POLICE FC WATEGEMEA UAMUZI WA CAF

Klabu ya Al Hilal Omdurman imepuzilia mbali madai ya Police FC ya Kenya kwamba klabu hiyo ya Sudan iliwachezesha wachezaji wasiofaa katika mkondoo wa pili wa kufuzu awamu ya makundi ya mashindano ya klabu bingwa barani Afrika. Kwenye taarifa, Omdurman ambayo iliwabandua Police FC, imeyataja madai hayo kuwa yasiyo na msingi. Miongoni mwa malalamishi ambayo […]

NYOTA YA STARLETS KUANGAZA BARANI

Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets imefuzu mashindano ya wanawake ya taifa bingwa barani Afrika WAFCON mwaka ujao, baada ya kuwalaza Gambia bao 1:0 hapo jana nchini Senegal na hivyo kuwabwaga kwa jumla ya mabao 4:1. Baada ya makabiliano katika kipindi cha kwanza bila mafanikio kwa timu zote, Mwanahalima Adam Jereko aliwapa Starlets bao la pekee […]

WANAHARAKATI WAKEJELI ‘MAIGIZO’ TANZANIA

Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi wa urais hii leo, huku mashirika ya kutetea haki za kidemokrasia yakimkosoa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa madai ya ukiukaji wa haki hizo kutokana na hatua yake ya kuwafungia nje wawaniaji wa upinzani. Wakiongozwa na kiongozi wa chama cha PLP Martha Karua, wameutaja uchaguzi huo kuwa maigizo na wala […]

EACC YAREJESHA ARDHI YA WAZIRI KARURA

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imeimarisha vita dhidi ya unyakuzi wa ardhi nchini, baada ya kufanikiwa kurejesha vipande kadhaa vya ardhi vyenye thamani ya mabilioni ya pesa katika maeneo mbali mbali nchini. Ya hivi punde ni ardhi ya umma yenye ekari 17 katika msitu wa Karura, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.8, ambayo […]

RUTO AWATAHADHARISHA MAJANGILI KASKAZINI

Rais William Ruto ametangaza kwamba serikali yake itarejesha utulivu katika kila eneo la taifa, na kuwaonya wamiliki wa silaha bila leseni kwamba chuma chao ki motoni. Akizungumza alipozuru eneo la bonde la ufa, Ruto amewataka wamiliki hao kuzisalimisha sialaha hizo mara moja la sivyo wapokonywe kisheria. Naye Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amesema tayari serikali […]

MAUAJI UON: DCI YAZIDISHA UCHUNGUZI

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wameimarisha uchunguzi dhidi ya mshukiwa wa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi Jane Atila, Nicholas Mutua, baada ya kuibuka kwamba mshukiwa anahusishwa na dhuluma dhidi ya waathiriwa zaidi. Kulingana na waathiriwa waliojitokeza hapo jana, mshukiwa aliwavamia na kuwatesa katika msitu wa KEFRI eneo la Kikuyu, akiwalazimisha wampe […]

WATU 11 WAMEFARIKI KUFUATIA AJALI YA NDEGE

Watu 11 wameripotiwa kufariki katika ajali ya ndege ambayo imeanguka katika eneo la tsimba-matuga eneo bunge la matuga kaunti ya Kwale. Ajali hiyo imethibitishwa na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini emile arao akisema kwamba ndege hiyo, nambari ya usajili 5y-cca, iliyokuwa na watalii ilikuwa ikielekea kichwa tembo maasai mara kutoka diani […]

MAHAKAMA YA MURANG’A YAHOFIA MSONGAMANO KWENYE MAGEREZA

Mahakama kuu ya Murang’a imeagiza  kuimarishwa kwa utendakazi kupitia mageuzi ya kidijitali hii ni kufuatia msongamano  unaozidi kuongezeka katika magereza mbalimbali katika kaunti hiyo. Akizungumza wakati wa hafla ya kutoa kompyuta na tarakilishi  kwa gereza la maranjau jaji wa mahakama kuu ya Murang’a Cecilia  Githua amesema mpango huo utahakikisha haki inatendeka kwa njia bora kwa kila mfungwa. Imetayarishwa na Jones Koikai

AFUENI  KWA WAFANYABIASHARA BAADA YA UJENZI WA BARABARA KUZINDULIWA NAKURU

Wafanyibiashara katika eneo bunge la Kuresoi North kaunti ya Nakuru wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Rais William Ruto kuzindua rasmi ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 12 ya Kinamba-Murinduku. Barabara hiyo inatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mazao, ikiwa ni pamoja na vitunguu, nyanya, pareto na mboga na wakati huo huo kuwaletea wakulima mapato kutokana na shughuli zao […]

CARABAO YAINGIA RAUNDI YA 4

Kipute cha Carabao kinaingia raundi ya 4 hii leo huku timu kama vile Manchester United, Everton na Aston Villa zikiwa zimebanduliwa nje ya mashindano hayo, nazo timu 5 pekee zilizo nje ya ligi kuu ziisalia. Klabu ya Grimsby Town inayoshiriki League 2 imekuwa kitovu cha gumzo kwenye mashindano hayo kufikia sasa, baada ya kuwabandua Manchester […]