RUSHWA, UFUJAJI TATIZO KUU- EACC

Utoaji na upokeaji rushwa ndilo kosa lililoripotiwa pakubwa nchini huku ufujaji wa fedha, ukiukaji wa maadili na udanganyifu katika ununuzi yakiwa masuala yaliyochunguzwa na tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC katika kipindi cha mwaka 2024-25. Haya ni kulingana na ripoti ya tume hiyo, ambayo pia imeonyesha maafisa wa umma kughushi vyeti vya masomo kupata […]

IEBC YATETEA CHAGUZI NDOGO

Chaguzi ndogo za hivi maajuzi ziliashiria utayari wetu kama tume kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 licha ya changamoto za hapa na pale za kiusalama. Ndiyo kauli ya tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC kupitia kwa mwenyekiti wake Erastus Ethekon, ambaye amehimiza ushirikiano wa washikadau ili kufanikisha uchaguzi huo mkuu. Nayo idara […]

WAIGURU AZINDUA UJENZI WA KMTC

Gavana wa kirinyaga Anne Waiguru amezindua ujenzi wa chuo cha mafunzo ya matibabu nchini   cha kwanza Kirinyaga, karibu na hospitali ya rufaa ya Kerugoya. Kulingana na gavana huyo  hatua hii inaonyesha ushirikiano kati ya serikali za kaunti na kitaifa. Mradi huu unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuwapa vijana elimu na ajira.ujenzi huo unaanza kwa […]

KALONZO KUSITISHA UUZAJI WA HISA

Kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka ameapa kusitisha uuzaji wa hisa za kampuni ya mawasiliano nchini. Kiongozi huyo ameahidi kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha kwa mpango ulioratibiwa na serikali wa kuuza hisa hizo unasitishwa. Aidha ameonya kwamba hatua hiyo inahyatarisha mali na uwekezaji wa taifa. Imetayarishwa na Jones Koikai

KENYA YAIPIKU NIGERIA KUONGOZA UKUAJI WA SEKTA YA KIBINAFSI AFRIKA

Kenya imerekodi mafanikio makubwa zaidi ya sekta ya kibinafsi kati ya mataifa makubwa ya kiuchumi barani Afrika mwezi Novemba, na kuongoza safu ya PMI ya S&P Global kwa alama 55.0. Kufuatia ripoti ya Finance in Africa, taarifa hiyo inaashiria ukuaji wa haraka zaidi katika miaka mitano, ukichochewa na kuongezeka kwa mauzo, maagizo mapya ya wateja, na kupunguza shinikizo la bei. Uganda ilifuatia kwa […]

MAKATO YA SHIF NA USHURU WA NYUMBA KWA FIDIA YA KUSITISHWA KWA KAZI SIO HAKI – MAHAKAMA

Mahakama ya Ajira na Mahusiano ya Kazi imetoa maamuzi kwamba kukatwa kwa Ushuru wa Nyumba na michango ya SHIF kutoka kwa fidia inayotolewa kwa kusimamishwa kazi kwa njia isiyo ya haki ni sawa na utendaji usio wa haki wa kazi. Hata hivyo, mahakama imethibitisha kwamba PAYE bado inatumika kwa manufaa kufuatia ripoti hiyo.Mahakama hiyo imefanya uamuzi huo katika mgogoro kati […]

WALIMU WA JSS KUPATA AJIRA MWAKA UJAO

Katibu wa wizara ya elimu, Julius Bitok, amewahakikishia walimu wa JSS waliokuwa chini ya kandarasi kwamba serikali itawapa ajira ya kudumu kunzia mwaka ujao wa kifedha. Bitok amewataka walimu hao kuwa na subira akisema kwa serikali itashughulikia matakwa yao. Imewtayarishwa na Jones Koikai

 SALLY BOLO:KIPIGO CHA GOR MAHIA MWAMKO WA KOGALO

Makamu wa rais wa Gor Mahia, Sally Bolo amesema kuwa kushindwa kwa mechi ya 98 ya mashemeji derby dhidi ya wapinzani wao AFCleopards, ni mwamko wa k’ogalo katika ligi kuu ya kenya. Kipigo cha gor mahia cha 1-0 dhidi ya ingwe kilimaanisha k’ogalo wameshindwa kushinda katika mashemeji derby katika makala matatu mfululizo, baada ya kushiriki […]

JOYCILINE AVUNJA REKODI

Joyciline Jepkosgei alikimbia mojawapo ya mbio kali zaidi za maisha yake aliposhinda marathon ya valencia katika muda wa rekodi wa saa 2:14:00. Mkenya huyo, mwenye umri wa miaka 31, alidhibiti mbio za wanawake kuanzia mapema na kumshinda mwenzake na bingwa wa dunia peres jepchirchir katika hatua za mwisho. Jepchirchir alivuka mstari kwa 2:14:43, na hivo […]

KALONZO KUANDIKISHA TAARIFA

Viongozi wa kenya kwanza sasa wanamtaka kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka kuandikisha taarifa na DCI kuhusu matamshi yake kuwa mkuu wa majeshi marehemu Francis Ogolla aliuawa.  viongozi hao wamesema ni sharti kalonzo achunguzwe ili athibitishe matamshi yake na iwapo yamechochewa kisiasa.  Imetayarishwa na Jones Koikai