SENETA CHERARGEI ATAKA KUONDOLEWA AFISINI MURKOMEN

Seneta wa Nandi Samson Cherargei anataka kuondolewa afisini kwa waziri wa usalama Kipchumba Murkomen akidai kuwa amefeli katika majukumu yake. Cherargei badala yake anapendekeza nafasi hiyo kurejeshewa naibu wa rais Kithure Kindiki anayesema alipohudumu katika wizara hiyo visa vya uhalifu vilipungua. Imetayarishwa na Maureen Amakhobe

OCS AKANA POLISI KUWAUA WAANDAMANAJI

Polisi hawakuhusika katika mauaji ya waandamanaji wakati wa vurugu zilizotokana na mswada tata wa fedha mwaka jana. Ndio msimamo wa aliyekuwa ocs wa kituo cha polisi cha Kamukunji Robert Mugo anayedai kuwa wale waliokuwa na kundi la maafisa waliowatuma ni wahalifu na wala hawakuwa waandamanaji. Mugo ambaye sasa anasimamia kituo cha polisi cha Githurai amesema […]

IG KANJA AFICHUA MLALAMISHI KWENYE KIFO CHA ALBERT OJWANG

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amethibitisha kuwa mwanablogu Albert Ojwang’ aliyefariki katika kituo cha polisi cha Central Jijini Nairobi alikuwa akiechunguzwa kwa madai ya kumchafulia jina naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kwenye mitandao ya kijamii. Katika taarifa kwa wanahabari, Kanja amesema naibu wake alikuwa amewasilisha malalamishi rasmi ya kuchafuliwa jina na mwnablogu […]

GACHAGUA ATAKA DIG LANGAT ATIMULIWE

Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ameshinikiza kufutwa kazi kwa naibu inspekta mkuu wa polisi wa kitengo cha polisi wa kawaida Eliud Langat kutokana na kifo cha mwanablogu Albert Ojwang’ Gachagua akisema Langat anafaa kuwajibishwa na wala si maafisa wa polisi waliosimamishwa kazi. Kupitia taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Gachagua amesema Langat anafaa kuwajibishwa […]

UKAME WA MCCARTHY WAIBUA HOFU

Mkufunzi wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Benni McCarthy ataendelea kusubiri ushindi tangu achukue hatamu za uongozi wa kikosi hicho, baada ya timu hiyo kutoka sare ya kutofungana dhidi ya Chad kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa nchini Moroko Jumamosi iliyopita. Stars ambao wanashikilia nafasi ya 111 kwenye jedwali la FIFA, walianza mechi hiyo […]

KIBERA SOCCER WOMEN, VIHIGA QUEENS FAINALI ZA FKF CUP

Warembo wa Kibera Soccer Women watamenyana na Vihiga Queens kwenye fainali za makala ya 4 ya kombe la FKF CUP mwaka huu kufuatia ushindi wao hapo jana. Kibera Soccer Women wametinga fainali hizo baada ya kuwatandika mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Police Bullets mabao 2:0 hapo jana, mabao hayo yakifungwa na Maximilla Munika na […]

URENO WATAWAZWA MABINGWA UEFA NATIONS LEAGUE

Cristiano Ronaldo aliiongoza Ureno kuwacharaza majirani zao Uhispania kwenye fainali za kipute cha UEFA Nations League jana usiku, na kuipa ureno taji la pili la fainali za mashindano hayo tangu mwaka wa 2019. Ronaldo alilazimisha sare ya mabao 2 kunako dakika ya 61 baada ya Uhispania kuchukua uongozi kwenye kipindi cha kwanza kupitia mabao ya […]

AMOLLO ATISHIA MSUMARI WA MWISHO KWA GACHGUA

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ametishia kuwasilisha mswada bungeni kwa lengo la kumpiga marufuku aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua dhidi ya kuwania afisi yoyote ya umma. Otiende ambaye anamtuhumu Gachagua kwa madai ya kueneza siasa za migawanyiko, amesema kuwa Gachagua hajapata funzo lolote kutokana na kutimuliwa kwake kutoka afisini mwaka jana. Ametishia kuwa iwapo Gachagua […]

MWUGUZI MAKUENI ACHUNGUZWA KWA ‘KULIPIZA KISASI’

Serikali ya kaunti ya Makueni inachunguza tukio ambapo mwuguzi mmoja anadaiwa kudinda kumhudumia mwanamke aliyetaka kujifungua katika kituo cha matibabu cha Mavinye Little Dispensary na kumlazimu mwanamke huyo kusaka huduma za mkunga wa kienyeji licha ya serikali kuendeleza kampeni za kuwataka akina mama wajifungulie hospitalini. Kulingana na Tabitha Mutuku ambaye ni mama mkwe wa mwanamke […]

RAIS RUTO AENDELEA KUJITETEA

Mradi wa nyumba za bei nafuu utawapandisha hadhi wakenya wanaoishi katika mitaa duni na kuwapeleka katika nyumba za kisasa. Ndio kauli ya Rais William Ruto ambaye ameendelea kutetea mradi huo licha ya ukosoaji kwamba mradi huo unatumiwa kufuja fedha. Aidha, Rais ametetea ubomoaji unaoendelezwa na serikali ya kaunti ya Nairobi dhidi ya wanaokwepa kulipa ushuru. […]