya Ardhi na usalama hazitaingilia kati kutatua […]