MASAIBU YA MOI HAYAISHI LEO- WAHADHIRI

Shughuli za masomo zimeendelea kutatizika katika chuo kikuu cha Moi, wafanyakazi na wahadhiri wakidai kutishiwa na usimamizi wa chuo hicho huku wakidai kuendelea na mgomo wao. Wakizungumza wakati wa mkutano wao jijini Eldoret, wahadhiri hao wakiongozwa na katibu mkuu wa UASU tawi la Moi Busolo Wekesa wamesema wamepokezwa Zaidi ya nyaraka 20 kutoka kwa chuo […]

MIA MBILI YA MAUTI

Mwanaume mwenye umri wa miaka 25 amefariki kufuatia mzozo wa shilingi 200 katika soko la Garissa Lodge, eneobunge la Kisumu ya kati. Inaripotiwa kuwa mzozo huo ulitokea baada ya wanaume hao wawili kuuza kiatu na kwamba walipaswa kugawana mapato. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kisumu ya kati Peter Mulai, mtuhumiwa, kwa jina Nicholas […]

KAUNTI YA NAIROBI KUPOKEA NYONGEZA YA MAJI ZAIDI YA LITA MILIONI 100

Uhaba wa maji katika kaunti ya Nairobi unatarajiwa kupungua kwa kiasi kikubwa kufuatia kukamilika kwa mradi wa northern Water collector tunnel. Wakaazi wa kaunti ya Nairobi wanatazamiwa kupokea lita milioni 100 000 40 za maji kutoka kwa mradi huo ambao unachukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa wakaazi ambao wamekuwa wakishuhudia uhaba wa maji kwa mda […]

WATANZANIA WAWILI WAKAMATWA KWA KUFANYA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU MJINI MOMBASA

Maafisa wa polisi kutoka Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) huko Mombasa wamewakamata raia wawili wa Tanzania kwa biashara haramu ya mifupa ya tembo yenye thamani ya shilingi million 3.3. Katika operesheni ya pamoja na maafisa kutoka Kituo cha Polisi cha Mtwapa, Paul Kuya, mwenye umri wa miaka 36, na Paul Telek, mwenye umri wa […]

WAKAAZI WA KAUNTI YA TRANSNZOIA WALALAMIKIA KUBAGULIWA KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TRANSNZOIA-SEBIT

Wakaazi wa kaunti ya Pokot magharib wameandamana kulalamikia kubagulia katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Transnzoia -Sebit. Wakazi hao wameitaka kampuni ya uchina ambayo inaendeleza ujenzi wa barabara hiyo kutokuwa na upendeleo wakati wa kutoa nafasi za ajira. Mwakilishi wa wadi ya Mnagei Richard Todosia ametoa wito kwa uongozi wa kampuni hiyo kushughulikia malalamishi […]

WADAU WAIBUA HOFU KUHUSU GREDI 9

Washikadau katika sekta ya elimu wameibua hofu kuhusiana na ukosefu wa utayari wa serikali kufanikisha masomo ya gredi ya 9 yanayoanza mwaka ujao, wakiitaka kuharakisha ujenzi wa madarasa na kuwaajiri walimu Zaidi wa sekondari msingi JSS. Wadau hao wanaojumuisha walimu na wazazi kote nchini, wamesema hadi sasa hawajapokea orodha ya mahitaji ya mtaala wa gredi […]

KINDIKI AMRITHI GACHAGUA, TENA

Uongozi wa chama cha UDA umepata sura mpya baada ya baraza kuu la chama hicho kumteua naibu Rais Kithure Kindiki kuwa naibu kinara wa chama hicho kuchukua mahali pake aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua. Gachagua ametimuliwa kutoka wadhifa huo baada ya kubanduliwa kutoka mamlakani na bunge la seneti na lile la kitaifa. Akipokea wadhifa huo, […]

MAGAVANA WALALAMIKIA KUCHELEWESHWA KWA MGAO WA KAUNTI

Magavana wa eneo la kaskazini mwa Kenya wameendelea kuilaumu serikali ya Kenya baada ya kuchelewesha mgao wa fedha za kaunti kutoka hazina kuu ya kitaifa. Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa gavana wa Kaunti ya Lamu Issa Timami amesema kuwa serikali za kiaunti hazina fedha za kuendeleza shughuli za kaunti ikiwemo kuwalipa wafanyikazi wa kaunti. Imetayarishwa na Janice […]

OGAMBA:TUTASHUGHULIKIA KESI ZA UDANGANYIFU ZA KCSE KIBINAFSI SIO KITAASISI

Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amethibitisha kuwa visa vyote vya udanganyifu katika mitihani inayoendelea ya Cheti cha Elimu ya Sekondari ya Kenya (KCSE) havitaathiri taasisi za masomo ambapo matukio hayo yatabainika. Akizungumza wakati wa kusimamia usambazaji wa karatasi za mitihani katika ofisi ya makao makuu ya Kaunti Ndogo ya Lang’ata, Ogamba amesema Wizara itashughulikia […]

NETO AOKOA SARE YA CHELSEA HUKU JITIHADA ZA KUWANIA TAJI LA ARSENAL ZIKIPATA PIGO JIPYA

Pedro Neto aliipiga Arsenal pigo jipya katika mbio zao za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza huku winga huyo wa Chelsea akifunga bao zuri na kuokoa sare ya 1-1 katika debi ya London jana Jumapili. Timu ya Mikel Arteta ilikuwa imepata uongozi kupitia bao la Gabriel Martinelli katika kipindi cha pili kwenye uwanja wa Stamford […]