EPL KUREJEA ARSENAL WAKIPATA PIGO

Ligi ya soka nchini Uingereza inaingia mechi ya 8 wikendi hii huku klabu ya Arsenal ikikadiria majeraha kwa wachezaji wake muhimu. Miongoni mwa wachezaji wanaohifwa kukosa mechi ya Arsenal na Fulham ni Martin Zubimendi na Ben White kutokana na majeraha. Kwenye mazoezi hapo jana, Zubimendi hakuhudhuria huku White akilemewa na kuonekana akipokea matibabu pembeni pa […]

POLICE FC KUCHEZA BILA MASHABIKI, WANAHABARI

Mechi ya raundi ya pili ya kuwania ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika CAF kati ya Police FC ya Kenya na Al-Hilal ya Sudan hii leo imehamishwa kutoka uwanja wa Kasarani hadi ule wa Ulinzi Complex. Kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini FKF, uhamisho huo umetokana na ibada ya kitaifa ya mazishi ya Waziri […]

OWALO ACHUKUA MIKOBA YA ODINGA GOR

Miamba wa soka nchini Gor Mahia wamemteua mkuu wa utendakazi wa serikali kama mlezi wake, na kuchukua mahali pa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Uteuzi wa Owalo umewekwa wazi na mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier, akisema Owalo anaanza majukumu yake mara moja ili kujaza pengo la Odinga aliyeaga dunia. Odinga amekuwa mlezi wa […]

MAGAVANA WAMWOMBOLEZA ODINGA

Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga alikuwa kiongozi mwazi, mtetezi wa ugatuzi, mwanasiasa mwerevu na kigogo aliyepigania haki. Ndio ujumbe wa baraza la magavana likimwomboleza Odinga, ambaye magavana wamemtaja kama baba wa ugatuzi nchini. Magavana wamewahimiza wanasiasa wengine kuiga mfano wake. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KABURI LA ODINGA LAANDALIWA BONDO

Maandalizi ya eneo atakakozikwa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga katika eneo la Bondo kaunti ya Siaya yanaendelea, zikiwa ni siku 2 pekee zimesalia kabla ya mazishi hayo. Shughuli ya uchimbaji kaburi ilianza hapo jana baada ya eneo kutambuliwa na kakake Odinga, Oburu Odinga, ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya kitaifa ya mazishi. […]

POLISI WAIMARISHA DORIA NAIROBI 

Usalama umeimarishwa katika jiji la Nairobi huku matayarisho ya ibada ya kitaifa ya mazishi ya waziri mkuu wa zamani Raila Odinga yakiendelea. Polisi wameshika doria katika majengo ya bunge, uwanja wa michezo wa Nyayo na kwenye barabara mbali mbali ikiwemo Bunyala, Lang’ata na Uhuru Highway. Polisi wameshika doria kuanzia alfajiri, baadhi wakitumia farasi, huku maelfu […]

IBADA YA MAZISHI YA ODINGA KUANZA

Ibada ya kitaifa ya mazishi ya waziri mkuu wa zamani Raila Odinga inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa, ikiratibiwa kudumu kwa muda wa saa 2 pekee kuanzia saa tatu asubuhi katika uwanja wa michezo wa Nyayo. Kwa mujibu wa mwenyekiti mwenza wa kamati ya kitaifa ya mazishi ya Odinga naibu Rais Kithure Kindiki, ibada hiyo […]

MWILI WA ODINGA WAWASILISHWA KASARANI

Maelfu ya waomboleza wamefurika katika uwanja wa michezo ya Kasarani jijini Nairobi tayari kutazama mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Mwili huo tayari umewasili uwanjani humo baada ya zaidi ya saa 5 barabarani, maafisa wa jeshi na wale wa polisi wakiwa na wakati mgumu kuwadhibiti waombolezaji kwenye msafara huo ambao umekuwa na viongozi […]

WAKURUGENZI WAKUU  WAONYA KUHUSU ATHARI KUBWA KUTOKA KWA USHURU WA TRUMP NA KUISHA KWA MUDA WA AGOA

Maafisa wakuu wa sekta ya utalii na uundaji bidhaa nchini Kenya wanatarajia kupata pigo kubwa kutoka kwa ushuru mpya wa kibiashara wa Rais wa Marekani Donald Trump na kumalizika kwa Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika (Agoa). Utafiti wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) unaonyesha kuwa asilimia 64 ya zaidi ya Wakurugenzi 1,000 waliohojiwa wametaja athari mbaya kutoka kwa […]

FIFA YAELEZA MATUMAINI MAREKANI ITAKUWA TAYARI

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limesema kwamba lina matumaini kwamba miji 16 itakayoandaa fainali za kombe la dunia nchini Marekani mwaka ujao itakuwa tayari kuandaa mashindano hayo. Hii ni baada ya kauli ya Rais wa marekani Donald Trump kudokeza kwamba mechi hizo zinaweza kuhamishiwa maeneo mengine kutokana na hofu za kiusalama. Siku ya Jumanne wiki […]