KARUA AWATAKA WAKENYA KUTETEA HAKI ZAO

Kiongozi wa chama cha PLP, Martha Karua, ametoa wito kwa wakenya kutetea haki zao kikamilifu huku chama cha wanasheria nchini LSK  kikizindua wiki ya uhamasishaji wa kisheria 2025. Hafla hiyo ambayo imeanza hii leo na inatarajiwa kuamilika tarehe 31, 2025, ambapo zaidi ya  mawakili 18,000 wa Kenya wakitoa mashauriano ya kisheria bila malipo nchini kote. Karua ameangazia vikwazo vya kimfumo […]

WANNE WAFARIKI KWENYE MAANDAMANO CAMEROON

Watu wasiopungua 4 wameuawa kwenye maandamano katika kitovu cha uchumi jijini Douala nchini Cameroon huku baraza la kikatiba likijiandaa kutangaza matokeo ya urais hii leo. Kulingana na msimamizi wa eneo hilo Samuel Dieudonne Diboua, vituo vya polisi wamevamiwa na waandamanaji walio wafuasi wa mwaniaji wa upinzani Issa Tchiroma, na polisi walilazimika kutumia nguvu ili kujilinda. […]

BABU OWINO MAHAKAMANI KUPINGA SHERIA

Mbunge wa Embakasi East Babu Owino na mkenya mwingine kwa jina Mwaura Kabata, wamewasilisha kesi mahakamani kupinga sheria iliyopitishwa maajuzi kuhusiana na mgongana wa maslahi ama conflict of interest inayowaruhusu mawaziri kujihusisha na siasa. Kwenye kesi hiyo, walalamishi wanataka amri za muda kutolewa kufutilia mbali utekelezaji wa sehemu ya 25 ya sheria hiyo, wanayoitaja kuwa […]

ODM?: HUENDA TUKAJIONDAO SERIKALINI

Chama cha ODM kimesisitiza kuwa hakina makubaliano yoyote ya kisiasa na UDA, tofauti na madai kwamba ODM iliingia serikali baad ya kutiwa saini mkataba wa ushirikiano kati ya aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga na Rais William Ruto. Kwenye mahojiana na kituo kimoja cha habari nchini, naibu kinara wa ODM Abdulswamad Nassir, amesema chama hicho […]

KTDA YASIMAMISHA SHUGHULI ZA USAFIRI NA MAFUNZO YA WAFANYAKAZI

Mamlaka ya ustawi wa kilimo cha majani chai KTDA imesimamisha safari zote za wafanyakazi, mikutano ya nje, na shughuli za mafunzo katika kampuni zake tanzu kama sehemu ya udhibiti wa gharama na utawala. Katika ripoti ya ndani iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Wilson Muthaura, uamuzi huo ulielekezwa na Bodi ya Biashara kuunga mkono kipaumbele kinachoendelea cha utawala, utiifu na usimamizi wa […]

EZE AIPA ARSENAL HATAMU, BRENTFORD IKIZIDISHA MASAIBU ANFIELD

Kiungo wa Arsenal Eberechi Eze aliifungia Arsenal bao lake kwanza la msimu tangu kuigura klabu ya Crystal Palace, na kuihakikishia Arsenal ushindi mwembamba na muhimu wa bao 1:0 dhidi ya klabu hiyo. Ushindi wa Arsenal umeimarisha uongozi wao wa ligi kuu ya Uingereza, hasa baada ya washindani wao Chelsea, Manchester City na bingwa mtetezi Liverpool […]

NAIROBI UNITED WAANDIKISHA TAARIFA

Klabu ya soka ya Nairobi United inayoshiriki ligi kuu ya soka KPL imeandikisha ukurasa mpya katika historia ya soka nchini baada ya kuwa klabu ya kwanza kuingia awamu ya makundi katika mashindano ya ubingwa wa mashirikisho ya mabara ya CAF yaani CAF Confederations Cup katika jaribio la kwanza. Naibois, jinsi wanavyofahamika kwa jina la utani, […]

HARAMBEE STARLETS WAIMARISHA MAANDALIZI

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets inajiandaa kwa mkondo wa marudiano wa mechi ya kufuzu katika mashindano ya ubingwa wa wanawake bara Afrika WAFCON dhidi ya Gambia hapo kesho. Starlets wataingia kwenye mechi hiyo wakihitaji angalau sare ya aina yoyote ili kufuzu, baada ya kupata ushindi wa mabao 3:1 katika mkondo wa […]

WETANG’ULA ATETEA SHERIA YA KOMPYUTA

Viongozi wanaoegemea mrengo wa Kenya Kwanza wametetea sheria mpya kuhusu matumizi mabaya ya kompyuta na uhalifu wa kimtandao ya mwaka 2025, wakisema sheria hiyo inalenga kulinda walichotaja kuwa ustawi wa jamii. Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wakiongozwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, na kiongozi wa […]

MITIHANI YA KPSEA, KJSEA WAANZA

Mamilioni ya watahiwa wa grade 6 na grade 9 wameratbiwa kuanza mitihani yao ya KPSEA na KJSEA asubuhi hii huku serikali ikitoa hakikisho kuwa mipango na mikakati yote ya kufanikisha mitihani hiyo imekamilika. Mtihani wa KJSEA ambao ni wa grade 9 mwaka huu ni wa kwanza kabisa chini ya mtaala wa umilisi CBE. Waziri wa […]