ODINGA AWAKOSOA WABUNGE KUHUSU MASAIBU YA KAUNTI

Huku kukishuhudiwa mtafaruku baina ya bunge la kitaifa na lile la seneti kuhusu mgao wa serikali za kaunti ambao umelemaza utoaji huduma mashinani, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga amelishutumu bunge la kitaifa kutokana na mahangaiko hayo. Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Odinga amesema kupunguzwa kwa mgao huo kutoka shilingi bilioni 400 hadi bilioni […]

JE MWANGA WA MWANGAZA UTAZIMWA?

Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza natarajiwa kujua hatima yake ya kuendelea kuhudumu kama gavana wa kaunti ya meru hii leo. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa iwapo italiondoa agizo linalozuia kuondolewa mamlakani kwa gavana wa Mwangaza au la. Uamuizi huo vile vile utaamua iwapo gavana mwan gaza ataendelea kuhudumu kiama gavana wa kaunti […]

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA MLIPUKO WA GESI KATIKA KAUNTI YA HOMABAY

Mwanaume wa makamo amefariki na mwingine kujeruhiwa katika mlipuko wa gesi uliotokea Oyugis, Rachuonyo Kusini, Kaunti ya Homa Bay. Mwanaume huyo, ambaye bado hajafahamika, amefariki papo hapo baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Chifu wa Oyugis, Emily Owuor, amesema mwathiriwa huyo alikuwa amesimama takriban mita 20 kutoka eneo la mlipuko alipogongwa na vipande vya […]

NTSA YAWAONYA WAMILIKI WA MAGARI YASIYOFAA BARABARABA DHIDI YA KUYATOA BARABARANI

Mamlaka ya usalama barabara NTSA iewaonya wale wanaopanga kutoa magai yao ya zamani barabarani kwa lengo la kupata pesa msimu huu wa krismasi. Mkuu wa usalama barabarani Samuel Musumba amesisitiza kuwa hakuna magari yasiyofaa kuwa barabarani ambayo yataruhusiwa kuwa barabartani kwa ajili ya kulinda usalama wa wakenya wanaosafiriMusumba aidha ameeleza kuwa mamlaka hiyo itaimarisha utendakazi […]

SENETI YACHUNGUZA NJAMA KWENYE MKATABA WA MATIBABU WA BILIONI 6.3 KWA POLISI

Seneti imeanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa njama kati ya Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) na kampuni za bima binafsi kuhusiana na mkataba wa matibabu wa shilingi bilioni 6.3 na Huduma ya Polisi ya Taifa (NPS). Uchunguzi huu unafuatia ripoti za ucheleweshaji au kukataliwa kwa fidia kwa maafisa wa polisi walioumia wakiwa kazini, kama inavyobainishwa […]

HOFU YA KUSITISHA SHEREHE ZA TAMADUNI YATANDA MIONGONI MWA VIJANA KAUNTI YA KAKAMEGA

Sherehe za michezo ya tamaduni ambazo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka katika kaunti ya Kakamega zimeibua hisia kinzani huku baadhi ya wakazi wakisema hazitafanyika. Vijana wanaoshiriki michezo ya sanaa wa kaunti hiyo wametoa wito kwa kaunti hiyo kupitia wizara ya michezo kuweka wazi tetesi zinazonezwa kwamba tamasha ya mashindano ya tamaduni inayoandaliwa kila mwaka haitakuwapo […]

WAIGURU AAHIDI KUIMARISHA BIASHARA KIRINYAGA

Shughuli za biashara zimeratibiwa kurahisishwa katika kaunti ya Kirinyaga kufuatia mpango wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Kagio kwa ushirikiano wa serikali kuu na ile ya kaunti hiyo ili kupunguza msongamano. Akizungumza katika mkutano eneo hilo, gavana Anne Waiguru amesema kuwa masoko 11 zaidi yatajengwa chini ya mpango wa kichecheo cha uchumi […]

UASIN GISHU YAPATA NAIBU GAVANA MPYA

Wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu wanatarajia kuimarika kwa utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo baada ya kupata naibu gavana mpya kufuatia kuapishwa kwa Evans Kapkea kujaza pengo lililoachwa na John Barorot. Kapkea ambaye amekuwa akihudumu kama mwakilishi wadi ya Tembelio, aliteuliwa na gavana Jonathan Bii mwezi Agosti baada ya Baroro kujiuzulu. Akizungumza baada ya […]

WAKULIMA MACHAKOS WAPATA ‘MBEGU ZA MATUMAINI’

Wakulima katika kaunti ya Machakos wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuzindua mpango wa kuwapa mbegu za kupanda msimu huu wa mvua ya vuli. Akizindua mpango huo katika eneo la Matuu, gavana Wavinya Ndeti amesema kuwa wanalenga wakazi walio na mapato ya chini kwa lengo la kuimarisha utoshelevu wa chakula. Mbegu za mahindi, […]

MWEZI WA WATOTO: WATOTO NAROK WAPATA AFUENI

Ni afueni kwa familia zilizo na kesi mahakamani zinazohusu Watoto katika kaunti ya Narok baada ya mahakama ya Narok kuzindua rasmi mwezi wa huduma na haki kwa Watoto ili kushughulikia kesi zao kama suala la dharura. Hakimu mkuu wa mahakama hiyo Hezron Nyamberi, amehakikishia umma kwamba wahudumu wote wa mahakama wako tayari kushughulikia kesi hizo […]