UPDF YAKANA KUWAZUILIA NJAGI, OYOO

Utata umeendelea kuibuka kuhusu waliko wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo baada ya jeshi la ulinzi la Uganda UPDF kukana kuwazuilia wawili hao walioripotiwa kutekwa nyara nchini Uganda yapata mwezi mmoja uliopita. Kwenye taarifa yake kwa mahakama, UPDF imesema kwamba imeendesha uchunguzi na msako katika vituo vyote vya kuwazuilia washukiwa ila hakuna taarifa kuhusu wawili […]

ODM YASHINIKIZA KAHIGA AKAMATWE

Matamshi ya gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga yaliyoonekana kusherehekea kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga yamechukua mkondo tofauti, chama cha ODM sasa kikitaka akamatwe kwa misingi kwamba matamshi hayo ni sawa na uchochezi wa kikabila. Mwenyekiti wa chama hicho Gladys Wanga, na naibu kinara Simba Arati wamehofia uwezekano wa matamshi hayo kuvuruga mshikamano […]

POLISI ‘WAHALIFU’ WAKAMATWA

Maafisa wa DCI wanatarajiwa kuwafikisha mahakamani hii leo washukiwa 4 wakiwemo maafisa wa zamani na wa sasa wa polisi wanaohusishwa na visa vya utekaji nyara na wizi wa kimabavu jijini Nairobi. Mmoja wa washukiwa Cleophas Wambua aliyekuwa akihudumu kama afisa wa polisi katika kaunti ya Homa Bay, alinaswa hapo jana mafichoni eneo la Kitengela akiwa […]

MVUA KUBWA KUANZA LEO, IDARA YAONYA

Umetakiwa kuchukua tahadhari kuhusu mvua kubwa katika maeneo mbali mbali kuanzia leo, ambao ndio mwanzo wa kipindi kifupi cha mvua ya Oktoba- Novemba kuelekea Disemba. Katika taarifa, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua inayoshuhudiwa katika maeneo ya Ziwa Victoria, Rift Valley, nyanda za juu za Magharibi mwa Rift valley inatarajiwa kuonhezeka ndani […]

AFUENI KWA WANAFUNZI WA KAUNTI YA TURKANA BAADA YA UJENZI WA MADARASA

wanafunzi wa shule ya msingi ya kalokol kaunti ya turkana wamepata afueni baada ya  kampuni ya  kenya pipeline kuwajengea madarasa mapya matatu. Hii ni baada ya shule hiyo kusombwa na maji baada ya ziwa turkana kufurika kusababisha wanafunzi kusongamana  kwenye madarasa  na sasa madarasa hayo sasa yanatazamiwa kutumika kufanyia mitihani wa kitaifa. Imetayarishwa na Jones Koikai

GAVANA WA NYERI AOMBA MSAMAHA

Gavana wa kaunti ya nyeri mutahi kahiga ameiomba familia ya odinga msamaha na kusema kwamba matamshi yake hayakuwa ya kukejeli kifo chake hatua ambayo imevutia hisia kali kutoka kwa wananchi. Hata hivyo kutokana na tukio hilo , amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wake kama naibu mwenyekiti wa baraza la magavana.   . Amesisitiza kwamba matamshi yake ya hapo jana yalikuwa yake binafsi na wala sio matamshi yanayowakilisha […]

SERIKALI KUANZISHA USHURU MPYA WA MAFUTA, UMEME

Wakenya katika siku zijazo huenda wakalazimika kulipa ushuru mpya wa mafuta na umeme huku serikali ikichukua hatua ya kuanzisha Hazina ya Kawi Shirikishi (CEF) ili kufadhili miradi muhimu ya kawi na kupunguza utegemezi wa mikopo. Kulingana na Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, hazina hiyo itachukua michango kutoka kwa wadau wa sekta ya nishati pamoja na mgao wa […]

GAVANA KAHIGA AJIUZULU

Gavana Nyeri Mutahi Kahiga amejiuzulu kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa baraza la magavana kutokana na shutuma dhidi yake kuhusiana na kauli zake zinazoonekana kusherehekea kifo cha Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. Kupitia taarifa, Kahiga amejutia kauli zake na kuomba msamaha kwa familia ya Odinga, chama cha ODM, magavana wenzake na jamii ya eneo zima […]

HAALAND HASHIKIKI TENA

Erling Haaland alifunga mara ya 12 mfululizo jana usiku na kuisaidia klabu yake ya Manchester City kupata ushindi kwa mara ya kwanza ugenini katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kwenye mashindano ya bara Ulaya. Bao la fowadi huyo raia wa Norway na nahodha Bernado Silva yaliihakikishia City ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Villareal […]

GYOKERES AKATA KIU CHA MAGOLI

Mshambulizi wa klabu ya Arsenal Viktor Gyokeres alifunga mara 2 katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mechi ya klabu bingwa barani Ulaya, na kumaliza ukame wake mbele ya lango tangu kuwasili Emirates mwanzoni mwa msimu huu. Gabriel Magalhaes na Gabriel Martinelli walifungua mvua ya magoli kabla ya Gyokeres kuhakikisha kuwa Arsenal wanapata ushindi katika […]