CAPE VERDE YAFUZU KOMBE LA DUNIA MBELE YA CAMEROON

Timu ya taifa ya Cape Verde imefuzu mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kumaliza kileleni mwa kundi D, alama 4 mbele ya miamba wa soka barani Afrika Cameroon kwa alama 23. Blue Sharks walikamilisha kampeni yao jana usiku kwa kuwanyuga Eswatini magoli 3:0, mabao ya Dailon Livramento, Willy […]

ODM YAPATA PAA MAGARINI

Chama cha ODM kimepigwa jeki katika uchaguzi mdogo wa Magarini kaunti ya Kilifi baada ya mwaniaji wa kiti hicho kupitia chama cha PAA Michael Kingi kujiondoa ili kumuunga mkono mwaniaji wa ODM Harrison Kombe. Kupitia taarifa, PAA imesema kujiondoa kwa Kingi kumetokana na mashauriano na viongozi wengine waliojumuishwa kwenye serikali jumuishi. Aidha, PAA imesema uamuzi […]

WAHADHIRI WASHIKILIA MGOMO UTAENDELEA

Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma umeingia siku yake ya 29 hii leo huku wahadhiri hao wakishikilia kuwa wataendelea kugoma hadi serikali iwalipe shilingi bilioni 7.9 wanazodai Haya yanajiri baada ya mazungumzo baina yao na wizara ya elimu kuendelea kukosa mwafaka, huku Waziri wa elimu Julius Ogamba akisema huenda suluhu ikapatikana baadaye wiki […]

IPOA YASHUTUMU UVAMIZI DHIDI YA POLISI

Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA imeshtumu ongezeko la visa vya kuvamiwa kwa maafisa wa polisi na raia, kisa cha hivi punde kikiwa cha jana ambapo afisa wa GSU alishambuliwa na kuuawa kwa mshale katika lango la Ikulu ya rais jijini Nairobi. Afisa mwingine aliuawa nje ya uwanja wa ndege wa Jomo […]

KMPDU YATAKA KIAMBU IVUNJILIWE MBALI

Mgomo wa madaktari katika kaunti ya Kiambu umendelea kuibua maswali kuhusu uwezo wa serikali za kaunti kushughulikia masuala ya afya, madaktari kwenye kaunti hiyo wakisitisha huduma zao zote na kuanzisha mchakato wa kumtaka Rais William Ruto kuvunjilia mbali serikali ya kaunti hiyo. Kupitia muungano wao KMPDU, madaktari wameishutumu serikali ya kaunti ya Kiambu kwa madai […]

HAALAND AVUNJA REKODI ZAIDI

Hatriki ya Erling Haaland wikendi iliyopita iliiweka timu yake ya Norway katika nafasi nzuri ya kurejea tena katika mashindano ya kombe la dunia baada ya mara ya mwisho kushiriki mwaka wa 1998. Mshambulizi huyo wa Manchester City alifunga mabao 3 katika ushindi wa mabao 5:0 dhidi ya Israel. Kwa sasa Haaland amefunga bao katika mechi […]

MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA MOROCCO

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kwamba mashindano ya mwondoano kwa timu 4 zitakazomaliza katika nafasi ya pili bora kutoka makundi yote 9 kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu kombe la dunia yaani playoff yataandaliwa nchini Morocco kuanzia tarehe 13 hadi 16 mwezi ujao. Mshindi wa mashindano hayo atashiriki awamu ya mwondoano ya mabara ili kusaka […]

KAMPENI YA CAF KUKAMILIKA KESHO

Kampeni ya mataifa ya bara Afrika kuwania tiketi ya kufuzu kwa kipute cha Kombe la dunia mwaka ujao kitakamilika hapo kesho, wakati jumla ya mechi 17 zimesalia kabla ya kutamatika kwa kameni hiyo. Jumla ya mechi 8 zitachezwa hii leo katika makundi mbali mbali. Tayari timu za Algeria, Ghana, Morocco, Misri na Tunisia zimefunzu moja […]

TAJI BAADA YA TAJI KWA KIPYEGON

Bingwa mshikilizi wa rekodi ya dunia Faith Kipyegon ameendeleza umahiri wake uwanjani baada ya kunyakua taji lake la pili mfululizo kwenye mashindano ya Tiffany Athlos kwa mwendo wa kasi zaidi kuwahi kukimbiwa nchini Marekani. Mashindano ya Athlos huwajumuisha wanawake pekee yaliyozinduliwa Septemba mwaka jana jijini New York Marekani. Kipyegon alishinda mbio za mita 1,500 katika […]

BARABARA YA NJORO-MAU SUMMIT KUFUNGWA

Mamlaka ya kitaifa ya barabara kuu nchini imetangaza kufungwa kwa muda barabara ya Njoro- Mau summit ili kupisha kazi muhimu kwa ujenzi wa lami kufanyika . Kupitia tangazo la umma mamlaka hiyo imesema kuanzia tarehe 16 mwezi huu hadi tarehe 6 mwezi ujao, barabara hiyo itafungwa  huku madereva wanaotumia barabara hiyo wakishauriwa kutumia barabara ya Kibunja kama […]