SERIKALI YAWALIPA WACHAPISHAJI

Hatimaye serikali imetoa malipo ya shilingi bilioni 5.64 kwa wachapishaji wa vitabu, ikiwa ni sehemu ya deni la shilingi bilioni 11.4 ilizokuwa ikidaiwa na wachapishaji hao. Kupitia taarifa, taasisi ya ustawi wa mtaala nchini KICD na muungano wa wachapishaji KPA, umekiri kupokea fedha hizo kutoka kwa wizara ya elimu, hatua itakayofanikisha uchapishaji wa vitabu vya […]

SERIKALI, UPINZANI WALUMBANA KUHUSU 2022

Viongozi wa upinzani na serikali wameendelea kulaumiana kuhusu jinsi kampeni za aliyekuwa mwaniaji wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 kupitia tiketi ya Azimio Raila Odinga zilivyoshuhudiwa, chama cha Jubilee kikimtetea kinara wake Uhuru Kenyatta dhidi ya madai kwamba hakutoa fedha za kuwalipa maajenti. Kwenye kikao na wanahabari, Jubilee ikiongozwa na katibu mkuu Jeremiah […]

NYORO AKOSOA UFADHILI “USIOELEWEKA” WA ELIMU

Mjadala kuhusu ufadhili wa masomo ya shule za upili umechukua mkondo tofauti, mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro akitishia kuwaongoza wazazi kwenye maandamano ya kuishinikiza serikali kuongeza mgao huo anaosema ni mdogo na usioeleweka. Mbunge huyo amesisitiza kwamba serikali imeshindwa kuweka wazi kiwango halisi ambacho kila mwanafunzi anafaa kupokea, akisema huenda ikawalazimu wazazi kugharamia mapungufu hayo. […]

WAHUDUMU MAGARI: NA BADO!

Wahudumu wa magari mjini Busia wametetea hatua ya kupandisha nauli maradufu kwa wasafiri kutoka mjini humo kuelekea miji mingine, wakisema nauli itaendelea kuongezeka kwa kipindi cha wiki mbizi zijazo kutokana na idadi kubwa ya wasafiri. Haya yanajiri huku wasafiri wakilalamikia kiwango cha juu cha nauli wanayotozwa licha ya hali ngumu ya uchumi. Uhaba wa magari […]

WANAFUNZI 10 HOSPITALINI KUFUATIA AJALI KIMENDE

Wakati uo huo, wanafunzi 10 wa shule ya Bishop Okoth wamepelekwa katika hospitali ya kimisheni ya Kijabe kwa matibabu baada ya basi lao kuanguka katika eneo la Kimende kaunti ndogo ya Naivasha. Imearifiwa kwamba basi hilo lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi 46, lilikosa mwelekeo na kutoka nje ya barabara kuu ya Nairobi- Nakuru kabla ya kuanguka. Walioshuhudia […]

WATU 6 WAFARIKI, WENGINE WAJERUHIWA LONDIANI

Watu 6 wameaga dunia huku wengine 46 kujeruhiwa baada ya kuhusika kwenye ajali iliyohusisha basi na trela katika eneo la Fort Ternan kwenye barabara ya Londiani kuelekea Muhoroni mapema leo. Kamanda wa polisi kaunti ya Kericho James Ng’etich, amesema basi liligonga trela kutoka upande wa nyuma, magari yote yalipokuwa yakielekea upande wa Kisumu. Waliojeruhiwa wanatibiwa […]

JUBILEE YAMTETEA UHURU DHIDI YA ODM

Chama cha Jubilee kimejitokeza kumtetea kinara wake ambaye pia ni rais mstaafu Uhuru Kenyatta dhidi ya mashambulizi ya kisiasa kuhusiana na jinsi kampeni za aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga zilishughulikiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Kauli ya Jubilee imejiri kufuatia malumbano ya wazi kati ya katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna na mkurugenzi […]

NIGERIA WATINGA ROBO FAINALI AFCON

Super Eagles wa Nigeria walipaa juu kwa juu na kuingi robo fainali ya dimba la taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 baada ya kuwapepeta the Mambas wa Msumbiji kichapo cha mabao 4-0 nchin Morocco jana usiku. Mshambulizi wa Galatasaray Viktor Osimhen alifunga mara 2, Ademola Lookman na Akor Adams wakifunga moja kila mmoja na kuwapa […]

RATIBA YA KENYA CUP VOLLEYBALL YATOLEWA

Shirikisho la mchezo wa Voloboli KVF limethibitisha kwamba toleo la pili la ubingwa wa Kenya Cup Volleyball litaandaliwa kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 mwezi huu katika uga wa Kasarani Indoor Arena. Tangazo linaashiria mwanzo rasmi wa kalenda ya voliboli katika msimu wa 2025-26, ambapo timu za wanaume na wanawake zitashiriki. Aidha, shirikisho hilo limesema […]

BEATRICE CHEBET NJE YA UWANJA 2026

Mshindi wa nishani ya dhahabu 2 katika mbio za mita 10,000 na mita 5,000 katika mashindano ya Paris Olympics 2024 Beatrice Chebet atakuwa nje ya mashindano mwaka huu baada ya kuchukua likizo ya kujifungua. Haya ni kulingana na tangazo la ajenti wake, likimaanisha kwamba mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 hatatetea taji lake katika […]