UCL: INTER MILAN KUTAFUTA USHINDI DHIDI YA BODO GLIMT

Ligi kuu ya mabingwa barani ulaya hatua ya mwondoano itarejelewa hii leo kwa mkondo wa pili huku mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa, Inter Milan watakua nyumbani San Siro wakitafuta kubatilisha matokeo ya wiki iliyopita walipochapwa mabao 3-1 na Bodo Glimt. Inter lazima washinde mchezo wa leo ili kufuzu hatua nyingine. Mechi nyingine zitakazochezwa ni pamoja na […]

BARCELONA YAMSAJILI CHIPUKIZI AJAY TAVARES

Klabu ya FC Barcelona imemsajili mchezaji chipukizi Ajay Tavares kutoka akademi ya Norwich City. Tavares, mwenye umri wa miaka 16, anaripotiwa kuvutia vilabu kadhaa barani Ulaya. Norwich itapokea fidia ya malezi, ingawa haijathibitisha kiasi cha fedha kinachohusika katika makubaliano hayo. Mchezaji huyo alijiunga na Norwich akiwa chini ya umri wa miaka 12. Msimu uliopita alitokea […]

KATASI ANG’ARA LIGI KUU YA KPL

Kipa wa AFC Leopards, Humphrey Katasi, ameendelea kuwa tegemeo muhimu kwa timu hiyo katika msimu uliogubikwa na ushindani mkali. Akiwa na mechi 10 bila kuruhusu bao, Katasi anaongoza orodha ya makipa wenye mechi nyingi safi katika SportPesa Premier League na yuko katika nafasi nzuri ya kuwania tuzo ya kipa bora wa msimu. Katasi anaongoza kwa […]

KOCHA WA LUANDA VILLA AAMINI TIMU ITANUSURIKA NSL

Kocha mkuu wa Luanda Villa, Francis Chinjili, amesema ana imani kuwa timu yake itaendelea kusalia katika Ligi ya Daraja la Kwanza, maarufu kama National Super League. Chinjili amepuuza madai kuwa yuko chini ya shinikizo la kubadilisha hali ya timu hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha. Tangu achukue usukani Januari […]

VIONGOZI WA KENYA KWANZA KIPSIGIS WAMKOSOA GACHAGUA

Viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza kutoka jamii ya Kipsigis wamemkashifu aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake kuwa jamii ya Kalenjin haina kiongozi anayezungumza kwa niaba yake. Viongozi hao wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika bunge Seneti, Aaron Cheruiyot, wamesema kauli za Gachagua hazina msingi na zinalenga kuleta ubabe wa kisiasa ndani ya jamii hiyo. […]

MBUNGE MANYATTA AMKOSOA WAZIRI WA USALAMA

Mbunge wa Manyatta, Gitonga Mukunji, amemtaka Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen kuzingatia majukumu yake na kuacha kupuuza uchunguzi wa vurugu katika mikutano ya kisiasa. Akizungumza kwenye kituo kimoja cha runinga nchini Mukunji amekosoa kauli za Murkomen kuhusu mashambulizi yaliyoshuhudiwa katika mikutano ya kisiasa, ambapo Waziri huyo alidai kuwa raia na makundi ya upinzani wamepata gesi […]

WIZARA YA AFYA YAANZISHA UCHUNGUZI KUHUSU KIFO MUKUMU

Wizara ya Afya imeanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mama mjamzito kilichotokea katika hospitali ya kimisheni ya Mukumu, Kaunti ya Kakamega. Akizungumza mbele ya kamati ya bunge, Waziri wa Afya Aden Duale amesema wizara inafuatilia chanzo cha kifo cha Grace Wambui Misigo baada ya familia kudai kuwa wauguzi katika hospitali hiyo walimdhulumu wakati wa kujifungua hadi akafariki. […]

MAPENGO YA ESG YAENDELEA KWA WAFANYIKAZI KATIKA BIASHARA YA KILIMO NCHINI KENYA

Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Kenya, kikichangia takriban asilimia 22 ya Pato la Taifa na kuajiri kaya nyingi za mashambani, kulingana na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS). Katika miaka ya hivi majuzi, wawekezaji wa kimataifa na wa ndani, wadhibiti, na wanunuzi wamezidisha umakini wao kwenye viwango vya Mazingira, Jamii na Utawala […]

MZUNGUKO WA MWISHO KUELEKEA RAUNDI YA 16 UEFA

Mkondo wa mwisho wa kufuzu raundi ya 16 katika dimba la klabu bingwa bara Ulaya unasakatwa wiki hii, jumla ya mechi 8 zikisakatwa leo na kesho usiku. Katika pambano moja, Atletico Madrid watakuwa na kibarua cha kutegua msongamano dhidi ya Club Brugge, kufuatia sare ya mabao 3-3 katika mkondo wa kwanza, timu zote 2 zikiwa […]

SESKO AWEKA HAI MATUMAINI YA UNITED UEFA MSIMU UJAO

Benjamin Sesko alifunga bao la pekee la mchezo na kuwapa Manchester United ushindi muhimu na pointi 3 ugenini dhidi ya Everton jana usiku, na kuwaweka vijana hao wa Michael Carrick katika nafasi ya 4. Sesko alifunga bao jingine muhimu siku 13 zilizopita na kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham, na mara tena […]