WATAALAMU WA EBOLA WA AMERIKA WAWASILI KENYA

Wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka Amerika wamewasili nchini Kenya na kuanza maandalizi ya kituo maalum cha Ebola ambacho Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio amesema kitaanza kufanya kazi ndani ya siku saba zijazo. Ikulu ya White House imethibitisha kuwa Amerika inaandaa kituo maalum nchini Kenya kwa ajili ya kuwatenga raia wa […]

DCP YAMTAKA WAZIRI WA ELIMU KUJIUZULU

Chama cha DCP kinataka uchunguzi wa kina kufanyika kutokana kuhusiana na chanzo cha moto katika shule ya Upili ya wasichana ya  Utumishi. Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho Katibu mkuu John Metho ametaka wizara ya usalama kutoa taarifa ya kina kuhusiana na waraka wa serikali kukabiliana na majanga. Imetayarishwa na Hilda Ajema

GAVANA KIHIKA AAHIDI KUSAIDIA FAMILIA ZA WAATHIRIWA WA MOTO GILGIL

Huko Nakuru gavana Susan Kihika amesema serikali yake itashirikiana kikamilifu na serikali ya kitaifa katika kuzisaidia familia zilizoathirika na mkasa wa moto. Kauli yake imesisitizwa na Waziri   Murkomen akisema serikali inalenga kuwasaidia wazazi na wanafunzi na huduma za ushauri nasaha wakati huu ambapo zinaendelea kukumbwa na wakati mugumu. Imetayarishwa na Hilda Ajema

WAZIRI OGAMBA AZUNGUMZA KATIKA ENEO LA MKASA  WA MOTO HUKO GILGIL

Waziri wa elimu Julius Ogamba amesema kati ya wanafunzi 808 ambao walikua  katika shule ya  wasichana ya Utumishi huko Nakuru  wakati wa mkasa wa moto wanafunzi 79 wamejeruhiwa, huku 71 wakihudumiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini, saba wakiendelea kupokea matibabu. Akizungumza katika shule ya wasichana ya Utumishi Ogamba ametuma rambi rambi zake kwa familia na marafiki […]

NTSA KUZINDUA MFUMO WA KIDIJITALI WA KUTATUA MAKOSA BARABARANI

NTSA imesema itaanzisha mfumo wa kisasa wa utekelezaji wa makosa madogo ya barabarani kuanzia Juni 2026, katika hatua ambayo itawaruhusu madereva kupewa Arifa ya Polisi ya Uhalifu wa Trafiki ili  kuepuka kufika mahakamani.  Katika taarifa, Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ODPP, Mahakama na mashirika mengine ya […]

CRYSTAL PALACE YATWAA CONFERENCE LEAGUE NA KUANDIKA HISTORIA

Crystal Palace wameandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Europa Conference League, taji ambalo linaongeza mafanikio yao makubwa ya mwaka 2025. Kabla ya mwaka huu, Crystal Palace hawakuwa wamewahi kushinda taji lolote kubwa katika historia yao, lakini sasa wamefanikiwa kutwaa mataji matatu ambayo ni FA, Community Shield na Conference League ndani ya kipindi […]

ANTHONY GORDON AELEKEA BARCELONA KWA ADA KUBWA

Anthony Gordon yuko mbioni kujiunga na FC Barcelona baada ya bodi ya Newcastle United pamoja na wamiliki wao kutoka Saudi Arabia kukubali ofa rasmi ya uhamisho huo. Taarifa zinaeleza kuwa Barcelona italipa euro milioni 70 pamoja na nyongeza mbalimbali zitakazofikisha thamani ya dili hilo zaidi ya euro milioni 80 kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Gordon […]

ODEMBA AWAREJESHA MORANG’A NA SHIYONZO HARAMBEE STARLETS

Wachezaji Emily Morang’a na Vivian Shiyonzo ni miongoni mwa waliorejeshwa katika kikosi cha muda cha Harambee Starlets kilichotajwa na kocha Beldine Odemba kwa ajili ya mashindano ya mataifa manne yatakayofanyika Zambia. Odemba amedumisha sehemu kubwa ya kikosi kilichoshiriki mechi za hivi karibuni za kimataifa huku akiwajumuisha tena baadhi ya wachezaji waliowahi kuitumikia timu ya taifa […]

JULIUS YEGO ATAKA MASHINDANO ZAIDI YA KIMATAIFA NCHINI

Bingwa wa zamani wa dunia wa mkuki Julius Yego ametaka shirikisho la riadha nchini AK kuandaa mashindano zaidi yaliyoidhinishwa na shirikishi la riadha duniani humu nchini ili kuwasaidia wanariadha kufuzu kwa urahisi mashindano ya dunia ya mwaka 2027 yatakayofanyika Beijing. Kauli yake imejiri baada ya shirikisho la riadha duniani kutangaza viwango vipya vya kufuzu kwa mashindano hayo, ambapo wanariadha watalazimika kufikia […]

EMILY ADHIAMBO AIAMINI JUNIOR STARLETS DHIDI YA UGANDA

Mshambuliaji wa Junior Starlets Emily Adhiambo amesema ana imani Kenya itaifunga Uganda katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 17 itakayochezwa hapo kesho katika uwanja wa Nyayo. Kenya ilipata sare muhimu ya mabao 1-1 dhidi ya Uganda  katika mkondo wa kwanza uliochezwa Kampala, ambapo Adhiambo alifunga bao la kusawazisha baada ya […]