RUTO AKUTANA NA VIONGOZI WA MAGHARIBI

Rais William Ruto amefanya kikao na viongozi wa eneo la Magharibi mwa nchi akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, mawaziri Wycliffe Oparanya na Debora Mulongo, Pamoja na magavana wa eneo hilo isipokuwa Wilber Otichillo wa Vihiga, maseneta na wabunge. Kulingana na taarifa kutoka Ikulu, mkutano huo umelenga kujadili […]

RAIS RUTO AMFUTA MUTURI KAZI, MAGEUZI ZAIDI

Rais William Ruto amemfuta kazi waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi, na kumteua mbunge wa Mbeere North Geoffrey Ruku kuchukua nafasi ya Muturi, ambaye amekuwa akikosa kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri kufuatia msimamo wake kuhusu utekaji nyara na mauaji ya kiholela nchini. Katika mageuzi Zaidi, Aden Duale amehamishwa kutoka wizara ya mazingira hadi […]

KQ YAPATA FAIDA YA DOLA MILIONI 41.7

Licha ya changamoto katika sekta ya usafiri wa anga, Kenya Airways (KQ) imepata faida ya dola milioni 41.7 katika mwaka wa fedha 2024, ikitoka kwenye hasara ya dola milioni 174.6 mwaka 2023. Mkurugenzi Mkuu, Allan Kilavuka, amesema mafanikio haya yanaashiria mabadiliko makubwa, huku shirika likiendelea kuwavutia wawekezaji wa kimkakati. Mwenyekiti wa KQ, Michael Joseph, amesema […]

MWANAFUNZI AFARIKI BAADA YA KUPIGWA NA WAJOMBA

Polisi Nyamira wanachunguza kifo cha Brian Mogaka (22), aliyefariki baada ya kupigwa viboko na mjomba zake katika kijiji cha Nyankono, North Mugirango. Mogaka, aliyesimamishwa masomo kwa madai ya matumizi ya mihadarati, anadaiwa kushambuliwa baada ya mamake kuwaomba ndugu zake kumwadhibu. Polisi wa Ekerenyo wamepeleka mwili wake katika hifadhi ya maiti kwa uchunguzi zaidi. Imetayarishwa na Janice Marete

ARGENTINA YAFUZU KWA KOMBE LA DUNIA

Argentina ilisherehekea kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 kwa kuwalaza 4-1 mahasimu wao Brazil mjini Buenos Aires siku ya Jumanne. Julian Alvarez, Enzo Fernandez, Alexis Mac Allister na Giuliano Simeone waliwapatia ushindi mnono mabingwa hao wa dunia, ambao walikuwa wamehakikishiwa kufuzu Kombe la Dunia baada ya Bolivia kutoka sare ya 0-0 na Uruguay mapema […]

TUMEWAPANGIA POLICE FC ASEMA PAMZO

Kocha mkuu wa Posta Rangers FC Sammy ‘Pamzo’ Omollo anasema wana mpango dhidi ya vinara wa ligi Police FC wakati pande hizo mbili zitavuka panga katika mechi ya ligi Jumapili. Kulingana na ‘Pamzo’, wamejiandaa vilivyo kupindua kipigo cha mkondo wa kwanza cha mabao 3-2 kutoka kwa washambuliaji hao; jambo ambalo linaweza kuhatarisha uwezekano wa mchezaji […]

3K FC WANA MATUMAINI KUFANYA VYEMA WIKENDI HII

Timu ya Taifa ya Ligi Kuu ya 3K FC ina uhakika kabla ya mchuano muhimu wa wikendi dhidi ya Luanda Villa huku kukiwa na mvutano wa ligi ya daraja la juu msimu ujao. Kocha msaidizi wa klabu hiyo Moses Munene alielezea matumaini yake kuhusu hali na umakini wa timu hiyo kwa sasa. Kwa sasa wanazidi […]

TUTAHAMAISHA MICHEZO HADI KASARANI

Rais wa FKF Hussein Mohammed anasema uwezekano wa kuhamisha michezo ijayo ya Harambee Stars kutoka uwanja wa Nyayo hadi uwanja wa Kasarani. Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kushughulikia masuala ya kiusalama na  yaliyotokana na mechi ya Jumapili ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Gabon, alisisitiza haja ya kusogeza michezo hiyo […]

WASIWASI WA MATUMIZI YA BILIONI 1.34 BILA USHAHIDI WA MIRADI

Wasiwasi umeibuliwa kuhusu matumizi ya Shilingi bilioni 1.34 na Idara ya Utumishi wa Umma katika nusu ya kwanza ya mwaka wa kifedha wa 2024/25 bila ushahidi wa miradi iliyokamilika. Mdhibiti wa Bajeti (CoB), Margaret Nyakang’o, anasema licha ya mgao wa kufadhili majengo ya serikali, njia za watembea kwa miguu, na udhibiti wa ujenzi, hakuna matokeo […]

MIKOPO GHALI: CBK KUJIBU MBELE YA BUNGE

Wafanyabiashara bado wanakabiliwa na gharama kubwa ya mikopo licha ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) kupunguza kiwango cha riba. Kutokana na hali hiyo, Gavana wa CBK, Kamau Thugge, anatarajiwa kufika mbele ya Bunge la Kitaifa leo kueleza sababu za benki za biashara kutozingatia hatua hiyo. Wakati huo huo, Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa, […]