KOCHA MPYA WA POLICE FC AAHIDI KUREJESHA UBABE KLABUNI

Kocha mpya wa Police FC, Dusan Stojanovic, ameapa kurejeshaubabe wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) nakujenga kikosi chenye uwezo wa kushindana na vilabu vikubwabarani Afrika.Mtaalamu huyo raia wa Serbia alitambulishwa rasmi Jumapilijioni katika Uwanja wa Police Sacco, muda mfupi baada ya kikosichake kutoka sare tasa ya 0–0 dhidi ya Posta Rangers.Akizungumza kwenye […]

IDADI YA WALIOSAJILIWA NA IEBC KUFIKIA SASA

Ni wakenya 90,020 pekee ndio wamesajiliwa kama wapiga kura wapya katika zoezi linaloendeshwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC. Kwa mujibu wa ripoti ya tume hiyo, kaunti za Nairobi, Kiambu na Machakos zinaongoza kwa idadi ya waliosajiliwa kwa wapiga kura wapya 16,512, 9,917 na 4,026 mtawalia. Kufikia Oktoba 31, jumla ya wapiga kura […]

WAKULIMA WAPINGA ADA YA KUSAFIRISHA KUKU KWA SH20 MACHAKOS

Muungano wa Wafugaji  wa kuku Kenya (KPDA) umeibua wasiwasi kuhusu sheria mpya ya Kaunti ya Machakos ambayo imeweka  ada ya Sh20 kwa kila kuku anayehamishwa kutoka kaunti hiyo, na kuonya kuwa uamuzi huo utaharibu ufugaji wa kuku na kulemaza maisha katika eneo lote. Muungano huo, ambao unawakilisha wafugaji na wasindikaji wa kuku kote nchini, umeomba mkutano wa dharura na Gavana  wa […]

KCSE YAANZA LEO

Watahiniwa zaidi ya elfu 900 wanaanza rasmi mtihani wao wa kidato cha 4 KCSE hii leo, mtihani ulioratibiwa kufanywa hii leo ni ule wa kategoria ya kuandika. Kulingana na ratiba ya baraza la mitihani ya kitaifa KNEC, mtihani huo utakamilika tarehe 21 mwezi huu kwa karatasi ya 3 ya Fizikia. Waziri wa elimu Julius Ogamba […]

WANAFUNZI 14 MIONGONI MWA WAATHIRIWA MARAKWET

Wanafunzi 14 ni miongoni mwa watu 26 waliothibitishwa kufariki katika maporomoko ya ardhi katike eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet. Haya yanajiri huku shughuli za uokoaji zikiendelea huku zaidi ya watu 20 wakiwa hawajulikanani waliko kufuatia maporomoko hayo yaliathiri vijiji kadhaa mapema Jumamosi kutokana na mvua kubwa. Katibu mkuu katika wizara ya elimu Julius […]

WOLVES WAMNG’ATA KOCHA WAO PEREIRA

Klabu ya Wolves inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza EPL imempiga kalamu meneja mkuu Vitor Pereira baada ya kushindwa kushinda mechi hata moja katika mechi 10 za ufunguzi wa msimu. Pereira aliyetia Saini mkataba wa miaka 3 na kalbu hiyo mwezi Sptemba baada ya kuwaongoza Wanderers kuepuka kushushwa daraja msimu jana, aliandikisha pointi 2 pekee na […]

TIMU 32 KUJUA WAPINZANI WAO CAF, CONFEDERATIONS CUP

Macho yote yameelekezwa nchini Afrika Kusini ambako droo ya kipute cha klabu bingwa barani Afrika na kile cha CAF Confederations Cup kinaandaliwa, klabu 32 zikisubiri kuwafahamu wapinzani wao katika awamu ya makundi. Droo hiyo inayoandaliwa jijini Johannesburg itaanza saa nane kamili mchana saa za Afrika Kusini, ambazo ni saa saba za mchana Afrika Mashariki. Mabingwa […]

GOR WALAZIMISHWA KUTOA SARE

Klabu ya Gor Mahia ilitoka sare ya bao 1:1 na Ulinzi Stars katika mchuano wa ligi kuu KPL kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani hapo jana. Gor walianza vyema mchezo na kutamalaki kwa kipindi kirefu, ushirikiano wa Shariff Musa na Austin Odhiambo ukiwatatiza mabeki wa Ulinzi Stars, kabla ya juhudi zao kuzaa matunda katika dakika ya 6 wakati Felix Oluoch aliwaweka kifua […]

WAKENYA WATIA FORA NEW YORK, KIPCHOGE AMALIZA WA 17

Mkenya Benson Kipruto alikaza Kamba dakika za mwisho na kumweka nje mkenya mwenzake Alexander Mutiso na kuibuka mshindi wa mbio za New York City Marathon hapo jana katika kinyang’anyiro cha kihistoria. Kipruto aliandikisha muda wa saa 2, dakika 8 na sekunde 9, sekunde 0.16 mbele ya Mutiso na kuongeza taji hilo juu ya mataji mengine […]

IPOA YACHUNGUZA KIFO KITUO CHA POLISI

Mamlaka huru ya kuchunguza mienendo ya polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mshukiwa aliyeripotiwa kujitoa uhai katika kituo cha polisi cha Kisumu central. Kulingana na taarifa ya polisi, mwili wa mwendazake aliyetambuliwa kama Kelvin Oduor ulipatikana ukiwa unaning’inia kwenye dirisha la bafu la kituo hicho cha polisi. Marehemu alikuwa amekamatwa kwa madai ya wizi na vurugu na kushtakiwa kabla ya mahakama […]