AJALI KAKAMEGA: FAMILIA YAOMBOLEZA JAMAA 2

Familia moja katika eneo la Sabatia kaunti ya Vihiga inaomboleza kifo cha jamaa zao wawili walioangamia kwenye ajali hapo jana jioni katika eneo la Iguhu, idadi ya watu waliofariki hadi sasa ikiwa 10. Kwa mujibu wa familia hiyo, jamaa zao walikuwa safarini kutoka kwenye sherehe ya kifamilia katika eneo la Soy, wawili wakiangamia papo hapo […]

KENHA YATANGAZA KUFUNGWA KWA MZUNGUKO WA BARABARA YA WAIYAKI WAY, SOUTHERN BYPASS

Shughuli za usafiri zinatarajiwa kutatizika kwenye mzunguko wa Waiyaki way, southern Bypass na ule wa Western Bypass. Hii ni baada ya mamlaka ya kusimamia barabara kuu nchini KENHA kutangaza kufungwa kwa barabara hiyo eneo la Gitaru kwanzia tarehe 19 mwezi huu wa novemba hadi tarehe 19 mwezi decemba ili kupisha shughuli za ukarabati. Mamlaka ya […]

MSHUKIWA MKUU WA WIZI WA MTIHANI WA KCSE AKAMATWA HUKO NAKURU

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imemkamata mwanamume anayedaiwa kuwa mmoja wa wahalifu wanaotafutwa sana nchini Kenya kwa kuhusika na udanganyifu wa mtihani wa KCSE wa 2024 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo. Kulingana na dci Collins Kipchumba Kemboi mwenye umri wa miaka 23 anashirikiana na Dorothy Jerop Kiprono kuendesha mifumo ya uvujaji wa mitihani […]

PENALTY YA WEST HAM HAIKUSTAHILI

Mkuu wa waamuzi Howard Webb anasema West Ham haikupaswa kupewa penalti wakati wa mchezo wa mwisho wa Erik ten Hag akiwa mkufunzi wa Manchester United tarehe 27 Oktoba. The Hammers walipewa uamuzi huo kwa pendekezo la mwamuzi msaidizi wa video Michael Oliver kufuatia Matthijs De Ligt kumpinga Danny Ings. David Coote, mwamuzi wa uwanjani, alipunga […]

KOCHA WA KIBERA STARLETS APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa Kibera Starlets Ramadhan Vijago ana imani na uthabiti wa timu yake inapojiandaa kukabiliana na Kisumu All-Starlets Jumapili, licha ya majeraha kuathiri wachezaji muhimu. Timu ya Vijago imeanza vyema msimu wa Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF, ikiwa kileleni kwa alama 10 kutoka kwa mechi tano, ikijumuisha ushindi tatu, sare moja na kupoteza […]

NYOTA YA MOMBASA STARS YAZIDI KUANGAZA

Mombasa Stars ilishinda mechi yake ya pili ya msimu wa 2024-25 National Super League (NSL) Jumatano jioni baada ya kulaza Dimba Patriots 1-0 uwanjani Serani Sports Ground, Kaunti ya Mombasa. Rodgers Okumu alifunga bao la pekee dakika ya kumi, akimpita kipa wa Dimba Patriots baada ya kuunganisha krosi ya Kevin Washe kutoka upande wa kushoto. […]

CHEPNGETICH ATUZWA MWANASPOTI BORA

Ruth Chepngetich aliyevunja rekodi ya mbio za chicago ametajwa kuwa Mwanaspoti Bora wa wanahabari sjak wa mwezi wa Oktoba 2024 kufuatia ushujaa wake katika mbio za 46 za Chicago Marathon nchini Marekani mnamo Oktoba 13, ambapo alikimbia 2:09:56 na kuvunja moja- rekodi ya mwaka (2:11:53) iliyoshikiliwa na Ethiopia Tigst Assefa, kwa karibu dakika mbili. Chepngetich, […]

NAIBU GAVANA WA KAUNTI YA UASIN GISHU KUAPISHWA LEO

Naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Evans Kapkea anatarajiwa kuapishwa hii leo mjini Eldoret. Kapkea, mwenye umri wa miaka 34, na ambaye alikuwa Mbunge wa wadi ya Tembelio aliteuliwa na Gavana Jonathan Bii baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa naibu gavana wa kaunti hiyo John Barorot. Imetayarishwa na Janice Marete

MAUAJI KWARE: WANAHARAKATI WAIKOSOA SERIKALI

Huku visa vya mauaji dhidi ya wanawake vikiendelea kuongezeka nchini na serikali kushinikizwa kuwajibika, wanaharakati wameikosoa serikali kuhusiana na jinsi imeshughulikia mauaji ya wanawake ambao miili yao iliopolewa kutoka timbo ya Kware mwezi Julai jijini Nairobi. Katika kikao na wanahabari, wanaharakati wameikosoa serikali kwa madai ya kushindwa kuwatambua waathiriwa na familia zao, wakihusisha hatua hiyo […]

BALOZI WHITMAN AJIUZULU

Balozi wa Marekani humu nchini Meg Whitman amejiuzulu, baada ya kuhudumu katika wadhifa huo tangu mwaka 2022. Katika ujumbe wake, Whitman ambaye amekuwa akishinikizwa na vijana wa kizazi cha Gen Z kuondoka, amesema kuwa amewasilisha uamuzi wake kwa Rais wa Marekani anayeondoka Joe Bidden. Uamuzi wake wa kujiuzulu umejiri takribani wiki moja baada ya ushindi […]