NAIROBI UNITED WAZIDI KUANGUSHA MIAMBA

Klabu ya Nairobi United inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini KPL imeendelea kuvunja vizuizi na kujitangaza katika majukwaa ya kimataifa, baada ya kupata ushindi muhimu wa mabao 2:0 nyumbani dhidi ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia katika mkondo wa kwanza wa awamu ya mwisho ya mwondoano wa mechi za mashirikisho ya bara yaani CAF […]

ZANU-PF KUONGEZA MUHULA WA RAIS MNANGAGWA

Mrengo wa Upinzani nchini Zimbabwe umepinga pendekezo la chama tawala ZANU-PF kuifanyia marekebisho katiba ili kuongeza muhula wa rais Emerson Mnangagwa kwa kipindi cha miaka 2. Pendekezo hilo liliafikiwa Jumamosi iliyopita kwenye kongamano la chama hicho, na iwapo litapitishwa, Mnangagwa mwenye umri wa miaka 83 ataongoza hadi mwaka wa 2030. Hata hivyo, mojawapo wa viongozi […]

MNARA WA BABELI ODM

Katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna na gavana wa Siaya James Orengo wamependekeza mkabata wa maelewano kati ya chama hicho na UDA kuangaziwa upya, wakisisitiza kuwa ODM itamwidhinisha mgombeaji wake katika uchaguzi mkuu ujao. Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa kinara wa chama hicho Raila Odinga, msimamo wao ukitofautiana na viongozi […]

RUTO AWEKA WAZI AFYA YA ODINGA KABLA YA KIFO

Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga alianza kuwa na changamoto za kiafya takribani miezi 2 iliyopita kabla ya kuafikiana na familia kwamba asafarishwe nchini India kwa matibabu. Haya ni kwa mujibu Rais William Ruto aliyezungumza hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu hali ya afya ya Odinga wakati wa hafla ya mazishi ya kinara huyo wa […]

KENYA KUADHIMISHA MASHUJAA

Serikali imethibitisha kwamba maadhimisho ya sherehe za Mashujaa zinafanyika hii leo licha ya taifa kuendelea na kipindi cha maombolezo ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amewataka wakenya kujitokeza kwa wingi kuadhimisha sherehe hizo zitakazoongozwa na Rais William Ruto katika uwanja wa Ithookwe kaunti […]

BENKI ZINATARAJIA MAHITAJI YA CHINI YA MKOPO KAMA MAPATO YANAYOWEZA KUTUMIKA YANAPUNGUA

Asilimia kubwa ya Benki nchini zinatarajia mahitaji hafifu ya mikopo kati ya mwezi Oktoba na mwezi Novemba mwaka huu, kufuatia ripoti inayonukuu utafiti wa Benki Kuu ya Kenya (CBK). Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 67 ya benki zinatarajia mahitaji ya chini au ya chini sana ya mkopo katika kipindi hiki—chini kutoka asilimia 81 katika miezi miwili iliyopita wakati wakopeshaji wengi walitarajia mahitaji ya wastani hadi makubwa. […]

MUSYOKA AKATIZA ZIARA UINGEREZA, AREJEA

Aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka ambaye ni kinara wa Wiper, amelazimika kukatiza ziara yake ya siku 10 nchini Uingereza na kurejea nchini mapema leo kutokana na kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Akiwahutubia wanahabari baada ya kuwasili katika uwanja wa JKIA, Musyoka ameeleza kushtushwa na kifo cha Odinga, ambaye amekuwa mshirika wake […]

WAKENYA WAOMBOLEZA ODINGA NYAYO

Hali ya huzuni imetanda kwa muda katika uwanja wa michezo wa Nyayo, wakenya wakitokwa na machozi wakati mwili wa Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umewasili kwa ajili ya ibada ya kitaifa ya mazishi. Baadhi ya waombolezaji walisimama pembeni pa barabara ambako mwili wa Odinga ulipita kutia kutoka majengo ya bunge la kitaifa wakipunga vijibendera […]

WAKUU WA MATAIFA WAWASILI NYAYO

Wageni  mashuhuri wamefika katika uwanja wa michezo wa Nyayo kuhudhuria ibada ya kitaifa ya mazishi ya aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga inayoendelea kwa sasa. Miongoni mwao ni rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete na makamu wa rais Philip Mpango, ambao wamepokelewa katika uwanja wa JKIA na alieyekuwa makamu wa rais wa Kenya Kalonzo Musyoka. […]

RUTO, UHURU WAKUTANA NYAYO

Viongozi wakuu nchini na kimataifa wakiongozwa na Rais William Ruto, naibu wake Kithure Kindiki, Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, jaji mkuu Martha Koome na uongozi wabunge wamejiunga na maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa Nyayo ambako ibada ya kitaifa ya mazishi ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga inaendelea. Rais Ruto alitangulia kuwaongoza viongozi wengine kuutazama […]