WANARIADHA WAWILI WAPIGWA MARUFUKU

Kitengo cha Uadilifu wa Riadha (AIU) kimechukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanariadha wawili wa Kenya kwa ukiukaji wa dawa za kusisimua misuli, na hivyo kuzidisha kuangaziwa kwa vita vya Kenya dhidi ya dawa za kuongeza nguvu katika riadha. Bingwa wa taifa na mshindi wa medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 za Afrika, […]

GYOKERES ANYIMWA NDOTO YA JEZI NAMBARI TISA

Hatimaye Viktor Gyokeres yuko mbioni kujiunga na Arsenal baada ya The Gunners kufanikiwa katika mazungumzo na Sporting Lisbon, na kukubali kulipa jumla ya pauni milioni 63.7 baada ya kuhangaika kuhusu nyongeza . Ata hivyo Arsenal haitaweza kumpa Viktor Gyokeres jezi ya ndoto yake ya nambari tisa wakati mshambuliaji huyo wa Uswidi atakapokamilisha uhamisho wake wa […]

ODERA APIGIA UPATO MZUNGUKO WA RAGA

Mkurugenzi wa Chama cha Raga cha Kenya (KRU) Paul Odera amethibitisha umuhimu wa Mzunguko wa Kitaifa wa Saba katika kuunda mustakabali wa timu za taifa za saba, Shujaa na Simba. Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa msimu wa mzunguko wa Kitaifa wa 7s wa 2025 katika Uwanja wa RFUEA, Odera alibainisha kuwa mashindano hayo ya […]

MCCARTHY YUKO IMARA NA STARS

Kocha mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy Wednesday alisema anasimamia timu ya taifa kwa uthabiti, huku akipuuzilia mbali ripoti zinazoibuka zinazodokeza kuwa kuna uingiliaji wa nje katika kutaja kikosi kitakachofanya kazi wakati wa mashindano ya CHAN mwezi ujao. Akizungumza katika mkutano na wanahabari katika uwanja wa Nyayo, kocha huyo wa Afrika Kusini alithibitisha kuwa hakuna […]

MATIBABU KUTATIZIKA KIAMBU KUANZIA LEO

Huduma za matibabu katika kaunti ya Kiambu zimetarajiwa kutatizika kuanzia hii leo baada ya muungano wa madaktari KMPDU kutangaza kusitisha huduma zote ili kufanya maandamano ya kuishinikiza serikali ya kaunti hiyo kuangazia malalamishi yao. Kupitia taarifa, katibu mkuu wa muungano huo Dakta Davji Atellah amesema wahudumu wa afya watakongamana nje ya hospitali ya level V […]

GACHAGUA: RUTO HAFAMU CHANGAMOTO ZA NCHI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amemkosoa Rais William Ruto kwa kuzilaumu taasisi mbali mbali na kuzihusisha na maandamano yanayoongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z. Akizungumza katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani, Gachagua amesisitiza haja ya Rais William Ruto kuondolewa mamlakani ifikapo mwaka wa 2027. Gachagua amedai kuwa Rais Ruto hana ufahamu kuhusu changamoto […]

UJUMBE WA RUTO KWA WAKOSOAJI

Rais William Ruto amewataka wanaomkosoa kuweka wazi mpango wao wa kuboresha maisha ya wakenya badala ya kuendeleza ukosoaji, huku akiwapuzilia mbali wanaosisitiza kuwa hatachaguliwa kwa muhula wa pili. Akizungumza jijini Nairobi, Rais Ruto ametaka kupewa muda wa kufanya kazi yake, akisema wakati wa kuondoka mamlakani ukiwadia atafanya hivyo. Aidha, amemshutumu aliyekuwa jaji mkuu David Maraga […]

SHULE KULAZIMIKA KUFUNGA MAPEMA

Masomo katika shule za umma nchini yatalazimika kukatizwa mapema muhula huu kutoka na uhaba wa fedha, wakuu wa shule hizo wakisema hawana uwezo wa kuziendesha shule baada ya serikali kukosa kutuma mgao wa masomo. Changamoto za kifedha shuleni zimesababishwa na mgao kupunguzwa, kucheleweshwa au hata kutotumwa kwa shule ili kufanikisha shughuli za kila siku. Katika […]

WANDAYI AFICHAU SABABU YA BEI YA MAFUTA KUPANDA

Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amefichua kuwa hakukuwa na fedha katika hazina ya Ushuru wa Maendeleo ya Petroli za kutumika kuwakinga wakenya dhidi ya kupanda kwa bei za mafuta mwezi huu wa Julai. Wandayi amesema hayo alipofika mbele ya Kamati ya nishati katika bunge la Kitaifa, ambapo ameeleza kuwa serikali ilihitaji bilioni 2.5 kutoa ruzuku […]

FKF KUSHUGHULIKIA MISHAHARA YA WAAMUZI

SHIRIKISHO la Soka la Kenya (FKF) limejitolea kushughulikia masuala ya muda mrefu yanayohusu uchezeshaji wa mechi, likilenga sana kuhakikisha waamuzi wanalipwa kwa wakati na kutayarishwa ili kutoa uchezaji wa hali ya juu. Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaidhinisha waamuzi wapya 52 kutoka mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa FKF na Mjumbe wa […]