STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON

Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets imezidisha maandalizi yake ya mchuano kati yao na wenzao wa Gambia katika safari ya kuelekea mashindano ya kombe la wanawake la ubingwa wa bara Afrika WAFCON. Awamu ya kwanza ya mechi hiyo itaandaliwa Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nyayo, kabla ya marudiano tarehe 28 katika uwanja […]

FKF YAFUTILIA MBALI LIGI KWA SIKU 7

Shirikisho la soka nchini FKF limefutilia mbali ratiba za mechi zote za ligi nchini wakati wa kipindi cha siku 7 za maombolezo ili kumuenzi Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Kupitia taarifa, katibu mkuu wa FKF Harold Ndege amesema kuwa mecho zote za ligi kuu KPL, NSL kwa wanaume kwa wanawake na zile za mashinani […]

WAKENYA WAMIMINIKA JKIA

Huzuni imetanda katika uwanja waw a ndege wa kimataifa JKIA ambako maelfu ya wakenya wamewasili kusubiri mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Wengi wa waliowasili wameonekana wakitokwa na machozi, baadhi wakiwa wamevalia nguo zenye picha ya kinara huyo wa ODM. Matayarisho yanaendelea katika maeneo mbali mbali ambako mwili wa Odinga utapelekwa hii leo […]

OBURU ATEULIWA KUONGOZA ODM

Chama cha ODM kimemteua snenta wa Siaya Dakta Oburu Odinga kuwa kaimu kinara wa chama hicho kufuatia kifo cha kakae mdogo Raila Odinga aliyekuwa kinara wa chama hicho. Katika mkutano wa baraza kuu la chama mapema leo,  ODM kwa kauli moja imekubali kwamba Oburu achukue uongozi wa chama hadi kamati ya uchaguzi itakapokaa tena kutoa […]

MWILI WA ODINGA WAWASILI JKIA

Ndege ya RAO001 iliyobeba mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA dakika chache zilizopita, siku moja baada ya kifo chake nchini India. Viongozi mashuhuri wakiongozwa na rais William Ruto, naibu wake Kithure Kindiki, rais mstaafu Uhuru Kenyatta, mawaziri na viongozi wengine wakuu kutoka mirengo yote ya […]

MAOMBOLEZO YA BABA

Ulimwengu umejiunga na Kenya kuomboleza kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliyefariki hapo jana, viongozi wa mataifa na taasisi mbali mbali za dunia wakituma risala za rambi rambi. Waziri mkuu wa India, Narendra Modi amemtaja Odinga kama mnara wa taifa na rafiki wa India, akimkumbuka kwa juhudi zake za kuimarisha ushirikiano kati ya […]

ODINGA KUZIKWA JUMAPILI

Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga atazikwa Jumapili hii nyumbani kwake katika shamba la Opoda, eneo bunge la Bondo kaunti ya Siaya. Haya ni kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati ya kitaifa inayoongoza mipango ya mazishi, chini ya uongozi wa Naibu rais Kithure Kindiki. Kindiki amekariri tangazo la Rais William Ruto kwamba mazishi ya […]

ODINGA KUREJESHWA NCHINI LEO

Mwili wa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye pia ni kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, unatarajiwa kuwasili katika uwanja wa JKIA jijini Nairobi majira ya 8:30 asubuhi hii kutoka Mumbai nchini India. Vikosi vya wanajeshi tayari vimewasili katika uwanja huo kwa matayarisho ya kuupokea ujumbe maalum ukiongozwa na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi […]

BUNGE KUMWOMBOLEZA ODINGA ALHAMISI

Bunge limetenga vikao vya leo kumwomboleza waziri mkuu wa zamani Raila Odinga aliyefariki mapema jana kutokana na matatizo ya moyo alipokuwa akifanya matembezi ya asubuhi nchini India alikokuwa akitibiwa. Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, amesema vikao hivyo vitaanza saa nne asubuhi hadi usiku, ili kuwapa wabunge fursa ya kumkumbuka Odinga kwa mchango wake […]

SERIKALI YATANGAZA IJUMAA KUWA HOLIDEI

Serikali imetangaza kesho tarehe 17 kuwa siku ya likizo kwa taifa ili kuwapa wakenya fursa ya kuomboleza kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Kupitia notisi, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kumuenzi Odinga. Sherehe za kitaifa kuhusu mazishi ya kitaifa ya Odinga zitafanyika katika uwanja wa Nyayo […]