MWANAHARAKATI NJAGI, NDUGU WAWILI WAPATIKANA HAI

Ni afueni kwa familia za mwanaharakati Bob Njagi na ndugu wawili Aslam na Jamil Longton waliokuwa wametoweka kwa mwezi mmoja kupatikana wakiwa hai. Taarifa za kupatikana kwa watatu hao zimewekwa wazi na Rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Faith Odhiambo, ambaye amesema kuwa Njagi amejiwasilisha usiku wa manane katika kituo cha polisi cha Tigoni […]

MASENGELI AJIPATANISHA NA MAHAKAMA, AAHIDI USHIRIKIANO

Hatimaye naibu inspekta mkuu wa polisi katika kitengo cha polisi wa utawala Gilbert Masengeli, ameomba msamaha kwa mahakama iliyompata na hatia ya kupuuza mahakama alipodinda kufika mahakamani kutoa maelezo kuhusu walikokuwa wakenya 3. Masengeli ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu inspekta mkuu wa polisi, alihukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani ila kifungo hicho kikafutiliwa mbali kwa […]

KUNA NURU KWA KAUNTI, MGAO WAKARIBIA

Huenda masaibu ya kifedha ambayo yamekumba serikali za kaunti kwa kipindi cha miezi kadhaa yakafikia mwisho na kupisha tumaini, baada ya kuafikiwa kwenye mkutano kwamba mgao wa serikali hizo utatolewa hivi karibuni. Nyingi ya huduma kwenye serikali za kaunti zilikuwa zimelemazwa, ikiwemo kulipwa kwa mishahara ya wafanyakazi. Hata hivyo, afueni hii inajiri kutokana na mkutano […]

MAFUTA ‘MABOVU’ YANAUZWA NCHINI- KEBS

Kuna uwezekano kwamba wakenya wanatumia mafuta ya kupika ambayo hayaafikii viwango hitajika vya ubora, baada ya kubainika kwamba takribani lita milioni 32 za mafuta hayo zilizoagizwa kutoka Indonesia, Malasya na Misri yalikuwa na dosari. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya viwanda na biashara katika bunge la seneti, mkurugenzi mkuu wa shirika la kutathmini ubora wa […]

KANJA AAPISHWA KUWA INSPEKTA MKUU WA POLISI

Uongozi wa idara ya polisi umeimarika baada ya Douglas Kanja kuapishwa na kuanza majukumu yake rasmi kama inspekta mkuu wa polisi, na kujaza rasmi pengo lililoachwa na mtangulizi wake Japheth Koome. Hafla ya kumuapishwa imefanyika katika mahakama ya upeo jijini Nairobi, muda mfupi baada ya Rais William Ruto kumteua. Kanja atahudumu kwenye wadhifa huo kwa […]

MASENGELI AADHIBIWE KWA KUKAIDI AMRI ZA MAHAKAMA – WAKILI KHAMINWA

Hakuna aliye juu ya sheria, haya ni kwa mujibu wa Wakili John Khaminwa akimtaka Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli aadhibiwe kwa kutotii maagizo ya mahakama. Kulingana na Khaminwa hakuna aliye juu ya sheria kukataa kimakusudi kuheshimu amri za mahakama.Wakili huyo Mwandamizi amesisitiza kuwa amri za mahakama lazima zizingatiwe na wote na kuongeza kuwa […]

WATU WAWILI WAFARIKI KWA KUJITOA MHANGA UASIN GISHU NA HOMA BAY

Maafisa wa upelelezi wanachunguza visa viwili tofauti vya kujitoa mhanga vilivyoripotiwa katika kaunti za Uasin Gishu na Homabay mtawalia. Kisa cha kwanza ni cha Laban Kimeli ambaye mwili wake umepatikana katika nyumba yake katika kijiji cha Mogobich, Nandi, kisa ambacho kinashukiwa kuwa kujitoa mhanga. Kwa mujibu wa Maafisa wa Polisi waliotembelea eneo la tukio, alijifunga […]

GAVANA SANG AWAFUTA WAFANYIKAZI 1,100 WALIOAJIRIWA KINYUME CHA SHERIA ZA KAUNTI YA NANDI

Zaidi ya wafanyikazi 1,100 wa serikali ya kaunti ya Nandi waliopata ajira kinyume cha sheria wamefutwa kazi. Gavana wa kaunti hiyo Stephen Sang amesema bodi ya utumishi wa umma ya kaunti iko mbioni kubatilisha barua zote za ajira ambazo zilitolewa kinyume cha utaratibu. Wafanyikazi walioathiriwa, ambao majina yao yaliingizwa katika orodha ya mishahara ya kaunti […]

WAKAZI WA MATAYOS KAUNTI YA BUSIA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUMALIZA UHALIFU

Wito umetolewa kwa wakaazi wa Matayos kaunti ya Busia kuendelea kushirikiana na maafisa wa usalama katika kaunti hiyo katika juhudi za kukabiliana na utovu wa usalama ambapo umekithiri eneo hilo. Kamishina wa busia ameeleza kurithishwa na ushirikiano unaoendelea kati ya maafisa wa usalama na wazee wa vijiji akiwataka wakaazi kuimarisha ushirikiano ili kumaliza uhal.ifu katika eneo hilo. […]

UCHUNGUZI BAADA YA MOTO KUTEKETEZA DUKA LA BUNGE LA KAUNTI YA MIGORI

Polisi katika Kaunti ya Migori wanachunguza hali ambapo moto umeteketeza duka la bunge la kauntiKamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Suna Mashariki Ezekiel Kiche amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mfanyakazi wa bunge la kaunti alikuwa akichoma taka katika eneo la kuzoa taka moto huo uliposambaa hadi kwenye chumba cha kuhifathi chakula Kiche amesema […]