SERIKALI YATHIBITISHA MAUAJI TANZANIA

Serikali imeanzisha uchunguzi katika mauaji ya mwalimu raia wa Kenya John Ogutu aliyeuawa kwenye ghasia za baada ya uchaguzi nchini Tanzania alikokuwa akifanya kazi kama mwalimu katika eneo la Kinondoni. Haya ni kulingana na katibu mkuu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo, akithibitisha mauaji hayo kwa mara ya kwanza huku familia ya Ogutu […]

SERIKALI KUPUNGUZA LISHE YA MIFUGO, KAGWE

Sekta ya kilimo inatarajiwa kuimarika chini ya mpango wa serikali wa kupunguza gharama ya vyakula vya mifugo kwa lengo la kuwasaida wakulima kuongeza uzalishaji. Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe, amefichua mpango huo anaosema utaboresha Maisha ya wakulima. Alikuwa akihutubu katika eneo la Manyatta kaunti ya Kiambu. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UFADHILI MDOGO WAONGEZA MADAI YA FIDIA

Maelfu ya wakenya walioathirika katika migogoro kati ya wanyamapori na binadamu wanaendelea kuteseka kutokana na uchelewashaji wa mara kwa mara na ufadhili mdogo, hatua ambayo imechangia ongezeko la madai ya fidia inayotokana na migogoro hiyo. Akiwa mbele ya kamati ya uhasibu bungeni, katibu mkuu katika idara ya wanyamapori Silvia Museiya, amesema licha ya sheria inayoongoza […]

MAN CITY WASHINDA HUKU BARCELONA WAKISHIKWA

Klabu ya Manchester City ilipata ushindi wa mabao 4-1 kiulaini dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani hapo jana, City ikiwa haijapoteza mechi hata moja kwenye mechi 4 za ufunguzi katika dimba la klabu bingwa barani Ulaya. Phil Foden alifunga mara 2 huku Erling Haaland akiunga bao lake la 5 katika mashindano hayo msimu huu, na […]

STARS KUMENYANA NA SENEGAL MWEZI HUU

Shirikisho la soka nchini Senegal limethibitisha kwamba timu ya taifa ya Senegal maarufu kama Lions of Teranga, itamenyana na Harambee Stars ya Kenya katika mechi ya kirafiki tarehe 18 mwezi huu katika uwanja wa MArdan Sports Complex nchini Uturuki. Mechi hiyo itaashiria kufufua kwa matumaini ya mashabiki ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona wawili hao […]

POLICE FC WAFYATUA UPYA

Kocha mkuu wa Police FC Dusan Stonajovic amesifu ari ya wachezaji wake baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Sofapaka kwenye mechi yake ya kwanza tangu alipotambulishwa rasmi kuwaongoza mabingwa hao Mshambuliaji wa zamani wa Sofapaka Edward Omondi aliifungia Police bao muhimu katika kipindi cha kwanza na kuwapa pointi tatu, matokeo yameiondoa klabu hiyo katika eneo la kushushwa daraja. Akizungumza baada […]

IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA YAZUA HOFU

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imeibua hofu kuhusu idadi ndogo ya wapiga kura wapya waliosajiliwa, IEBC ikiripoti kuwasajili wakenya elfu 90 pekee katika kipindi cha mwezi mmoja. Kwa mujibu wa tume hiyo, kaunti ya Nairobi inaongoza kwa wapiga kura wapya ambao ni 16,000, huku kaunti za Tana River, Marsabit, Isiolo na Samburu zikikosa […]

WATOTO 164 WALIFARIKI HOSPITALINI KIAMBU, DUALE

Watoto waliokuwa wakitaka kuzaliwa pamoja na mama zao ndio walioathirika pakubwa na mgomo wa madaktari katika kaunti ya Kiambu, zaidi ya Watoto 160 na akina mama zaidi ya 10 wakiaga dunia wakati wa uzazi katika kipindi cha mgomo huo. Akizungumzia athari za mgomo huo mbele ya bunge la kitaifa, Waziri wa afya Aden Duale amethibitisha […]

WANAFUNZI WARUSHIWA KIBARUA KUREJEA VYUONI

Kibarua sasa ni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma kurejea vyuoni baada ya wahadhiri wao kusitisha mgomo wa siku 49 uliokuwa umelemaza masomo na kusababisha maelfu ya wanafunzi kurejea makwao. Mgomo huo umesitishwa baada ya wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu kukubali kulipwa deni lao la shilingi bilioni 7.9 kwa awamu mbili jinsi serikali […]

SERIKALI HUZIMA UMEME, RUTO

Umeme ambao umekuwa ukipotea katika baadhi ya maeneo nchini kati ya saa kumi na moja jioni na saa nne usiku umekuwa ukizimwa na serikali kutokana na mahitaji ya juu ya umeme ambayo serikali haiwezi kutosheleza. Haya ni kwa mujibu wa rais William Ruto kwenye kikao na wakenya wanaoishi nchini Qatar, akisema Kenya inahitaji zaidi ya […]