IPOA YATAKIWA KUCHUNGUZA VIFO WAKATI WA MSIBA

Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA imetakiwa kuanzisha uchunguzi mara moja kubaini chanzo cha vifo vya watu kadhaa waliofariki wakati wa kuutazama mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Familia ya Michael Okoth, mkazi wa Kibra mwenye umri wa miaka 23 ambaye mwili wake ulitambuliwa hapo jana, imesema imekuwa ikimsaka mwanao kwa siku […]

WAMATANGI AHUSISHA TAARIFA ZA VIFO NA SIASA

Serikali ya kaunti ya Kiambu imepuzilia mbali taarifa kuhusu vifo vya Watoto katika hospitali za kaunti hiyo kutokana na mgomo wa madaktari, ikizitaja taarifa hizo kuwa zilizochochewa kisiasa. Kulingana na gavana Kimani Wamatangi, taraifa hizo zinaenezwa na viongozi wa kaunti hiyo baada yake kuwazuia kunyakua ardhi ya umma na kufuja fedha umma kupitia tenda. Imetayarishwa […]

KIJANA MMOJA AFARIKI WAKATI WA USAJILI WA MAKURUTU

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na miwili ameripotiwa kufariki wakati wa zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na jeshi katika eneo la chwele, kaunti ndogo ya kabuchai. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa bungoma, David saina, kijana huyo, ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha masinde muliro huko kakamega, alizirai wakati wa tathmini ya udhibiti wa mwili na alithibitishwa […]

WAHADHIRI WAKATAA KUSITISHA MGOMO

Wahadhiri katika chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret wamesema wataendelea na mgomo hadi pale matakwa yao yatakapo tekelezwa. Mgomo huo  sasa umekuwepo kwa zaidi ya siku 30 huku wanafunzi wakiendelea kusubiri kwa matumaini kuwa mgomo huo utafikia kikomo hivi karibuni. Imetayarishwa na Jones Koikai

UASIN GISHU KIVUTIO KIKUBWA BIASHARA NDOGO

Kaunti ya Uasin Gishu imeibuka kuwa kitengo cha ugatuzi chenye urafiki zaidi wa kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo nchini, kinachofanya vizuri zaidi katika jiji la Nairobi, kulingana na ripoti mpya ya Viffa Consult. Kitengo cha Usaidizi wa Biashara cha Kaunti nchini kinaiweka Uasin Gishu kileleni kwa alama ya jumla ya asilimia 87, ikifuatwa na Machakos (asilimia […]

LIVERPOOL WAMEKUNG’UTA VUMBI, CHELSEA NA MADRID WASHINDA

Mshambulizi wa Liverpool Hugo Ekitike alifunga dhidi ya timu yake ya zamani jana usiku Liverpool ilipoweka kando masaibu yao na kuizaba Eintracht Frankfurt mabao 5-1 katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya. Mabingwa hao watetezi wa EPL waliingia mechezoni wakiwa wamepoteza mechi 4 mfululuzo, kikiwemo kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Galatasaray katika mechi ya […]

KLABU ZA KPL, NSL YAJIIMARISHA LIGI INAPOREJELEWA

Klabu ya Naivas FC inalenga kuendeleza msururu wa kutopoteza mechi katika ligi ya NSL msimu huu watakapomenyana na Mwatate United Jumamosi hii jijini Nairobi. Klabu hiyo imeanza kampeni yake kwa kishindo, ikipata ushindi mara 2 na kutoka sare katika mechi 1 mwanzoni mwa msimu, matokeo ambayo yamewaweka katika nafasi ya 3 kwa pointi 7. Kocha […]

AFANDE WAWASILI LIBYA KWA CAF

Klabu ya Police FC imewasili nchini Libya tayari kwa mechi muhimu dhidi ya Al- Hilal ya Sudan katika mechi ya marudiano ya awamu ya mwisho ya kufuzu katika awamu ya makundi ya mechi za klabu bingwa barani Afrika CAF. Polisi wana kibarua cha kupindua meza baada ya kukubali kichapo cha bao 1:0 nyumbani Ijumaa iliyopita, […]

KNCHR YAONYA KUHUSU KEJELI

Tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu KNCHR imewaonya wakenya dhidi ya kuwakejeli watu walio na changamoto za kimaumbile ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Kulingana na tume hiyo, watakaopatikana na hatia hiyo watatozwa faini ya shilingi milioni 1 au kifungo kischozidi mwaka mmoja au yote mawili. Onyo […]

MASWALI KUHUSU MALIPO YA 77M KUSAKA 13M NHIF

Kamati ya uhasibu wa umma katika bunge la seneti imeibua hofu kuhusu malipo ya juu yaliyotolewa kwa mawakili katika bima ya zamani NHIF katika kipindi cha mwaka wa kifedha wa 2020-21, shilingi milioni 77 zikiripotiwa kutolewa katika kesi ya kurejesha shilingi milioni 13. Hofu hiyo iliibuliwa kwenye kikao na afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya […]