KCSE 2025: WATAHINIWA 1,180 WAKOSA MATOKEO

Huku sherehe zikiendelea kuhusiana na matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka 2025, watahiniwa 1,180 hawana cha kufurahia baada ya wizara ya elimu kufutilia mbali matokeo yao kwa madai ya kuhusika na udanganyifu kwenye mtihani huo. Akizungumza katika shule ya AIC Chebisas kaunti ya Uasin Gishu wakati wa kutangaza matokeo hayo, Waziri wa elimu Julius Ogamba […]

KCSE 2025: IDADI YA A PLAIN YAONGEZEKA

Jumla ya watahiniwa 1,932 wa mtihani wa KCSE mwaka jana walipata alama ya A plain kwenye mtihani huo, ikiwa ni ongezeko la gredi hiyo ikilinganishwa na watahiniwa 1,693 waliopata A plain mwaka 2024. Haya ni kulingana na matokeo ya mtihani wa KCSE 2025 ambayo yametangazwa na Waziri wa elimu Julius Ogamba, akisema idadi ya watahiniwa […]

1,932 WAPATA A KCSE 2025

Watahiniwa 270,000 wa mtihani wa KCSE wa mwaka jana wamepata alama ya C+ na zaidi, ambayo ni alama ya wastani ya kuijunga na vyuo vikuu, ambayo ni asilimia 27 ya watahiniwa 993,000 waliokalia mtihani huo wa mwaka jana. Akizungumza baada ya kukabidhiwa matokeo hayo katika Ikulu ndogo ya Eldoret, Rais William Ruto ameweka wazi kwamba […]

ARSENAL WAPOTEZA NAFASI YA KIPEKEE

Viongozi wa ligii ya soka nchini Uingereza, EPL, Arsenal, walipoteza nafasi ya kupanua mwanya wa pointi 8 uongozini mwa ligi hiyo baada ya kutoa sare ya kutofungana dhidi ya Liverpool ugani Emirates Stadium. The reds ni mojawapo ya timu 2 pekee ambazo zimefanikiwa kuwacharaza vijana wa Mikel Arteta msimu huu, na walikaribia kuikabidhi kichapo cha […]

ROBO FAINALI ZA AFCON KUANZA LEO

Robo fainali za Kombe la Mataifa bingwa barani Afrika, AFCON, zinaanza leo huku mataifa 8 yakipigania nafasi ya kutinga nusu fainali. Algeria itavaana na Nigeria katika mechi kali, Algeria ikiwa haijapoteza mchezo wowote kwenye mashindano haya na inajivunia safu imara ya ulinzi. Nigeria, kwa upande wake, ina moja ya safu kali zaidi za ushambuliaji, ikiwa miongoni mwa timu zilizofunga mabao mengi zaidi hadi sasa.na ina rekodi nzuri katika […]

GOR MBIONI KUIMARISHA KIKOSI

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amethibitisha kwamba wachezaji zaidi wapo njiani kuelekea kwene klabu hiyo, baada ya kumsajili Jackson Dwang kutoka Posta Rangers Jumatano wiki hii. Kulingana na Rachier, klabu hiyo imemwagiza mkufunzi Charles Akonnor kutambua sehemu zinazohitaji kuimarishwa kikosini na kuchukua hatia mara moja. Mwenyekiti huyo amepinga taarifa kwamba Dwang amechukua nafasi ya […]

POLICE BULLETS WAREJEA KILELENI BILA MECHI

Kenya Police Bullets wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF-WPL baada ya kupewa ushindi wa mezani kufuatia wapinzani wao waliopangwa kukutana nao, KISPED Queens, kushindwa kufika kwa mechi hiyo. Ushindi huo wa mezani yaani walkover, uliotolewa Jumatano, umeipeleka Bullets kileleni wakiwa na pointi 22 baada ya mechi 10, na hivyo kufungua pengo dogo […]

RUTO: UPINZANI UNACHEZA PATA POTEA

Rais William Ruto ameukosoa muungano wa upinzani kutokana aanachokitaja kuwa kukosa ajenda na kucheza pata potea na masuala muhimu ya wakenya. Akizungumza kwenye kaunti ya Uasin Gishu wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa NYOTA, Rais Ruto amewatahadharisha vijana dhidi ya kutumika na viongozi wa kisiasa anaosema hawana suluhu kwa matatizo ya […]

JIJI LA MIJENGO OVYO

Imeibuka kwamba asilimia 55 ya majengo jijini Nairobi si salama na yamo katika hatari ya kuporomoka iwapo patatokea mtetemeko wa ardhi wa kiwango chochote. Haya ni kulingana na muungano wa watalaam wa mijengo, wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya waliohusika kwenye ujenzi wa jengo lililoporomoka mtaani South C wakati wa ujenzi na kuwaua watu wawili. […]

MATOKEO YA KCSE KUTANGAZWA LEO

Watahiniwa wa mtihani wa kitaifa KCSE mwaka 2025 wanatarajiwa kufahamu matokeo yao ya mtihani huo hii leo, ambayo yatatangazwa na Waziri wa elimu Julius Ogamba. Hafla hiyo itafanyika jijini Eldoret kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, watahainiwa 900,096 waliofanya mtihani huo wakipata mwelekeo kuhusu kozi watakazosomea katika vyuo vikuu. Wizara ya elimu imeahidi kuwa watahiniwa […]