KENYA KUANGAZIA UPYA MARUFUKU YA MITUMBA

Serikali ya Kenya inawazia kupiga marufuku uagizaji wa mitumba ili kufufua sekta ya ushonaji nchini, Wizara ya Biashara ikisema kuwa mitumba imedhoofisha viwanda vya nguo vya ndani. Kati ya mwaka 2019 hadi 2023, Kenya iliagiza mitumba ya thamani ya KSh 95.2 bilioni, huku kiwango kikiongezeka kwa asilimia 11.5 mwaka 2023 pekee. Hata hivyo, marufuku hiyo […]

MSAMAHA WA USHURU WA KRA WAFIKIA KSH 158 BILIONI

Mamlaka ya ukusanyaji ushuru Nchini, KRA, imetangaza kuwa zaidi ya walipa ushuru milioni 2.9 wamefaidika na Mpango wa Msamaha wa Ushuru ambao ulianza Disemba 27, 2024. Kwa mujibu wa Kamishna wa Ushuru, Humphrey Simiyu, tangu uzinduzi wa mpango huo, KRA imekusanya jumla ya shilingi bilioni 10.9 kama malipo ya kodi ya msingi kutoka kwa walipa […]

YIEMBE AITWA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA LA KLABU 2025

Msaidizi wa refa wa FIFA, Stephen Yiembe, atahudumu kandokando ya uwanja kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025, akiungana na kundi la maafisa wa mechi 117 walioteuliwa na shirikisho hilo la soka duniani kwa ajili ya mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 14 Juni hadi 13 Julai 2025 nchini Marekani. Yiembe ni […]

MARUFUKU YA USIKU YATEKELEZWA KAMIU BAADA YA MIIILI KUPATIKANA

Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha mauaji ya vijana wawili katika kijiji cha Kamiu kaunti ya Embu baada ya miili yao kupatikana barabarani. Mamlaka za eneo hilo zimeweka marufuku ya kutotoka nje usiku kuanzia saa tatu hadi saa kumi na mbili asubuhi huku chifu Sammy Njagi akionya kwamba yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa kama mshukiwa wa […]

OILERS WAPONGEZWA LICHA YA KUPOTEZA FAINALI KWA KABRAS

Kocha mkuu wa timu ya raga ya Shule ya Upili ya Kakamega ameisifu Menengai Oilers kwa juhudi zao licha ya kupoteza kwa alama 27–26 dhidi ya Kabras RFC katika fainali ya Kenya Cup. Kocha huyo, Wamanga, alisema ilikuwa mechi ngumu kwa mabingwa watetezi. Aliweka wazi kuwa anatarajia pambano kali zaidi katika fainali ya Kombe la […]

OKWARO ALENGA KUNG’AA AFCON NA KUINGIA KIKOSI CHA CHAN

Beki wa timu ya taifa ya Kenya chini ya miaka 20, Manzur Okwaro, analenga kung’aa kwenye mashindano ya AFCON kwa vijana na kupata nafasi katika kikosi cha CHAN. Okwaro mwenye umri wa miaka 19, alicheza mechi yake ya kwanza kwa timu ya wakubwa dhidi ya Gabon baada ya kumvutia kocha Benni McCarthy. Mchezaji huyo wa […]

GACHAGUA, NATEMBEYA WALILIA SERIKALI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, wamedai kwamba maisha yao yamo hatarini, wakisema serikali inawaandamana kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakiikosoa. Katika taarifa tofauti, Gachagua amemwandikia waraka Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja akiorodhesha matukio 6 anayosema yanatishia usalama wake, ikiwemo madai ya kuandamwa na idara ya ujasusi, na […]

UJENZI WA AFUENI WEBUYE

Huduma za matibabu katika kaunti ya Bungoma zinatarajiwa kuimarika kutokana na ujenzi unaoendelea wa jumba la ghorofa mbili katika hospitali ya rufaa ya kaunti ndogo ya Webuye itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa unaoshuhudiwa kwa sasa eneo hilo. Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka amekiri kuwepo kwa changamoto za msongamano wa wagonjwa, akidokeza kuwa kuna mikakati ya kupandisha cheo hospitali hiyo […]

WAMATANGI, WENGINE 8 MASHAKANI

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi na maafisa wengine wakuu wa kaunti hiyo akiwemo katibu Peter Njoroge wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka punde baada ya uchunguzi wa tume ya maadili na kukabili ufisadi kuhusiana na Sakata ya shilingi bilioni 1.5 kukamilika. Wamatangi amekamatwa mapema leo na kuhojiwa katika makao makuu ya EACC jijini Nairobi, tume hiyo ikisema imenasa […]

BUNGE LA KENYA LAPENDEKEZA KUBADILISHWA KWA SEHEMU YA 19 YA SHERIA YA AJIRA

Wabunge wamemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuifuta au kuirekebisha Sehemu ya 19 ya Sheria ya Ajira ya mwaka 2007, ambayo inazuia makato ya mshahara kuwa zaidi ya theluthi mbili ya malipo ya msingi ya mfanyakazi. Pendekezo hili linakuja kutokana na kuongezeka kwa makato ya kisheria kama vile Ada ya Makazi, Mfuko wa Bima ya Afya […]