IDADI YA WAFANYAKAZI VYUONI KUPUNGUZWA

Mamia ya wafanyakazi katika vyuo vikuu vya umma nchini wanakabiliwa na hatari ya kuachwa bila ajira baada ya serikali kutangaza kwamba haina uwezo wa kufadhili elimu katika vyuo hivyo. Waziri wa fedha John Mbadi ametangaza kwamba serikali imeweka mpango wa kuvinusuru vyuo hivyo, ikiwemo kufunga baadhi ya mabewa na kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kudhibiti […]

MASOMO YA WANAFUNZI NJIA PANDA

Hatma ya masomo ya wanafunzi katika shule za msingi na upili sasa iko kwenye njia panda, kufuatia tangazo la serikali kwamba haiwezi kufadhili kikamilifu elimu ya bure katika shule za msingi na upili za umma kutokana na uhaba wa fedha. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya elimu katika bunge la kitaifa, waziri wa fedha John […]

KEMSA YATAMBUA KAUNTI 11 BORA

Mamlaka ya KEMSA imetambua kaunti 11 ambazo zimeipa sekta ya afya kipau mbele katika bajeti zake. Kaunti hizi ni pamoja na Machakos,Kitui,Elgeyo Matakwet,Nyeri,Meru,Narok,Kisumu Busia Mandera na Turkana. Afisa mkuu mtendaji wa KEMSA Dkt Waqo Ejersa anasema kaunti hizo zimetenga fedha za kutosha kwa ununuzi wa dawa na vifaa vingine vya matibabu kutoa malipo yao kwa […]

POLISI WALIOKABILI WAANDAMANAJI HAWAKUPEWA CHAKULA,YASEMA IPOA

Polisi waliotumwa kukabili waandamanaji wakati wa maandamano ya Juni 25 na Julai 7 hawakupewa chakula na maji ya kutosha. Mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi Ipoa inasema maafisa hao waliotumwa kutoa ulinzi kwa majengo na taasisi za serikali maslahi yao hayakuangaziwa ipasavyo. Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja ametakiwa kuhakikisha bajeti ya kutosha imewekwa kushughulikia […]

KALOMBOTOLE KUZUILIWA HOSPITALINI MBAGATHI

Mshukiwa wa mauaji ya wagonjwa 2 katika hospitali ya Kenyatta Kennedy Kalombotole atazuiliwa katika hospitali ya Mbagathi. Ni uamuzi uliotolewa na hakimu wa mahakama ya Kibera Daisy Mutai anayesema mshukiwa hawezi kuzuiliwa katika kituo cha polisi kutokana na matatizo ya akili aliyo nayo. Mutai ameelezea haja ya Kennedy kuwa chini ya uangalizi wa wahudumu wa […]

BUNGOMA HIGH WATOA ONYO KWA WAPINZANI WAO

Huku michezo ya kitaifa ya shule za upili ikikaribia, Shule ya Upili ya Wavulana ya Bungoma imefyatua risasi ya onyo kwa wapinzani wao kabla ya mashindano ya raga ya wachezaji saba saba yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo katika Kaunti ya Kakamega. kocha mkuu wa timu hiyo, Titus Wangila, amesema kwa kujiamini kwamba timu yake iko tayari […]

RUTO AZINDUA DHAMANA YA TAIFA

Rais William Ruto amezindua dhamana ya taifa katika soko la hisa la Nairobi ili kufadhili ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Talanta unaojengwa na kampuni ya Kichina. Rais Ruto amesema kuzinduliwa kwa dhamana hiyo kutakusanya zaidi ya shilingi bilioni 44 za Kenya (sawa ana dola za Kimarekani milioni 340.6), ambayo ni mafanikio makubwa yanayothibitisha imani […]

UHAMISHO WA LIGI KUU YA UINGEREZA

Javi Guerra amekataa ofa ya kuongeza mkataba wake na Valencia, huku Manchester United ikisemekana kumfuatilia kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22. Winga wa Manchester City na England Jack Grealish, 29, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa upande wa kushoto wanaofikiriwa na Napoli Real Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 100 […]

BANDARI FC YAIMARISHA KIKOSI CHAKE

Bandari FC, timu pekee ya Coastal katika ligi ya daraja la juu imeanza kuimarisha kikosi chao kabla ya kampeni mpya, baada ya kumaliza katika nafasi ya nane isiyoridhisha msimu wa 2024/2025. Timu hiyo inayonolewa na kocha Ken Odhiambo ilikusanya pointi 44 kutoka kwa mechi 34 katika hali ambayo ilikuwa ya aibu kwa timu hiyo iliyofadhiliwa […]

KENYA IKO TAYARI KWA CHAN ASEMA MVUYRA

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Michezo Salim Mvurya Jumatano aliambia Seneti kwamba Kenya inapiga hatua kubwa katika kuandaa viwanja na vifaa vya mazoezi kabla ya kuandaa Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka wa 2025 na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mnamo 2027. Akiwa mbele ya kikao cha Seneti, Mvurya alisema Uwanja wa […]