THE GAMBIA WATEUA KIKOSI

Timu ya taifa ya wanawake ya Gambia imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaomenyana na Harambee Starlets Ijumaa wiki hii jijini Nairobi katika mkondo wa kwanza wa awamu ya mwisho ya kufuzu fainali za ubingwa wa bara Afrika kwa wanawake WAFCON. Starlets watakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza ugani Nyayo, kabla ya marudiano siku 4 baadaye […]

MWENYEJI WA FAINALI ZA RAGA YA WANAWAKE ATANGAZWA

Jiji la Nairobi litakuwa mwenyeji wa ubingwa wa mwaka huu wa raga ya wanawake barani Afrika kitakachoandaliwa kuanzia tarehe 15 hadi 16 mwezi ujao katika uga wa RFUEA. Tayari timu zitakazoshiriki zimewekwa kwenye makundi 4 kabla ya kipute hicho ambacho kitaandaliwa nchini kwa mara ya pili baada ya Kenya kuwa mwenyeji wa Makala ya 2014. […]

RUTO: NITAREJELEA ZIARA YANGU UKAMBANI

Rais William Ruto ametoa wito kwa wakazi wa eneo la Ukambani kujiepusha na siasa za migawanyiko, akiwahimiza kushirikiana na serikali yake ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo eneo hilo. Rais alikuwa akizungumza hapo jana wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mashujaa, akiahidi kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo maji, barabara na kilimo. Rais ameahidi […]

ODM YAMWITA RUTO AREJEE NYUMBANI 

Rais William Ruto atapeperusha bendera ya chama cha ODM kwenye kinyang’anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu iwapo atakubali kurejea chamani humo. Haya ni kwa mujibu wa naibu kinara wa ODM Simba Arati, ambaye amemtaja Ruto kama mwaasisi wa chama hicho na hivyo ana nafasi yake chamani. Kwenye hotuba yake ya Mashujaa hapo jana, Arati ambaye […]

KCSE KUANZA LEO

Jumla ya watahiniwa elfu 990 wa mtihani wa kitaifa wa kidato cha 4 KCSE wameratibiwa kuanza mtihani huo hii leo na kukamilika tarehe 21 mwezi ujao. Kwa mujibu wa ratiba ya baraza la mitihani ya kitaifa KNEC, mitihani ya Kifaransa, Kijerumani, lugha na ishara inaanza hii leo na kufuatiwa na mitihani ya utendaji yaani practical […]

TANZANIA YAMULIKWA KWA UKIUKAJI

Serikali ya Tanzania imejipata chini ya darubini ya jamii ya kimataifa kuhusu visa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu, shirika la Amnesty International likisema visa hivyo vinaongezeka taifa hilo linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu ambao umewaacha nje viongozi wa upinzani. Licha ya kusifiwa awali kwa kuondoa vikwazo vya mtangulizi wake John Magufuli, Rais wa sasa Samia […]

ODM: ENZI BABA KWA KUTEKELEZA AJENDA ZAKE

Viongozi wa chama cha ODM wamemtaka Rais William Ruto kutekeleza ajenda 10 zilizo kwenye mktaba wa maelewano uliotiwa Saini na Rais na aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga, wakisema ndiyo njia mwafaka ya kumuenzi Odinga. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, naibu mwenyekiti wa ODM Godfrey Osotsi, amesema ajenda hizo zinawakilisha maslahi ya mwananchi […]

MCHANGO WA BIASHARA NDOGO NA KATI  KATIKA UKUAJI WA UCHUMI

Imebainika kuwa Biashara ndogo ndogo na zile za kati, zinahusika pakubwa katika kutoa fursa za ajira  kwa wafanyakazi wengi wa Afrika, jambo ambalo ni muhimu katika kufungua sekta isiyo rasmi ya bara. Idadi ya watu barani Afrika inapoongezeka, benki ziko mbioni kutafuta masoko makubwa zaidi, kwani mara nyingi benki nyingi hupata biashara ili kupanua wigo wao. Kulingana na ripoti ya Mkakati wa Ajira kwa Vijana barani Afrika ya Benki ya Maendeleo […]

MAN UNITED YAZIDISHA MASAIBU YA LIVERPOOL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza EPL Liverpool wamepoteza mechi 4 mfululizo, ikiwa na mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11 baada ya kupokezwa kipigo cha mabao 2:1 nyumbani na Manchester United. United wanaonolewa na Ruben Amorim waliweka kando masaibu yao na kuanguka na miamba hao wa Uingereza, wakishinda mechi 2 za ligi […]

 KIKOSI CHA TAEKWONDO KENYA CHATAJWA

Wanaspoti 16 wakiwemo wanawake 8 na wanaume 8 wametajwa kwenye kikosi cha mwisho kitakachowakilisha Kenya katika mashindano yanayokuja ya ubingwa wa dunia wa Takekwondo kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21, yatakayoandaliwa mwezi Disemba jijini Nairobi. Miongoni mwao ni Williams Odhiambo, mshindi wa nishani ya shaba katika majaribio ya mwaka jana ingawa hakuchaguliwa katika mashindano […]